Surat al jini iliyotafsiriwa kiswahili

"Majini ni viumbe kama sisi tena wanamuabudu Allah" alisikika ustadh mmoja akisema
Ni kweli kuna tofauti kubwa kati ya Jini na shetani ...
Jini anaweza kuwa shetani kama vile binadamu anaweza kuwa shetani ukimuasi Allah
 
Nataka kuyatumia majini wazuri
Ukishamuita na ukamtumia huyo keshakuwa shetani ... Yale majini yanoyopanda vichwani mwa watu ni mashetani .. jini ana mipaka yake amewekewa hatakiwi kuingilia maisha ya binadamu..basi pale anapoingilia ameshakuwa shatani
 
Wako baadhi ya mashehe wanawatumia majina kwa kazi zao
 
So zile amri kumi aliandika nani.
 
Jini tena yupo kwenye kitabu cha Allah ?
Tatizo kubwa mlilonalo nyinyi ni uelewa! unaamini umefahamu kitu wakati umeifunga milango yako ya ufahamu. Huwezi kumfahamu jirani uliyenaye sasa kwa kutumia taarifa za jirani yako wa zamani. Hii ni sawa na ile hadithi ya yule kipofu aliyeona mara moja tu maishani mwake na alichokiona ni jogoo tu, sasa kila kizuri anachoambiwa yeye anabakia "kama jogoo!?" "kama jogoo!?"

Kitu mnachopaswa kuelewa ni kwamba kile mlichofundishwa kanisani kwamba jini ni malaika walioasi ni tofauti na kile kinachofundishwa msikitini. Sisi waislamu hatuamini kama jini aliwahi kuwa malaika hata siku moja. Jini ni kiumbe, malaika ni kiumbe, na Binadamu ni kiume na wote hawa watatu ni viumbe wa tofauti baina ya mmoja na mwengine. Ukishaliingiza hili akilini sasa ndo utaanza kuelewa mafundisho ya Uislamu yanasema nini kuhusu hivi viumbe vinaitwa majini.

kama umeelewa hapo juu sasa tuendelee.

Ukishangaa kuwepo majini wema na waovu pia naomba ushangae kuwepo wanadamu wema na waovu, kwa kuwa wote hawa ni viumbe dhalili kabisa wa Allah na yeye ndo aliyewaumba, na wote wameumbwa ili wamuabudu yeye tu. Tofauti ya malaika na hawa viumbe wawili ni kwamba malaika hawatendi dhambi na ndo maana hujawahi kusikiwa malaika watakuwa rewarded kwa matendo yao mema au labda wataadhibiwa iwapo watafanya madhambi (hii haipo kwenye mjadala kabisa), hakuna malaika anatenda maovu.

Turudi katika hiyo Suratul Jinn. kwanini msisome kitu na kukijua kinasemaje kabla ya kuchangia mada ukiwa bado ni mjinga wa unachokichangia? mmeaminishwa kwa kutishwa na mambo ya ajabu sana.
Hii sura anaambiwa mtume yale waliokuwa wakisema majini baada ya kumsikia yeye akisoma Quran, na kwamba kutokana na hiyo Quran walioisikia wameongoka baadhi yao kutoka katika maovu waliyokuwa wakitenda. Na pia Allah anamuelezea Mtume (pamoja na wasomaji wote wa Quran) pale majini waliposema na kushangaa juu ya upotevu wa baadhi ya watu waliojikinga kwa kuwatumainia hao majini ilhali hakuna wanachopata zaidi ya kuongezewa mzigo na upotofu.

Mi niwaombe ndugu zetu wakristo mujielimishe kwanza. Acheni hadithi za kuogopa jinamizi usiku kama watoto wadogo.
 
Minataka jini ili nipate utajiri nisaidie tafadhali niko tayari kuyafuga
 
Aliyetaka Surat Jinn hiyo imeshawekwa kazi kwake kusoma,
 
Minataka jini ili nipate utajiri nisaidie tafadhali niko tayari kuyafuga
Hakuna mtu anafuga majini, mnadanganywa! hao mnaodhani wanafuga majini wao ndo watumwa wa hao majini!

Sasa basi kama unataka kuwa mtumwa wa majini basi nenda katafute washirikina wakuongezee mzigo (Surah Jinn aya ya 6)
 
Ni kweli kuna tofauti kubwa kati ya Jini na shetani ...
Jini anaweza kuwa shetani kama vile binadamu anaweza kuwa shetani ukimuasi Allah
Kwahiyo wewe hapo hujawahi kumuasi Allah? kwahiyo wewe ni shetani.kwahiyo kumbe hakuna shetani kama shetani ila kila tu anayefanya dhambi ndio anageuka na kuwa shetani

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mtu anafuga majini, mnadanganywa! hao mnaodhani wanafuga majini wao ndo watumwa wa hao majini!

Sasa basi kama unataka kuwa mtumwa wa majini basi nenda katafute washirikina wakuongezee mzigo (Surah Jinn aya ya 6)
Kuna shehe wa msikiti sitautaja jina ameniambia atanisaidia ni kazi ndogo sana
 
Hakuna mtu anafuga majini, mnadanganywa! hao mnaodhani wanafuga majini wao ndo watumwa wa hao majini!

Sasa basi kama unataka kuwa mtumwa wa majini basi nenda katafute washirikina wakuongezee mzigo (Surah Jinn aya ya 6)
Kuna bibi jirani alikua anapandisha majini mpaka shehe anakuja kuyatuliza
Nikukumbushe wako waislamu ni ndugu zetu mambo mengine tunaona hatuadisiwi
 
Kuna bibi jirani alikua anapandisha majini mpaka shehe anakuja kuyatuliza
Nikukumbushe wako waislamu ni ndugu zetu mambo mengine tunaona hatuadisiwi
Mwambie huyo bibi jirani yako atafute shekhe wa kweli amtoe hayo mashetani! kama yanatulizwa sio shekhe huyo ndo walewale wavaa makoti ya kidaktari Muhimbili kumbe matapeli.
 
Mwambie huyo bibi jirani yako atafute shekhe wa kweli amtoe hayo mashetani! kama yanatulizwa sio shekhe huyo ndo walewale wavaa makoti ya kidaktari Muhimbili kumbe matapeli.
Shehe ambaye ni imam wa msikitini unasema tapeli ndo aliyeniambia kuna namna ya kuwatumia
 
Mwambie huyo bibi jirani yako atafute shekhe wa kweli amtoe hayo mashetani! kama yanatulizwa sio shekhe huyo ndo walewale wavaa makoti ya kidaktari Muhimbili kumbe matapeli.
Huyo ni shekhe wa kweli na ni imamu wa msikiti sitaki niutaje kwa sababu sio vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…