Swala la ardhi ya Bagamoyo ni strategy ya kisiasa tu, lakini kiuhalisia serikali ya Zanzibar haimaanishi kile ilichoongea

Duh... Mkuu Mr Dudumizi , kauli huumba, lisemwalo lipo!, tembelea hapa uone mimi nilisema nini Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Kwa faida ya wavivu wa kufollow links

P
Asante mkuu Pascal Mayalla nimesoma ulichoandika na kuelewa vizuri utabiri wako.

Kifupi mimi nimekuwa nikifuatilia san michango yako toka miaka hiyo.

Na hata ulipotabiri ujio wa hayati Magufuli kuwa raisi, nilisoma uzi ule, nilichangia comment na ku Like pia.

Pamoja sana P
 
Ila JPM alikosea sana kumteua yule kuwa mgombea mwenza, au katiba hakuisoma vizuri? Au ndo ilikua lazima kuweka usawa??
 
Kwa hiyo unamaanisha tusiogope kauli isiyo na ushahidi, muhimu kwanza wangetuambia hizo ekari zinaanzia wapi na kuishia wapi ndio tuanze kulalamika tukishahakikisha?

Mimi niliamini ile kauli kwasababu ya huyu mzanzibari tuliyenaye huku Bara, anayeonekana "kupakumbuka" sana kwao wakati huu, hasa nikikumbuka ule msamaha wa deni la Tanesco kwa Zanzibar juzi tu
Hahaha huyu wa bara ni jamii ile ile ya kina Mwinyi ambao wazazi au babu zao walikwenda kule kwa nia ya elimu akhera na kulowea huko.

Laiti angekuwa yule mwenyewe kabisa wa ndani ndani basi hiyo nafasi aliyonayo leo huku bara isingekuwa yake.

Kinachofanyika ni kumtengenezea njia mdogo wake ili hiyo 2025 katika kura ya maoni akutane na njia nyeupee.

Lkn kiuhalisia namba 1 tulienae huku ni mdigo wa Tanga.
 
Kuwa na uwezo au vinginevyo, wewe amini tu huu ni upepo uliofunguliwa kwa sababu maalum. Ukishapita watu wataendelea na maisha yao bila kusikia tena habari ya ardhi hiyo ya Bagamoyo.
Hao jamaa inasemekana ardhi ni ya kwao toka enzi za Nyerere afu wewe unasema eti ni tolii.
 
Habari zenu wana JF wenzangu,

Kuna mshituko mkubwa umetukumba watanganyika, hasa kuhusu hili swala la serikali ya Zanzibar kudai kuwa ina eneo lake la ardhi huko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kama ilivyo kawaida ya baadhi yetu, huwa hatukurupuki kulalamika bila kufuatilia kwa makini kina cha kile kilichoongelewa na serikali au mtu husika.

Ukweli ni kwamba hili swala limetumiwa kisiasa makusudi na namba 1 wa huko, ili aweze ku win kiurahisi katika mbio za kumchagua mgombea uraisi wa nchi hiyo kupitia chama anachotokea, na vile vile kupita katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika miaka miwili tu ijayo.

Ikumbukwe kwamba namba 1 huyo babu zake ni wandengereko wa Mkuranga mkoani Pwani, ambapo baba yake mwenyewe alieleza kwamba alipelekwa katika kisiwa hicho na wazazi wake ili akajifunze elimu akhera na baadae kurudi mkuranga kuendelea na mambo mengine.

Ila kwa bahati mbaya au nzuri baba huyo alipofika huko, akaongeza na elimu dunia na mwisho wake kulowea huko hadi kuwa namba 1 wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Sasa namba 1 wa sasa historia anaijua na kamwe hawezi kufanya mzaha wa kumega palipo asili yake, huku akijua kwamba huenda na yeye ikatokea siku 1 akawa namba 1 tena wa JMT kama ilivyotokea kwa baba yake.

Kuna msemo wa waingereza unasema "Home sweet Home" na ndio maana namba 1 huyo miaka yake yote ya siasani hakuwa kugombea huko alipo sasa, bali alikuwa anagombea kule ilipo asili yake (mkuranga)

Sasa kwa vile amezungukwa na wazalendo uchwara wa Zanzibar ambao wengi wao wanaonesha chuki ya dhahiri kwake kama mzanzibar-mtanganyika na Tanganyika yetu kwa ujumla. Basi ndo akaja na style ya kuwafubaza kwa kile wapendacho kukisikia ili iwe rahisi kuchagulika kwa kuamini kwamba namba 1 huyo yuko pamoja na wao katika kupigania masilahi ya kisiwa chao.

Mnaofikiri kuwa Bagamoyo itamegwa chini ya namba 1 huyu wa sasa basi mtasubiri sana na ukizingatia hata huyu wa Muungano nae asili yake ni huko udigoni Tanga. Maana angekuwa original wa kule kisiwani, kamwe asingepewa nchi kama ilivyokuwa kwa kina dr SAS alienyang'anywa tonge mdomoni na mzee rukhsa kwa sababu ya kile nilichoeleza hapo juu.

Karibuni kwa kuchangia kistaarab.

Tanganyika nitakupenda mpaka kufa.
Suali kwani watu hawaruhusiwi kumiliki Ardhi Tanzania?
Ikiwa matajiri au watu wakigeni wana ruhusiwa kumiliki ardhi kwanini iwe viroja SMZ kumiliki Ardhi?
 
Katika siasa kila mtu anaweza kuongea lolote, lkn inapokuja swala la utekelezaji mambo huwa zero.

Hakuna nchi au mtu anaeweza kumega ardhi halali ya Tanganyiko.

Hili hata Malawi au Idi Amin huko alipo analijua, sembuse Kazanzibar
Umemwambia sahihi yaani ukitaka kutolewa fasta hata kufa jimix mega ardhi yetu uone Cha mtema Kuni
 
Habari zenu wana JF wenzangu,

Kuna mshituko mkubwa umetukumba watanganyika, hasa kuhusu hili swala la serikali ya Zanzibar kudai kuwa ina eneo lake la ardhi huko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kama ilivyo kawaida ya baadhi yetu, huwa hatukurupuki kulalamika bila kufuatilia kwa makini kina cha kile kilichoongelewa na serikali au mtu husika.

Ukweli ni kwamba hili swala limetumiwa kisiasa makusudi na namba 1 wa huko, ili aweze ku win kiurahisi katika mbio za kumchagua mgombea uraisi wa nchi hiyo kupitia chama anachotokea, na vile vile kupita katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika miaka miwili tu ijayo.

Ikumbukwe kwamba namba 1 huyo babu zake ni wandengereko wa Mkuranga mkoani Pwani, ambapo baba yake mwenyewe alieleza kwamba alipelekwa katika kisiwa hicho na wazazi wake ili akajifunze elimu akhera na baadae kurudi mkuranga kuendelea na mambo mengine.

Ila kwa bahati mbaya au nzuri baba huyo alipofika huko, akaongeza na elimu dunia na mwisho wake kulowea huko hadi kuwa namba 1 wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Sasa namba 1 wa sasa historia anaijua na kamwe hawezi kufanya mzaha wa kumega palipo asili yake, huku akijua kwamba huenda na yeye ikatokea siku 1 akawa namba 1 tena wa JMT kama ilivyotokea kwa baba yake.

Kuna msemo wa waingereza unasema "Home sweet Home" na ndio maana namba 1 huyo miaka yake yote ya siasani hakuwa kugombea huko alipo sasa, bali alikuwa anagombea kule ilipo asili yake (mkuranga)

Sasa kwa vile amezungukwa na wazalendo uchwara wa Zanzibar ambao wengi wao wanaonesha chuki ya dhahiri kwake kama mzanzibar-mtanganyika na Tanganyika yetu kwa ujumla. Basi ndo akaja na style ya kuwafubaza kwa kile wapendacho kukisikia ili iwe rahisi kuchagulika kwa kuamini kwamba namba 1 huyo yuko pamoja na wao katika kupigania masilahi ya kisiwa chao.

Mnaofikiri kuwa Bagamoyo itamegwa chini ya namba 1 huyu wa sasa basi mtasubiri sana na ukizingatia hata huyu wa Muungano nae asili yake ni huko udigoni Tanga. Maana angekuwa original wa kule kisiwani, kamwe asingepewa nchi kama ilivyokuwa kwa kina dr SAS alienyang'anywa tonge mdomoni na mzee rukhsa kwa sababu ya kile nilichoeleza hapo juu.

Karibuni kwa kuchangia kistaarab.

Tanganyika nitakupenda mpaka kufa.
Shakespeare called this MUCH ADO ABOUT NOTHING. Hakuna kitu, hapa ni porojo tu nenda zako jitafutie riziki yako.

TAZAMA RAMANI UTAONA NCHI NZURI, YENYE MITO NA MABONDE MENGI YA NAFAKA. UTUMWA WA NCHI KARUME AMEUKOMESHA.
 
Back
Top Bottom