Swali ambalo Hayati Mwalimu Nyerere aliulizwa na wazungu akajibu kisanii matokeo yake tunayaona sasa

Ulitaka ajibu vipi? Kwamba bado hatujakua tayari kujitawala? Wee ndio wale wamelewa kasumba ya wazungu. Kwani wenyewe unaamini walikua wanatutawala ili tupate uwezo wa kujitawala? Hakika watu ka wewe wanatia huruma kwa ujinga.
Hawa ndiyo aina ya watu tunao wasikia huku mitaani wakisema Bora wabishi Kama mbwa au paka Marekani au Ulaya kuliko kuishi Tanzania akiwa binadamu.
Wapo wengi wavivu wa kufikiri na kujitafutia wenyewe. Utawasikia wakisema Tanganyika tuliomba Uhuru mapema siyo kama Kenya.

Wanasahau kuna kisiwa hapa Africa kinaitwa Mayotte bado kinatawaliwa na France hadi leo 2024 na bado masikini sana hakifanani na France yenyewe.
 
Msumbiji na Angola zilicheleweshwa Uhuru hadi 1975 bado masikini.
Zimbabwe ilicheleweshwa hadi 1980 bado masikini sana.
Marekani ilipata Uhuru miaka 300 kabla ya hizo lakini inaongoza kiuchumi.
Utaona hapo tofauti Africa walikuja kuchukua utajiri na America walienda na kuhamua kupajenga na kuoafanya pawe nyumbani kwao.
 
Nyerere aliitawala nchi kwa miaka 26,
Katiba mbovu ambayo Nyerere alikuwa anailalamikia yeye ndiye alikuwa muasisi wake na alikuwa na uwezo wa kubadilisha, kwa nini hakufanya hivyo??
 
Wakati sisi tunapata uhuru Msumbiji, Angola na Zimbabwe walianzisha vita na wakoloni wao kwa hiyo kwa miaka takribani 15 hizo nchi zilikuwa vitani.
 
Nyerere was right
 
Nyerere aliitawala nchi kwa miaka 26,
Katiba mbovu ambayo Nyerere alikuwa anailalamikia yeye ndiye alikuwa muasisi wake na alikuwa na uwezo wa kubadilisha, kwa nini hakufanya hivyo??
Hakufanya na haikua lazima yeye tu ndio afanye, watu wengine walikatazwa kufanya baada ya yeye kuondoka?
 
Wakati sisi tunapata uhuru Msumbiji, Angola na Zimbabwe walianzisha vita na wakoloni wao kwa hiyo kwa miaka takribani 15 hizo nchi zilikuwa vitani.
Sisi tulikuwa vitani na Uganda, plus tulisaidia ukombozi wa nchi ulizotaja na zingine.
It's pretty much like what EU/NATO are doing now in Ukraine-Russia conflict. Hivyo siyo jambo baya kusaidia jirani for security and economic reasons.
I have mentioned Ukraine issue just to preempt wale wanaolaumu kwamba uhamuzi mbaya Nyerere kupeleka majeshi Uganda na pia kwenye ukombozi wa nchi za SADC.
 
Wasomi walikuwa wengi tu, lakini ujasiri ulikuwa mdogo, plus invisible power alizosomewa huko bagamoyo, ndizo zilizofanya watu sahihi warudi nyuma na yeye kusonga mbele, mazonge ni mengi mno toka zamani, wabubu waliamini nguvu za kiza, mpaka kutuwekea vitu ambavyo baadhi vinaendelezwa na kuheshimiwa mpaka leo hii.
 
Tatizo ni kuwa uelewa wako ni mfupi. Kusema kuwa matatizo ya Tanzania leo yanatokana na jibu la Nyerere ni ujinga wa hali ya juu sana, kwani Nyerere aliondoka Madarakani mwaka 1985 ikiwa ni miaka tisa kabla Rwanda hawajachinjana mwaka 1994, lakini Rwanda hawana matatizo yaliyopo Tanzania leo hii.

Pambana kama vijana wa Kenya, hawasemi Jomo Kenyata alituletea matatizo haya, bali wanapambana nayo head on; fanya hivyo na wewe .
 
Mwl.alikuwa na akili zote timamu,alihitaji kujenga siasa kwanza kabla ya uchumi wa watu Kwa sababu watu Wakiwa na Uchumi na nyakati zile Nchi isingetawalika ndio maana hata yeye aliponea mapinduzi zaidi ya mara 5.
 
Mbona dingi alitoa jibu la kitaalum kabisa.

Ni upungufu wa akili mtu kumlaumu Nyerere miaka 40 toka astaafu na miaka 25 toka afariki Dunia.

Kwamba hatima ya maendeleo na maono ya nchi hii yalikua kwa Nyerere tu, sio?
Waambie hao ......wameshindwa kujiendeleza lawama wanamtupia marehemu asiyeweza kujitetea
 
Mwl.alikuwa na akili zote timamu,alihitaji kujenga siasa kwanza kabla ya uchumi wa watu Kwa sababu watu Wakiwa na Uchumi na nyakati zile Nchi isingetawalika ndio maana hata yeye aliponea mapinduzi zaidi ya mara 5.
Alipinduliwa coz ya kuwafanya wa tz wawe masikini.
Wa tz walikuwa wanataka maendeleo ya Kweli na ya kisasa.

Leo mpaka viongozi wakuu Wana lalamika Kazi hazifanyiki , kila kitu kwenye nji hii ni siasa.

Na nani alisema Nchi ikiwa na matajiri haitawaliki, Sio Kweli hata kidogo, Shughuli za kiuchumi zinahitaji Amani na utulivu ili kuleta maendeleo.

Tanganyika ilipata Uhuru Kwa England, Nchi ilikuwa na amani na Shughuli za uchumi zilikuwa zimekuwa vizuri Tu
England ili ipea Tanganyika Uhuru wake, lakini mpaka Nyerere anangatuka uchumi wa Nchi total ulikuwa collapsed.
Ndio maana alikufa Kwa Ngoma
 
Lile jibu lilikuwa la falsafa kubwa sana, akili ndogo hawawezi kulielewa.
Hiyo falsafa kubwa sana ni ipi hapo?

Nilichokiona mimi ni kwamba Nyerere alitumia tu common sense ya kawaida ambayo mtu mwingine yeyote mwenye akili za kawaida, naye angesema vivyo hivyo, pengine labda kwa kutumia maelezo na mfano tofauti lakini maudhui yakawa ni yaleyale.

Mporaji yeyote wa mali ya mtu hana haki ya kumpangia chochote huyo aliyempora hiyo mali yake.

Hicho ndicho Nyerere alichokisema, kimsingi.

Utamporaje mtu koti lake halafu uanze kumpangia mambo kuhusu hilo koti?

Wewe mporaji hukuwa na huna haki ya kumpora mtu mali yake.

To me that’s just basic common sense. I don’t see it as being a big time philosophical idea.

Just a basic moral compass issue.

However, the example he [Nyerere] gave was very easy for anybody to understand.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…