Swali chokonozi: Hayati Magufuli aliwapigania wanyonge gani?

Swali chokonozi: Hayati Magufuli aliwapigania wanyonge gani?

Jiwe hata mumpambe vipi mwenyezi Mungu mwenyezi kaamua alivyoamua kwa sababu ya kuokoa watu huyu angemaliza watu , unadhulumu watu pesa zao , unafungulia watu kesi bandia za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ili uchukue hela zao , unapora bureau de change , unatumbua hovyo , hutaki kuongeza mishahara , kupandisha madaraja utafikiri hela zake za mfukoni mwake , unapoteza watu , funga , filisi aende mbinguni thubutu labda mungu wa afande Sele .
 
Wauzaji wa barabarani. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Amewaacha taabani kuliko alivyowakuta , wanyonge mliomo humu hebu twambieni mmepiga hatua gani? Ulikuwa na baiskeli moja , gari moja , duka moja , laki moja , pikipiki moja Leo amekuacha na ngapi ? Mishahara ameikuta kiasi gani na ameacha kiasi gani ? .Zile bilioni 96 na 180 zilizoibwa zimefanya kazi Sana ya manipulate msiba huu well done ila Mungu hadhihakiwi .
 
Ndugu zangu poleni na msiba.

Tukiwa tunaendlea na maombolezo ya JPM, naomba kuwajua wanyonge ambao huyu mtu aliwapigania na kuwatetea.

Hii itasaidia kuweka kumbukumbu sawa. Kabla hatujamwita na kumfananisha na masiya. Je wanyonge aliowapigania ni kina nani?

Aliwakuta wakiwa na hali gani kinaisha 2015? Amewaachaje hapo 2021 alipofariki?

Mnyonge wa Tanzania ni nani, anafanyah mini yupo wapi? Maswali haya yatasaidia.

Ni katika kipindi chake watumishi hewa walifujuzwa kazi bila kulipwa chochote hawa wanategemewa na wanyonge huko kwao.

Alipora KOROSHO za wanyonge huko Kusini. Hawa ni wanyonge.

Aliongoza makato kwenye mikopo ya elimu ya juu. Hii ilisumbua wanyonge hasa watumishi wa umma.

Vitambulisho vya Wamachinga yalikuwepo sasa vipi na biashara zinafanyika kiholela holela.

Ewe mnyonge wa Tanzania nikukute wapi?
Swali zuri mkuu , huwa nashangaa mtu kukubali kwamba yu mnyonge, binafsi Sina pesa Kama wale ila haitatokea kua mnyonge,hata siku moja, unyonge sio sifa mzuri,so ukikubali hu mnyonge jua una matatizo
 
Jiwe hata mumpambe vipi mwenyezi Mungu mwenyezi kaamua alivyoamua kwa sababu ya kuokoa watu huyu angemaliza watu , unadhulumu watu pesa zao , unafungulia watu kesi bandia za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ili uchukue hela zao , unapora bureau de change , unatumbua hovyo , hutaki kuongeza mishahara , kupandisha madaraja utafikiri hela zake za mfukoni mwake , unapoteza watu , funga , filisi aende mbinguni thubutu labda mungu wa afande Sele .
Hii comment ingefunguliwa uzi wake ikajitegemea..jaman niliwaonea huruma matajiri wenye bureau de change balaa..dah hapana jaman twende mbele turudi nyuma kifaa kiliumiza wengi
 
Hoja ya kwanza nataka kukuhoji ni hilo swala la watumishi hewa.

Hivi wewe una akili sawa sawa kwanza.....?!

Yaani mtu amefanya kosa kisheria halafu unakuja kuandika kama hoja ya kutaka huyu mtu aonekane kaonewa, kweli upo serious we mkosa hekima?!

Hivi ni wapi umeshawahi kusikia mtu anaefoji na kughushi vyeti vya taaluma, akigundulika basi atasimamishwa kazi na kupewa zawadi ya kulipwa malipo kwa utendaji wake?!

No wonder hii inchi yetu ina sheria za kipumbavu sana muda mwingine kwenye taasisi nyeti kama uhamiaji, TRA na mashirika ya bima.

So ulitaka tuendelee kusapoti watu wanaodanganya kwa kutumia vyeti feki tu kwasababu wanafamilia zinawategemea?!

Upuuzi wa karne huu......... Yaani mtu anaandika kabisa kutetea uovu as if hakuna kosa hapo.....
Kama alitaka kupambana na waliofoji vyeti angeenda na jeshini huko, polisi, pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama

Mbona huko hakugusa kuondoa walio foji vyeti?

Yalikuwa maigizo tu

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Maisha yamejawa na mambo mengi Sana ambayo mengine yanahitaji utulivu kuweza kuyapambanua. Kuna msemo wa kizungu unasema " empty words hamper the nation, hard work save it" sisi vijana tunaongea Sana polojo kuliko hata uwezo wetu wa kufanya kazi. Raisi sio malaika hawezi kufanya miujiza ambayo haiwezekani. Taifa linahitaji devotion yaani kujitoa kwa watu wake katika ubunifu, waminifu, uhodari, ujasiri, weledi na uchapakazi. Leo watu wachache wanamlaumu Raisi huku wengine wakitengeneza na maisha yanasonga vizuri. Vijana tuach polojo na degree zetu za copy and paste. Leo unasema Raisi alidhulumu kolosho, weka evidence na sio kupotosha watu. Zingene huwa ni propaganda za maadui ambao maslahi yao yamekinzana na maslahi ya umma. Kuwa Raisi wa wanyonge sio kuwagawi hela ni kuwapa watu confidence hasa grass root. Raisi wetu hakuwa malaika anakosea Kama wengine. Jiulize tukikupa wewe utafanya Nini? au tumpe baba yako mnywa gongo Kama atatoboa
Hao wapambe wake, walikuwa wanakubali hata hayo mapungufu?tuanzie hapo, shida ni kuwa alionekana kama sio binadamu wa kawaida, ambaye hana pungufu hata moja!!sasa utawapa hao wanyonge confidence bila kuwa na shughuri za kiuchumi za kufanya??kama mfumo wa elimu ndio huu, unaona eti somo la history ya nchi ni muhimu sana leo, ubunifu huo utatoka wapi?!!kuna mema aliyafanya na kuna mabaya pia!!hasa kwenye demokrasia na haki za binadamu huku hapanaaa!!!kwenye korosho, nani asiyejua kilichowakuta watu huko??kuna hatua gani serikali imechukua juu ya kuwasaidia hao wakulima kuwakwepa hao kina KANGOMBA??na kwenye kahawa huko?kama sio udhurumaji tu?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kuitwa Mnyonge sio neno nzuri, ni kama kashifa tu

Ila naona watu wanashabikia na kufurahi kuitwa wanyonge
Hahaaa!!wanyonge ni wengi na ndio wapiga kura, ila matajiri ni wachache na ndio wanaoendesha uchumi wa nchi.sasa jamaa aliwatia moyo na kuuona unyonge ni baraka, na utajiri ni laana ili, kila wanachosaidiwa wakione kama ni hisani kumbe ni pesa zao!!na kuwafanya wamuone tajiri kama ndio adui yao!!!
 
Maisha yamejawa na mambo mengi Sana ambayo mengine yanahitaji utulivu kuweza kuyapambanua. Kuna msemo wa kizungu unasema " empty words hamper the nation, hard work save it" sisi vijana tunaongea Sana polojo kuliko hata uwezo wetu wa kufanya kazi. Raisi sio malaika hawezi kufanya miujiza ambayo haiwezekani. Taifa linahitaji devotion yaani kujitoa kwa watu wake katika ubunifu, waminifu, uhodari, ujasiri, weledi na uchapakazi. Leo watu wachache wanamlaumu Raisi huku wengine wakitengeneza na maisha yanasonga vizuri. Vijana tuach polojo na degree zetu za copy and paste. Leo unasema Raisi alidhulumu kolosho, weka evidence na sio kupotosha watu. Zingene huwa ni propaganda za maadui ambao maslahi yao yamekinzana na maslahi ya umma. Kuwa Raisi wa wanyonge sio kuwagawi hela ni kuwapa watu confidence hasa grass root. Raisi wetu hakuwa malaika anakosea Kama wengine. Jiulize tukikupa wewe utafanya Nini? au tumpe baba yako mnywa gongo Kama atatoboa
Ok sante kwa ku-comment
 
Kama hata hujui kwamba korosho ziliporwa huko mkoa ya kusini 2017 basi wewe kweli una degree ya ku copy na kupest. Nilikuwepo mikoa hugo najua kilichotokea

Chakula kilijeuka mbegu zikajiotea hovyo ghalani. Aibu sana
 
Wale watumishi walikuwametoa jasho lao kuitumikia serikali. So they deserved their right!

Kwanini uadhibu walioajiriwa tu....mbona waliowaajiri hawakuadhibiwa? Think again!

Kwanini bashite hakuadhibiwa?

Zoezi lile lilikuwa la uonevu mkubwa kwa wanyonge halisi wa nchi hii.

Waliowaajiri walidanganywa na vyeti walivyopewa!

Huwezi kudai mafao uliyoyapata kwa udanganyifu!

Makonda alias Bashite alitemwa ama hukuona!?
 
Z
Hakuna kitu kama hicho. Hiyo mikataba mingi haikusainiwa na awamu ya magufuri. Mikataba imesainiwa kipindi cha awamu ya kikwete na mkapa.

Na hata wahusika wazee akina mkapa na kikwete wanakiri kuwa ile mikataba ilikuwa ni ya kimangungo na nyakati zile hawakuona madhara yake ila wanaona sasa....

Sasa ulitaka asitie hata jitihada kuivunja....?!

Tatizo watoto wa sasa hivi research hamfanyi mnategemea kupewa taarifa Twitter na kwenye mitandao mingine ya kijamii. Lema au tundulissu aandike jambo ninyi mumnukuu na kuandika upuuzi wake kama ndio maoni yenu.

Tumieni akili....
Msukule mwingine huu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
wanyonge wa kimara hadi kibamba ambao hawakumpigia kura wakaisoma namba ila wa mwanza waliitwa wapiga kura wake akakataza wasibomolewe
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Umemaliza Mkuu 🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾

Back
Top Bottom