D
DeletedMember281674
Guest
Serikali imebainisha kwamba ifikapo januari 2022, elimu itakuwa ya kulipia..???!? Elimu ipi? Ya Serikali ipi???Ndugu zangu poleni na msiba.
Tukiwa tunaendlea na maombolezo ya JPM, naomba kuwajua wanyonge ambao huyu mtu aliwapigania na kuwatetea.
Hii itasaidia kuweka kumbukumbu sawa. Kabla hatujamwita na kumfananisha na masiya. Je wanyonge aliowapigania ni kina nani?
Aliwakuta wakiwa na hali gani kinaisha 2015? Amewaachaje hapo 2021 alipofariki?
Mnyonge wa Tanzania ni nani, anafanyah mini yupo wapi? Maswali haya yatasaidia.
Ni katika kipindi chake watumishi hewa walifujuzwa kazi bila kulipwa chochote hawa wanategemewa na wanyonge huko kwao.
Alipora KOROSHO za wanyonge huko Kusini. Hawa ni wanyonge.
Aliongoza makato kwenye mikopo ya elimu ya juu. Hii ilisumbua wanyonge hasa watumishi wa umma.
Vitambulisho vya Wamachinga yalikuwepo sasa vipi na biashara zinafanyika kiholela holela.
Ewe mnyonge wa Tanzania nikukute wapi?