Swali chokonozi: Hayati Magufuli aliwapigania wanyonge gani?

Jiwe hata mumpambe vipi mwenyezi Mungu mwenyezi kaamua alivyoamua kwa sababu ya kuokoa watu huyu angemaliza watu , unadhulumu watu pesa zao , unafungulia watu kesi bandia za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ili uchukue hela zao , unapora bureau de change , unatumbua hovyo , hutaki kuongeza mishahara , kupandisha madaraja utafikiri hela zake za mfukoni mwake , unapoteza watu , funga , filisi aende mbinguni thubutu labda mungu wa afande Sele .
 
Wauzaji wa barabarani. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Amewaacha taabani kuliko alivyowakuta , wanyonge mliomo humu hebu twambieni mmepiga hatua gani? Ulikuwa na baiskeli moja , gari moja , duka moja , laki moja , pikipiki moja Leo amekuacha na ngapi ? Mishahara ameikuta kiasi gani na ameacha kiasi gani ? .Zile bilioni 96 na 180 zilizoibwa zimefanya kazi Sana ya manipulate msiba huu well done ila Mungu hadhihakiwi .
 
Swali zuri mkuu , huwa nashangaa mtu kukubali kwamba yu mnyonge, binafsi Sina pesa Kama wale ila haitatokea kua mnyonge,hata siku moja, unyonge sio sifa mzuri,so ukikubali hu mnyonge jua una matatizo
 
1.Makonda
2.Sabaya
3.Doto James
4.Heri James
5. Mama D
6. johnthebaptist
7...............
8.........
 
Hii comment ingefunguliwa uzi wake ikajitegemea..jaman niliwaonea huruma matajiri wenye bureau de change balaa..dah hapana jaman twende mbele turudi nyuma kifaa kiliumiza wengi
 
Kama alitaka kupambana na waliofoji vyeti angeenda na jeshini huko, polisi, pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama

Mbona huko hakugusa kuondoa walio foji vyeti?

Yalikuwa maigizo tu

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Hao wapambe wake, walikuwa wanakubali hata hayo mapungufu?tuanzie hapo, shida ni kuwa alionekana kama sio binadamu wa kawaida, ambaye hana pungufu hata moja!!sasa utawapa hao wanyonge confidence bila kuwa na shughuri za kiuchumi za kufanya??kama mfumo wa elimu ndio huu, unaona eti somo la history ya nchi ni muhimu sana leo, ubunifu huo utatoka wapi?!!kuna mema aliyafanya na kuna mabaya pia!!hasa kwenye demokrasia na haki za binadamu huku hapanaaa!!!kwenye korosho, nani asiyejua kilichowakuta watu huko??kuna hatua gani serikali imechukua juu ya kuwasaidia hao wakulima kuwakwepa hao kina KANGOMBA??na kwenye kahawa huko?kama sio udhurumaji tu?
 
Reactions: BAK
Kuitwa Mnyonge sio neno nzuri, ni kama kashifa tu

Ila naona watu wanashabikia na kufurahi kuitwa wanyonge
Hahaaa!!wanyonge ni wengi na ndio wapiga kura, ila matajiri ni wachache na ndio wanaoendesha uchumi wa nchi.sasa jamaa aliwatia moyo na kuuona unyonge ni baraka, na utajiri ni laana ili, kila wanachosaidiwa wakione kama ni hisani kumbe ni pesa zao!!na kuwafanya wamuone tajiri kama ndio adui yao!!!
 
Ok sante kwa ku-comment
 
Kama hata hujui kwamba korosho ziliporwa huko mkoa ya kusini 2017 basi wewe kweli una degree ya ku copy na kupest. Nilikuwepo mikoa hugo najua kilichotokea

Chakula kilijeuka mbegu zikajiotea hovyo ghalani. Aibu sana
 

Waliowaajiri walidanganywa na vyeti walivyopewa!

Huwezi kudai mafao uliyoyapata kwa udanganyifu!

Makonda alias Bashite alitemwa ama hukuona!?
 
Z
Msukule mwingine huu
 
Reactions: BAK
wanyonge wa kimara hadi kibamba ambao hawakumpigia kura wakaisoma namba ila wa mwanza waliitwa wapiga kura wake akakataza wasibomolewe
 
Reactions: BAK
Umemaliza Mkuu πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…