Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Shirikisho la soka hapa nchini almaarufu kama TFF linaratibu, kuongoza na kusimamia soka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. CAF ni kwa Afrika nzima na FIFA ni kwa dunia. TFF inatekeleza majukumu yake, pamoja na mambo mengine, kupitia Kamati na uongozi wake.
Jana, Kamati ya Maadili imemfungia Msemaji wa Yanga Haji Sunday Manara kujihusisha na soka 'ndani na nje ya nchi' kwa kipindi cha miaka miwili pamoja na kuamriwa kulipa adhabu ya milioni 20. Manara, akiungwa mkono na klabu yake ya Yanga, ameonyesha nia ya kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo. Tunasubiri kuona kitakachotokea.
Lakini, nimechukua muda wangu (pamoja na kwamba sijafanikiwa kupata, kusoma na kuelewa Kanuni zilizoiongoza Kamati jana) kutafakari juu ya kufungiwa kwa Manara 'ndani na nje' ya Tanzania. Najiuliza, TFF inaweza kumfungia mtanzania-kama Manara kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi?
Yaani, uamuzi wa TFF juu ya jambo lolote unaweza kuvuka mipaka ya Tanzania na hata kuingia mipaka ya CAF na FIFA? Mfano, Manara hawezi kwenda na kuwa Msemaji wa URA ya Uganda? Kama mamlaka ya TFF yanavuka mipaka ya Tanzania, uamuzi wa jana utabaki salama.
Kama mamlaka ya TFF, kupitia Kamati zake, hayavuki mipaka ya Tanzania, adhabu hiyo haipaswi kubaki salama kwasababu ina makosa surani pake na kumbukumbu zake (on the face of it and its records).