SWALI FIKIRISHI: Kwanini CCM wanawalaumu Wapinzani huku wao ndo watawala kwa miaka 59

Umesema ukweli tupu!!
 
Lete ushahidi wa kilichoharibiwa na wapinzani sehemu yoyote ile alafu serikali inaangalia tu ilihali kuna polisi na mahakama.
In short, upinzani wa Tanzania upo kuzuia na kupinga Maendeleo yanayofanywa na serikali iliyopo madarakani, Na sio kuikosoa na kuielekeza serikali njia sahihi(ambalo kazi kubwa ya upinzani)
(1) Kwa mfano, Ujenzi wa uwanja wa ndege chato ulitaka wapinzani wasipinge?
(2) Vipi kuhusu manunuzi ya ndege? Tija ipo?
(3) Ujenzi wa Stiga gorge, je mpango wa ujenzi ulikuwa ni kwa kipindi hiki?
(4) Vipi kuhusu Ujenzi wa jengo kubwa la TRA chato ulikuwa sahihi?
(5) Hospital ya rufaa chato, ni sahihi? (Geita mjini hakuna hospital ya rufaa).
 
Wanazuiaje maendeleo? Wanahujumu? Mbona wahujumu uchumi wanaoshtakiwa kila siku ni watu wa CCM?
Propaganda za kitoto kabisa hizo kupata kutokea katika nchi hii.
Na ujumbe huu wa kijinga umekuwa ukitumiwa awamu hii ya 5 na ndio umewaangusha sana mbele ya wananchi
 
Acha akili na mawazo mgando kama za Gwaji Boy. Hayo maendeleo si yangeonekana kwenye majimbo yaliyo chini ya ccm toka tupate Uhuru?
 
Suala la debate liwe la kisheria ni lazima sio hiyari, ukiwa unataka kuwa kiongozi mkuu wa nchi ni lazima ukubali kuulizwa. Ni vizuri kuongelea uliyofanya ila haikufanyi usiulizwe maana ukija katika uchaguzi mpya utaulizwa unataka kufanya nini sio ulifanya nini, uliyoyafanya umeshapigiwa kura ndio maana unaomba tena tukijikita kila mara ohhh unajuwa tulikuwa na shule 2 leo 10 sijui Ma Dr 10 leo 20 hiyo haisaidii lolote na wala nchi haitaendelea. Hapa naomba miaka 5 sababu tunataka kufanya A, B, C ... na kama hukuyafanya uliyoahidi nyuma utaulizwa.
 
Kaka tuache ujinga. Ndio maana tukiwa CCM tunadharaulika. Upinzani umeanza rasmi Tanzania mwaka 1992. Maendeleo gani tuliyapata kabla ya hapo wakati hakukuwapo wa kupinga kila kitu?
 
Kabla ya upinzani kuwepo Tanzania ilikuwa inaenda vizuri kiuchumi
Kaka tuache ujinga. Ndio maana tukiwa CCM tunadharaulika. Upinzani umeanza rasmi Tanzania mwaka 1992. Maendeleo gani tuliyapata kabla ya hapo wakati hakukuwapo wa kupinga kila kitu?
 
Mkuuu hujamjibu mleta mada,soma tena uzi wake alafu umjibu.
 

Unaijua siasa? Kazi ya chama tawala ni ipi na ya upinzani ni ipi??

Unataka upinzani waseme "CCM na Magufuli ni wazuri na wanafanya kazi vizuri lakini tunaomba kura tu!"

Tuiache siasa iwe siasa, upinzani kuwa against serikali ndiyo kazi halali ya upinzani!!

Haiwezekani serikali wakajenga flying over upinzani wakaenda kubomoa kwamba ndiyo kupiga maendeleo ila upinzani watakwambia ile flying over serikali imepoteza pesa tu kwani haijasolve tatizo na ndiyo maana mvua kidogo mji unasimama!! Upo?
 
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana! ungejaribu hata kumuelewa mleta mada usingeandika hizi pumba ulizoandika hapa, Mgombea wa ccm anaposema nchi yetu ilikuwa imefika pabaya, je ni viongozi wa chama gani walikuwa madarakani? ufisadi, uuzwaji wa wanyama wetu kiholela, mikataba ya hovyo, nk ni upinzani gani uliyafanya hayo? ni lini na wapi upinzani walizuia maendeleo yasipelekwe kwa wananchi?
 
Mapungufu ya CCM ndio yamejenga upinzani leo,na yataendelea kupaisha upinzani kesho
 
Ni vigumu kufanya debate na mtu ambaye atatukana. Sawa tu Rais alivyokataa. Kisiasa imekaa vizuri.
Matusi ni kwaajili ya kutukana na ni mazuri yakitumika mahala pake. Kwahiyo kama mtu wako anaeleza ujinga kwenye debate kwanini asitukanwe?

Angalia sasa amekuwepo madarakani, hajaajiri. Sasa hivi anasema chagueni ccm ili atoe ajira. Huo si ujinga? Hapo akitukanwa si ni sawa?
 
Kazi ya upinzani sio kuelekeza serikali. Ni kuanika mapungufu ya kiutendaji ya serikali. Na ndicho wanachofanya. Unapotosha kwa mkusudi kuwa wanapinga Maendeleo.Hawajapinga ujenzi wa miundombinu. wanapinga taratibu kutofuatwa katika manunuzi eg. kutumia pesa bila idhini ya bunge, kukosa kuwa na vipaumbele sahihi eg. kujenga international airport chato huku maji shida, dawa shida, mikopo elimu ya juu shida, mishahara duni + hakuna nyongeza miaka 5 sasa etc..; kumnyima ajira CAG anayehoji upotevu wa 1.5T ; kukandamiza uhuru wa habari na kujieleza, kuweka 'mfuko' kwa rais mahakama na bunge, kuwepo mauaji, utekeji, kesi za kubambika etc; biashara ya ununuzi wabunge namadiwani waupinzani etc. Mambo haya yanafanyika chini ya ccm. Tunashukuru sana wapinzani wanavyo tuwekea wazi maovu haya. Mimi na Watanzania wote wasio wanafiki na wazalendo wa kweli kura zetu ni kwa LIS.U na wabunge na madiwani wa upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…