SWALI FIKIRISHI: Kwanini CCM wanawalaumu Wapinzani huku wao ndo watawala kwa miaka 59

Mbona hujasema wapinzani wamekwamisha jambo gani lililofanywa na fisiemu?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kwamba vijana waliajiliwa kisha wapinzani wakawachomoa huko ajirani ili waishutumu serekali vizuri si ndiyo???
 
Maendeleo ya nchi bila kulitaja bunge ambapo wanadiscuss budget, na kudiscuss baraza la mawaziri kuhusu utekelezaji wake wa hiyo budget unakuwa unazungumza nini sasa.

Natamani kuandika sana,lakini nafsi yangu inasema inatosha.
Kuna yule alinunua ndege na kujenga uwanja wa chato, je bunge lilihusika mkuu?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ni vigumu kufanya debate na mtu ambaye atatukana. Sawa tu Rais alivyokataa. Kisiasa imekaa vizuri.
Mkuu akitukana si ndio vizuri maana tunakuwa tusha jua pumba ipi mchele upi!
 


Kuwa mkweli tu. Km kusinzia Bungeni, wahusika ni wabunge wa vyama vyote. Km ni bajeti za maendeleo, tumeshuhudia kipindi cha miaka mitano iliyopita majimbo ya upinzani yakinyimwa miradi ya maendeleo kwa makusudi kabisa . Isitoshe mgombea urais anasema wazi kabisa kuwa uchaguzi uliopita mlichagua upinzani , kilichowapata mnakijua, chagueni tena muone.

Tuache itikadi za kisiasa tujadili ukweli ili kuwasaidia hata hao watawala wetu kuyaona mapungufu makubwa ya kiutawala ambayo yanasababisha chuki miongoni mwa jamii hususan dhambi mbaya kabisa ya ubaguzi.
 
Umekuja serious mwenyewe, Umeandika Kwa kuhamaki nikajua unapoint za maana. Wai! PUMBA TUPU

Unataka kutuambia wabunge wa CCM ndio hutoaga hoja za kuwatetea wananchi kuliko wabunge wa Upinzani?

Unataka kutuambia wabunge wa CCM ndio wanashindaga majimboni kwao muda wote na wa upinzan ndo wanazurura Dar?

Unataka kutuambia wabunge wa CCM ndio wanakuwaga makini na Macho muda wote pale Bungeni wakati wa Upinzani wanakiwa wanasinzia? Wasira aliku ni wa chama gani? Komba alikuwa ni wa Chama gani?

Kweli nyie mmepanic, mmeanza kichanganya mafile.
 
Ni vigumu kufanya debate na mtu ambaye atatukana. Sawa tu Rais alivyokataa. Kisiasa imekaa vizuri.
Joe yuko jino kwa jino na Donald kila uchao, na wanatoleana lugha kali. Kwa hiyo Magu ni mwoga wa kuambiwa ukweli?
 

Mvua ya siku moja? Hahaha
Hata kungekuwa na lami Mpaka bafuni kama kwa mvua ya siku moja watu wanakaa road masaa 10 Kuna maana gani?

Umetoka kazini saa 11 na umefika kwako saa tisa usiku then unasema Habari za flyover
 
Hivi kwa zama hizi huwezi mjua tapeli ? 'Hawa viongozi wa kitaifa mara nyingi niliwaonya kuhusu kutunza kauli zao, waliniona mimi kapunjunju sasa hivi wanaomba kura tena kwakupiga magoti ni wanafiki tu hao 'there are failed politiciancs'
 
Haahahaa
 

inamaana huoni jinsi chama tawala hasa kiongozi mkuu nao wanavyowatia doa viongozi waliopita kwa kujifanya wao sasa hivi ndio wanafanya kazi na wenzao waliopita hakuna walichofanya!?, hivi kiongozi kusema nchi hii ilikua ya ovyo kuna tofauti gani na wapinzani wnaposema nchi hii iko ovyo?, embu jibu hoja yenye mashiko sio porojo, hii serikal na chama chake ndio kimetufikisha hapa kwa miaka yote hii yani ni ovyo kabisa, shame on them
 
Sidhani kama kuna 'ushirikiano' kati ya akili yako na vidole vyako wakati wa kuandika! Hii yote inaonyesha ulivyo mvivu wa kufikiri!
Kaa chini uwe uwaze kabla ya kuandika, ukishindwa kaa kimya kuficha upumbavu wako.
 
Maendeleo ya nchi bila kulitaja bunge ambapo wanadiscuss budget, na kudiscuss baraza la mawaziri kuhusu utekelezaji wake wa hiyo budget unakuwa unazungumza nini sasa.

Natamani kuandika sana,lakini nafsi yangu inasema inatosha.
hahahahaaa kwani hilo bunge linaongozwa na wa chama gani? inamaana hujui au huonagi pindi wapinzani wanapotakaga kuibana serikali ktk utekelezaji wa bajeti yake jinsi wanavyotendewa mabaya? je huoni jinsi bunge linavyoendeshwa kwa misingi ya uchama na kupokea maamlisho toka juu?
 

Hivi barabara ikishajengwa wapinzani wazuia nini au zahanati ikijengwa au wananchi wakipelekewa maji. Hivi kwa akili yako unaona sawa kutumia mabilioni ya pesa kujenga uwanja wa kimataifa chato ambao anatumia Rais peke yake kuliko kutumia pesa hizo katika huduma za jamii kama afya na elimu. Unajenga daraja pale oysterbay unaacha jangwani wananchi wanahangaika kwa kupita wakati wa mafuriko
 

Kwani ni nani aliyeondoa bunge live na nia yake ilikuwa nini ukijibu hilo swali ndo utajuwa kama wapinzani wanakuwa na hoja bungeni au la
 
Ni vigumu kufanya debate na mtu ambaye atatukana. Sawa tu Rais alivyokataa. Kisiasa imekaa vizuri.
Kukosoa si kutukana. Toa mfano wa tusi moja tu alilotukana mpinzani toka mfumo wa vyama vingi uanze. Usipotoshe ukweli.
 
haijalishi ni nani atashinda ktk uchaguzi mkuu huu hila CCM na serikali si kwamba hawakufanya kitu hila wamefanya machache/kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na muda wa zaidi y miaka 49 waliokaa madarakani na naamini watafanya tena madogo sana kwa kipindi km icho kikacho km watabaki kua madalakani labda km mifumo ya siasa na katiba itabadilishwa na kuwekwa yenye tija zaidi kwa kizazi cha kileo maana ninachoamoni kinachoifanya nchi izidi kudumaa ni mfumo wa siasa na katiba ya nchi hii maana imekua ni nchi ya chama kimoja kilichojificha ktk vyama vingi na katiba hisiyowabana vya kutosha viongozi wakuu na mihimili ya serikal. jamani ndugu zangu hii nchi ni ya kwetu sote tumelisishwa nasi tuwalisishe watakaokuja baada yetu hivyo ni sisi wenye mamlaka ya kutaka tuwalisishe nchi ya aina gani. TUSIFANYE MAKOSA OCTOBER 28, TWENDENI TUKAIJENGE NCHI MPYA KWA UCHAGUZI ULIO SAHII. tuseme kwa pamoja SASA BASI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…