Nimeandika nyuzi kadhaa hapa JF katika kipindi hiki Cha mwaka 2025 mwezi march, Ila sikuwahi kuandika chochote before.
Kiukweli kilichonileta huku kwa namna ya mwandishi badala tu ya kua mfwatiliaji wa nyuzi za watu kama nilivokua hapo kabla ni upweke.
Leo nimefikiri kua niandikie kitu Cha kweli kilichonileta hapa, sabab siku zote nikiandika utani au nyuzi za kufikirisha huwa tu nakua najiliwaza, Ila kiukweli sipo sawa.
Nafahamu hapa watu wa mzaha ni wengi kiasi watanibeza na nini. Ila sema moyo unanituma nitamke shida iliopo moyoni ... Wale wa utani sawa nitanieni .. wale wa serious wanishauri.
Na wale hata wa kuniombea kwa Imani zao sawa wataniombea.
Ila nahisi labda nikisema hili wazo la kujiua labda litanipungua.
Tatizo langu ni Nini Hasa ??
Kiufupi on my late 20s yrs katika maisha ya utafutaji nimeingia hasara kubwa kwenye biashara mwaka Jana mwishomi... mpaka Sasa nimepambana Sana Ila bado nina deni kubwa kwa watu tofauti tofauti ambapo deni limezidi hata mtaji nilio nao.
Na huku mtaji ulobaki haukidhi kulipa madeni Wala Nini...
Mambo yanavozidi kunikaba .. Mara Kodi Mara TRA ndo nawaza nachomokea wapi Ila mbele naona kifo tu... Manake Sasa nguvu za kuvimba zimeisha.
Mimi na degree yangu na umri wangu mchanga bado 28 yrs naona tumefeli kabisa.
Natamani hata ningepata laki tatu nikaagiza mzigo DAR nikakimbizana kuagiza walau Radio za pikipiki ambazo hapa Mbeya nilipo ni adim na zinakimbiza Sana
Ili from there nianze kupunguza madeni nilonayo walau Kila siku nirejeshe 10,000 to 15,000 Ila Sasa zimebakia tu kua wishes... Sjawah kukamata hata 20,000... kutokana na stress nakosa hata focus kwenye deal zangu..
Najua siwez fikia hatua mbaya Ila wazee. Nipo vibaya kias kuwa wazo la kujiua limedominate Sana kichwa changu, nilijarb kufikir juu ya namna ya kukwepa kuona familia yangu ikiaibika mbele ya macho yangu juu ya kuteleza kwangu nilikoteleza ktk biashara.
I wish niseme tu kinitoke labda ntapona .... Wale wa utani heb nitanieni.
Wale vichwa heb nishaurini mwenzenu tafadhari. .. Kodi ya frame inaposogea, dead line ya madeni imepita Sana. Ila sema ndo ivi for now Kila nikiamka kichwa tu kinauma.