Mkono ,macho na masikio ya serikali yapo kila sehemu na kila mahali.ndio maana unakuwa unaona mara nyingi Mheshimiwa Rais akitengua uteuzi wa viongozi mbalimbali aliowateua au kuwahamisha au kusimamisha kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina. Haya yanatokea ni kwa kuwa mamlaka ya juu inakuwa imepokea taarifa na kuamua kuchukua hatua.
Kumbuka nafahamu kuwa siyo kila taarifa ikishafika mezani lazima ichukuliwe na kunyonywa tu kama dodoki kwa kufanya utenguzi wa mtu fulani au watu au viongozi au kiongozi fulani anayetuhumiwa kwa jambo fulani.
Ni lazima taarifa ichakatwe,ni lazima uchunguzi ufanyike tena kwa kutumia watu wengine tena ili kuianisha ukweli wa taarifa iliyotangulia na ile itakayokwenda kubainika baada ya uchunguzi kufanyika. Nalazima ifahamike kwanini hiki kimefanyika na mhusika .je ni kwa maslahi ya Taifa au maslahi binafsi.
Mambo kama ya Rushwa napo ni lazima uchunguzi na upelelezi ufanyike kwa kina .ndio maana wakati mwingine wanatoka na kutolewa watu wizarani huko kwenda huko halmashauri kufanya uchunguzi juu ya mtandao fulani unaoweza bainika kutafuna pesa za umma.nafikiri hapa unaweza kumbuka kilichotokea kule kigoma pale Mheshimiwa waziri mkuu alipogundua kuwa kuna mtandao wa ufujaji wa pesa za umma ambao umeanzia juu kabisa huko. Haya yanakuwa yanabainika kwa kuwa kuna macho ya serikali ambayo yanaipa serikali taarifa.hivyo fahari kuwa vyombo vyetu vya usalama vipo kila sehemu na vinafanya kazi usiku na machana kuhakikisha kuwa mambo yote yanakwenda sawa kwa maslahi ya Taifa.
Haya ya kudhulumiana mtu na mtu au kucheleweshwa kulipwa madai na halmashauri ni mambo yatakayoendelea kushughulikiwa kila siku,,kikubwa ni kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa na kufichua Vitendo vya dhuluma na unyanyasaji wanavyokumbana navyo katika ofisi za umma ili hatua zichukuliwe.
Serikali ya Rais Samia Ni Serikali ya haki na iliyodhamilia kutenda haki kwa kila mtu bila kujali hali yake .