Kuendesha Serikali ya Kijamaa ni mzigo kwa wananchi....
Unadumbukiza bilion 32 kujenga soko k.koo utafikiri kuna huduma zimesimaa kwa kuungua soko hilo...
Serikali imekua ikijenga majengo makubwa yasiyo na tijaa...
Kodi za wananchi hazinufaishi wananchi....
Hatujawahi pata Rais mwenye dhamira ya kuondoa umasikini na kuwapa wananchi dira ya kuondokana na umasikini....
Nadhani badala ya serikali kutoa fedha hii moja kwa moja watumie mfumo PPP...
Mamlaka za serikali za mitaa nyingi [wilaya, miji, manispaa na majiji] zinatumia mfumo wa PPP kwa ujenzi wa masoko...
Mfano kwa Jiji la DSM, wafanyabiashara wenyewe wanaweza kujenga soko hilo na serikali kazi yake ikawa ni kuandaa designs, mobilization ya resources, kutoa ardhi na mengine ya namna hiyo...
å CHA KWANZA, kinachotakiwa kufanyika ni kupata orodha ya wafanyabiashara wote wanaotaka kuwa wapangaji kwenye jengo litakalojengwa...
å CHA PILI, waandalie mkataba wa upangaji wa aidha miaka 2, 5, au 10...
å CHA TATU, wakokotolee gharama za upangaji na kila mmoja alipe in advance na fedha hiyo itumike kwenye ujenzi soko...
Mathalani kama mkataba ni wa miaka 10, ina maana kila mfanyabiashara atalipa kodi ya miaka hiyo kulingana na thamani ya nyumba/chumba/kizimba anachotaka kuchukua. Kutakuwa na GRADE YA VYUMBA/NYUMBA/VIZIMBA kulingana na aina ya biashara ya mtu MF. banks au financial institutions, hotel, maduka nk nk...
Kwa miaka yote hiyo, yeye ndiye atakuwa mpangaji mmiliki halali wa eneo na kama ataamua kuacha biashara ama amefilisika, atatoa taarifa kwa mbia mwenzake [i.e serikali/jiji la DSM] ili aweze kumpangisha mtu mwingine hadi contract expired time yake na fedha itakuwa yake...
Baada ya mkataba kwisha, 100% serikali kupitia Jiji inakuwa mmiliki wa majengo/jengo na kila mpangaji ataanza kulipa tens kodi ya pango...
Sasa tuashumu serikali inapokea maombi ya wafanyabiashara 20,000 na kila mmoja akaweza kutoa fedha kiasi cha wastani wa TZS 50,000,000 maana yake zitapatikana jumla ya TZS 1,000,000,000,000 [TILIONI MOJA]..!!
Hii maana yake kwa fedha hii wananchi wenyewe wanaweza kujijengea soko la kisasa la aina yake duniani bila serikali kutumia hata senti moja kutoka kwenye fedha za kutoa huduma zingine kwa umma!
å MWISHO, kupitia biashara zitakazokuwa zinaendelea na kufanyika kwenye soko hili, serikali itajipatia kodi za aina mbalimbali kwa kiwango cha kutosha na kutisha sana...
Na kwa kuwa soko litakuwa la kimataifa na kila mfanyabiashara anapenda KARIAKOO, mimi nauhakika kutakuwa na msururu wa malaki ya wafanyabiashara watataka kuwa wabia wa soko hili...!!
Mawazo yangu haya kwa kukukwoti wewe..