Soko la Kariakoo litajengwa upya; inakadiriwa na kudaiwa kuwa serikali itatenga bilioni 32 kulijenga upya. Hili si jambo baya. Ila naomba kuuliza kwa hizo bilioni 32 Watanzania watarajie nini kwenye soko hilo kubwa na maarufu zaidi nchini...
Hofu yangu isije ikawa umechukulia Soko la Kariakoo kama sehemu ya kushusha na kuuza nyanya, biringanya, viazi mbatata, and the like huku ukisahau, kwavile ni City Center, Kariakoo Market is just a brand, na jengo lake linaweza kuwa hata na maduka makubwa ya kuuza bidhaa za jumla!
Hofu yangu isije ukawa unachukulia Kariakoo Market kama sehemu ambayo wanaoenda hapo ni watu kutoka Mbagala, Manzese, Mwenge, and the like but Kariakoo ni kubwa kuliko hayo mambo!!
We all know wafanyabiashara kutoka nchi jirani huwa wanaenda Kariakoo kununua bidhaa... hawaendi Kariakoo kununua nyanya na vitunguu bali kununua bidhaa za viwandani ambazo maduka yake yanaweza kuwa housed kwenye jengo la Soko la Kariakoo!
Ukijenga multiple basement levels, unaweza ndani yake ukajenga Self Storage Units ambazo KATU haziwezi kukosa Wapangaji!! Hizi Self Storage Units unaweza kuziweka hata kwenye floor zingine, above the first floor! Na amini usiamini, kwa mazingira ya Kariakoo, hizi Self Storage Units zinaweza kuwa na demand kubwa sawa tu na demand ya frames za biashara!!
So, YES... kutakuwa na Value For Money labda wenyewe tu washindwe kufahamu jinsi ya ku-utilize eneo husika!!