Swali Fyatu la Jumamosi: Hili Soko la Bilioni 32 litakuwa na Vitu Gani Ndani?

100%
 
Najiuliza pia hivi hili soko likijengwa pembezoni mwa mji hawa watu ambao tunasema ni overpopulated na wapo katikati ya mji watakuwa saved na soko gani?

Au ndio nao wataanza kutoka mjini saa kumi alfajiri kuelekea pembezoni ili waweze kuwahi kununua mahitaji yao na kurudi?

Hivi hakuna uwezekano wa kujenga barabara za juu kupunguza msongamano katikati ya mji na ikawezekana kufika kariakoo kwa muda mchache?

Je kwa jinsi mji wa Dar ulivyokaa ni sehemu ipi ya pembezoni inaweza fikika kirahisi bila foleni kwa mfumo wa barabara tulizonazo?

Je hizo nchi zingine ambazo miji ni over populated wanajenga masoko nje ya mji (pembezoni) au yapo katikati ya miji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi soko la kariakoo lijengwe tena kubwa tu lakini pia pawe na masoko ya ku serve maeneo mengine kama Tegeta, Gongo la mboto etc.

Soko la k.koo kwa size ya sasa ni dogo sana na linasababisha msongamano mkubwa sana wa wanunuzi. Kama kinachotembea kwenye media ni kweli kuwa ndio soko jipya la k.koo basi nakubaliana nao kabisa wameona mbali.

Hatuwezi kubaki na k.koo tuliyonayo leo ambayo ilijengwa miaka sijui ya 60 au 70 huko tunahitaji soko kama hili ili kuweza ku serve population ya mjini iliyo ongezeko.

Muundo wa majengo mengi ya k.koo na mji wa Dar kwa ujumla kwa sasa hivi ni wa ghotofa tatu kwenda juu.

Wakati K.koo inajengwa maeneo mengi ya Dar nyumba zilikuwa za bungalow sasa hili ongezeko kubwa la watu linahitaji soko kubwa sana katikati ya mji na wala sio pembezoni ya mji.

Wale wa pembezoni wajengewe masoko ili wasilazimike kuja mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye maelezo ya waziri wa tamisemi. Amesikika akisema kuwa jengo litakuwa na basement ya ghorofa mbili,...achilia mbali ground level floor na ghorofa nne kwenda juu.

Maelezo haya ya kitalaamu tena ya ubunifu yangepaswa kutolewa na wabunifu wa majengo kwani wao ndio wanaojua changamoto zinazojitokeza kwenye ujenzi wa jengo alilolinadi waziri Ummy Mwalimu pamoja na gharama zake.

Hizi kauli za kisiasa kwenye mambo ya kitaaluma kwa lengo la kuwafurahisha wapiga kura mara zote huongeza gharama maradufu.
 
Ccm inatutesa dola million 14 nisawa na billion 32 zakitanzania hapa watanzania Mana yake kwenye thamani yafedha yetu wanaelewa kweli
 
Stand ya mabasi mbezi pamoja na fidia tumetumia bil. 50 soko la magomeni tumetumia bil.3

Kwa hizi bil 32 za mama tungejenga Kariakoo moja Dar nyingine Mbeya, Arusha, Mwanza na Ruvuma Songea.

Muda si mrefu utasikia mfereji wa milioni 700, karavati ya bil 1 na darasa la milioni 400
 
Mkiambiwa katiba mpya inahitajikika hakuna anaejali ,mnaamini kwenye mtu binafsi baadala ya kuamini kwenye taasisi.Nchi ingekuwa na muongozo wa kila raisi atafuata misingi na mipango aliyoikuta na uajibishwaji kwa kila mmoja atakae fisadi aku kufanya jambo lolote.
 
Duh! Una akili kama mchwa braza! Sema ukileta akiki zako hizi kwa wale jamaa utakuwa unaleta hujuma kali kwa matumbo yao!
 
Litakuwa na zile bidhaa zote zilizoungua
 
Leo asunuhi nimeijiwa na wazo la ajabu wakati najiandaa kwenda ibadani, hivi tukitangaza kuuza kipande kimoja wapo cha sehemu ya ardhi yetu mfano Kigamboni mzima tukatangaza kuwa inauzwa; mfano dola bilioni 100 tu, na atakayenunua awalipe wenye ardhi pale.

Hivi si ndo utakuwa mwisho wa umaskini na kulipa madeni yote tunayodaiwa?

Sjui niliwaza vizuri!! Yaani kuliko kuendelea na umasikini huu wa kifala bora tuuze viwilaya kama viwili vitatu kwa anayetaka,kisha hela ile tumalize changamoto zote watu tuishi maisha mazuri kuliko maisha haya ya kuvaa barakoa kinafiki ili tupewe katilioni kamoja nukta tatu kakutudhalilisha.
 
Ungehoji Kwanza na ule uwanja wa ndege chato wa billion 40 una faida gani kwenu wasukuma
 
Ndugu Zanzibar-ASP:

Kwani kuna mtu amesema ikijengwa Kariakoo kunazuiwa kujengwa masoko mengine pembezoni mwa miji kulingana na uhitaji wa watu..?

Mimi nadhani tunaongelea soko la Kariakoo kama soko mama na kubwa la yote na kama soko la kimataifa
 
Una akili nyingi sana
 
Toka ulivyomsapoti yule dictator basi sina imani wala amani na wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…