Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Swali Fyatu la Mwezi: Wakimpa Sifa Zake, Watapunguza za Kwao?

Kutoka moyoni kabisa, jiwe ameirudisha nchi hii miaka 50 nyuma . Ameinajisi nchi hii kiasi kwamba ktk muda wa miaka 5 amejenga nyufa za kijamii, kisiasa na kiuchumi

Matatizo ya kiuchumi tunayopitia Sasa yametengenezwa na jiwe. Aliwachukia wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa hata akatamaka hadharani kuwa wataishi kama mashetani.

Kauli ya kishenzi na kifedhuli kabisa. Mpuunzi mkubwa huyu. Hakujua kuwa hawa ndiyo miyo ya uchumi na watoa ajira wakubwa. Ndiyo mpk leo mama anahangaika kuurejesha uchumi ktk mstari.

Kijamii na kisiasa kila mtu anajua jinsi jiwe alivyoivua nguo nchi hii. Kwahiyo siandiki kitu.

Kumsifia jiwe kunahitaji mtu kuwa na roho ya usherani
Mimi nakubaliana nawe kwa kiasi fulani kuwa mwendazake John P. Magufuli alikuwa na mapungufu yake mengi kiuongozi hususani katika eneo la UTU, DEMOKRASIA, HESHIMA na ni mtu ambaye hakuwa na SUBIRA wala UVUMILIVU na HAKUAMINI KTK KUSHUGHULIKIA MAMBO KWA KUFUATA UTARATIBU WA KISHERIA NA KIKATIBA kwa watu wake...

Aliamini kuwa yeye ndiye MWANZO na MWISHO wa kila kitu katika nchi hii. Kwa sababu ya imani yake hii, John P. Magufuli akawa na kiburi na kuanza ku - abuse madaraka na mamlaka yake ya u - Rais. Hii ilikuwa ni kasoro kubwa kwa kiongozi huyu na ubaya wake huu unafunika mazuri mengi aliyofanya..!!

Lakini pia it's not fair at all kutompa sifa katika maeneo aliyofanya vizuri. Mojawapo ni uamuzi wake wa kuuweka ktk vitendo uamuzi wa kuhamishia makao makuu (ikulu) ya serikali Dodoma ulioshindikana kwa miaka takribani 55 ya uhuru. Huu ulikuwa uamuzi sahihi na mzuri sana..

Yako mengine mengi mazuri ambayo serikali aliyoiongoza wakati wake ilichukua maamuzi ya kuyatekeleza. Mfano ujenzi wa reli ya SGR. Hili Mimi nampongeza sana huko alipo. It was a bold and good decision..

Yako maamuzi mengine mabaya sana aliyofanya.

Mfano;
✓ Kuminya uhuru wa watu wa kujiamulia mambo yao, kukusanyika na kujieleza yaani DEMOKRASIA. That was a grave mistake..!

✓ Kuua au kuwaumiza watu waliokuwa wanakosoa mbinu na style ya utawala/uongozi wake Kwa kutumia njia mbalimbali..

✓ Kupuuza taratinu, sheria na katiba ya nchi katika serikali yake kuanzia ma - DCs, RCs, mawaziri na hadi yeye mwenyewe Rais walipokuwa wakitenda majukumu yao ya kiutawala...

Ubaguzi wa kikabila na kieneo na wa kiitikadi za kisiasa katika kuwahudumia watu. Mathalani kwenye hili aliwahi kusema akiwa maeneo mbalimbali ya nchi kuwa kama watu wa eneo hilo watakuwa na kiongozi asiyetokana na chama chake cha CCM, basi yeye kama Rais wa nchi hangewapelekea huduma bora za kijamii kama Maji, umeme, elimu nk nk.. This was too bad indeed..!

✓ Si tu ubaguzi, Rais Magufuli alikuwa hulka ya upendeleo kwa misingi ya ukabila na urafiki na kama ungependa kumwabudu..

## Hayo☝️☝️☝️☝️yote na mengine yaliharibu kabisa upande wote wa sifa njema ya ujasiri katika kufanya maamuzi aliokuwa. Na whether tunapenda au hatupendi, mtu yeyote achilia mbali kiongozi kama Rais akiwa na tabia hizo, asitegemee kufika mbali..

Huyu ndiye alikuwa John P. Magufuli. Alikuwa na UZURI na pia UBAYA wake.

🙏🙏🙏🙏🙏
 
Maridhiano ya kitu Gani na ni ya nani na nani aliyefanywa kitu Gani? Ni maigizo matupu ya kujaribu kutuhadaa ati Kuna kitu kiliharibiwa na sasa wanarekebisha. Haya tufanye huo uchaguzi uliharibiwa, vipi usingeharibiwa ndo ingekuwaje? Mfano mbunge wa Mbeya mjini angekuwa Sugu badala ya Tulia ndo Ingekuwa Nini? Acheni maigizo ya kijinga na hata kama hampendi kusikia lakini JPM hawezi kupotezwa na chuki zenu zisizo na miguu Wala kichwa. Ni bahati mbaya hatunaye, lakini kazi alizofanya zipo na zinaonekana.
Nyie ndo mnalazimisha tumsifie wakati kuna mambo ya kijinga yalifanyika kwenye utawala wake. Uwanja wa ndege wa Chato una faida gani kwa taifa? Hata hiyo ikulu ya Dodoma ni kuongeza tu gharama kwa Taifa wakati ya Dar ipo. Marais waliopita hawakuwa wajinga kuendelea kuwepo Dar. Waziri wa fedha enzi za mwalimu Amir Jamal alitahadharisha sana kuhusu gharama za kuhamia Dodoma na zoezi akasikilizwa... enzi zile kulikuwa na unafuu kuliko sasa hivi lakini bado ikaonekana ni gharama... sasa from nowhere anajitokeza mtu anakomba hazina kwa mambo ambayo hayakuwa kwenye mipango ya nchi. SUKUMA GANG KAENI KIMYA
 
Kwa hiyo kwa akili zako, mfano Mwl. Nyerere aliyerithi nchi ikiwa na madaktari wa binadamu wawili,angeacha kusomesha watu na badala yake angeweka juhudi ahamie Dodoma? Kama siyo uamuzi wa kijasiri kusomesha watu Bure mpaka chuo kikuu, hata wewe na huyo JPM tusingemjua.
Kupanga ni kuchagua, siyo kukurupuka na kila kinachokuja kichwani. Leo man jeuri, mnasema tumejenga wenyewe bila kutumia wataalam kutoka nje, kwa sababu watu (human resources) waliandaliwa.
Nyerere alijua tunayo dhahabu na hakuichimba kwa kigezo cha kutokuwa na wataalam wa kusimama shughuli za uchimbaji.
Kila jambo hutendeka kutegemea wakati husika na mahitaji. Unapoona bwawa la Nyerere ni suluhisho la matatizo ya umeme wapo wanaona tofauti,wao wanaona gesi ndio suluhisho.


Mimi binafsi sina kingine zaidi ya heshima kuu kwa Mwalimu JK Nyelele,

yeye ndio Rais bora kabisa kwangu then anakuja JPM,

hapo nilikuwa nazungumzia marais waliofuata baada ya Mwalimu......vile vile sikuwa na lengo la kudharau mambo mengine mazuri yaliyofanywa na marais wengine ila nilikuwa namuweka tu sawa huyo jamaa aliyesema kwamba mwisho wa siku kodi za wananchi ndio zinazitumika kufanya hiyo miradi..... ndio nikamjibu hivyo



Na Mwisho kabisa,umeme wa gas kwetu hauwezi kuwa nafuu kufananisha na umeme wa maji kwa kuwa hiyo gas ingawa ipo ndani ya nchi yetu lakini si mali yetu tena ....yaani ni kama unavyoona mchango wa madini kwenye maendeleo ya Taifa hili ulivyo mdogo pamoja na madini yote tuliyonayo
 
View attachment 2642893
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna watu ambao tunawakumbuka kwa umahiri na weledi katika kazi, vipaji au matendo yao. Michael Jordan aliichezea timu ya mpira wa vikapu ya Chicago Bulls na kujionesha kuwa ni mchezaji bora Zaidi wa mchezo huo duniani. Wengi wanalijua jina la Michael Jordan lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzake wanne waliokuwa wanaunda kikosi cha kwanza. Hili pia ni kweli kuhusu mchezaji bora Zaidi wa soka duniani Pele. Wengi wanalijua na kukumbuka jinsi Pele alivyoongoza Brazili kwenye makombe ya dunia. Ni wachache sana wanaweza kukutajia wachezaji kumi wengine walioshinda na Pele kombe la dunia mara ya mwisho.

Hata hapa Tanzania kuna watu wanakumbukwa kwa umahiri wao lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya watu wengine kwenye vikosi vyao. Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, au hata Remmy Ongara. Tunajua nyimbo zao, tumewahi kuzisikia lakini tukiuliza wana bendi wenzao ni kina nani ni wachache wanaweza kutaja hata majina mawili.

Ukweli ni kuwa kuna watu wanatokea katika fani mbalimbali na wanakuwa vinara na bora kuliko wengine. Tunapowataja hawa wengine na kuwasifia haina maana tunadharau mchango wa wengine. Ukimtaja Lionel Messi kwa mfano au Cristiano Ronaldo mara moja watu watajua unawazungumzia kina nani lakini ni wachache wanaweza kukutajia majina ya wachezaji wenzao kwenye zile timu zilizokuza majina yao. Unaposema sifa za vinara haina maana unafuta sifa au unadharau sifa za wengine!

Juzi wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Dodoma ambayo sasa inaifanya Ikulu ya Dar-es-Salaam kuwa Ikulu Ndogo kuna watu walisimama na kumwaga sifa mbalimbali. Niliamka mapema (huku niliko) niweze kushuhudia kama watakuwa na ujasiri wa kumtaja mchezaji kinara aliyewafanya wawepo pale siku ile. Bahati mbaya karibu kila aliyesimama ama alinyemelea kulitaja jina la mchezaji huyo bora au alilitaja kama kulipita tu kuwa “alikuwa ni mmoja wa timu”.

Jina la Joseph Pombe Magufuli, kinara wa marais wote waliowahi kutokea Tanzania, shujaa wa uthubutu, na mbunifu wa maono ya maendeleo ya haraka lilitajwa kana kwamba na yeye alikuwa na mchango kama wengine tu. Yote hiyo ilifanywa kwa makusudi kabisa wakijaribu kufifisha jina hilo na hawakutaka kusikia makofi na shangwe ambazo wangelitendea haki zingesikaka. Waliogopa kuona kuwa yumkini huyu bwana akiwa amelala kaburini milele kuna watu wanamkumbuka na kummiss!

Wanatuambia kuwa mpango wa kuhamishia Ikulu ulianza toka miaka ya sitini na hatimaye maamuzi yakachukuliwa na taratibu hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa ili kuhamia taratibu Dodoma. Jakaya Kikwete akatupa stori kuwa aliagiza watu waende Malaysia waone mambo yanavyofanyika huko na sisi tuje kuiga. Sikumbuki kwa miaka kumi ya Kikwete kama kuna siku ulifanyika mjadala hata mmoja Bungeni wa jinsi ya kuhamia Dodoma na kujenga Ikulu Dodoma na kuwa aliwaambia Watanzania kuwa ametuma iende Malaysia! Sijui hiyo timu iliongozwa nan ani! Lakini tunakubali.

Tunaambiwa kuwa viongozi wote waliotangulia wamekuwa wakifanya kama kupokezana vijiti kuliongoza taifa. Wanasahau kuwa Magufuli hakumwachia Samia kijiti; kamwachia gogo! Ni wazi Rais Samia anajitahidi kwa uwezo wake wote kuonekana anaweza kukamilisha miradi hii yote; na kweli tunaona ikimalizwa. Lakini ndugu zetu hawa wanataka tuamine kuwa kama Magufuli asingefanya alivyofanya leo tungekuwa na Ikulu Dodoma au Mji wa Serikali, au miradi hii mingine mikubwa siyo tu ya kimkakati kama inavyoitwa bali ya uthubutu uliopitiliza.

Yaani, kwa miaka Zaidi ya arobaini hawa jamaa walishindwa kuhamia Dodoma walikuwa wanalipia vipindi vya CDA hata sijui tulikuwa tunaambiwa nini. Kwa miaka arobaini walikuwa wanajipanga, na kuandaa ramani, na kuandaa warsha na semina. Kwa miaka arobaini wanaenda Dodoma, usiku usiku wanawahi kurudi Dar, kwa miaka arobaini wanaimba “Dodoma Dodoma” lakini kila wakiama ni “Dar, Dar”.

Akaja Magufuli akasema maneno matupu hayaliwi na upepo haufungwi kanga! Akawakimbiza mchakamchaka watu wazima na majasho hadi kwenye kucha; mambo yakaanza Kwenda. Yaani, yaliyowashindwa kwa miaka arobaini mtu kayaweza kuyasukuma kwa miaka mitano! Halafu wanatuambia “na sisi tulicheza”. Wanasema kweli Pele alifunga goli lakini sisi tulitoa pasi; wanasema Lionel kachukua kombe la dunia lakini sisi tulimbeba! Hatutaki kuwakumbuka!

Sasa wameamua tu kuwa hawamtaja Magufuli kwa sifa zake; hawatamtaja kwa uthubutu wa barabara, meli, mashule, madaraja. Yaani, kuna watu walijenga daraja moja kubwa kwa miaka kumi halafu anakuja mtu anajenga Matano wanajilinganisha naye! “Na sisi tulijenga barabara na sisi tulijenga daraja” msimpe sifa sana yule; alikuwa ati wa kawaida tu. Ni wivu gani huu?

Hivi kweli wakisema sifa za Magufuli kwa haki kabisa, na kusema kuwa alikuwa ni mchezaji nyota wao watapunguziwa sifa zao? Hivi watakapoenda kuwasha umeme wa Bwawa la Nyerere si wataanza kutupigisha stori tena kama za Ikulu! “Oh hili wazo lilikuwa la Nyerere, na sisi wengine tukapokezana vijiti”! Hivi mkimpa sifa Magufuli anazostahili nyinyi mtapungukiwa? Mtaonekana mnamshusha Samia? Au Samia mwenyewe anaweza kuona wivu badala ya kuona Fahari kuwa alikuwa ni sehemu ya miaka mitano ya Magufuli.

Ndio maana ile sauti anayoisikia Rais Samia haikomi. Itaendelea kumlilia na kumkumbusha kutimiza miradi lakini aifanye kwa haki isiwe kana kwamba anaona ana kivuli cha Magufuli. Magufuli akishangiliwa haina maana nay eye hatoshangiliwa; sifa za Magufuli zikiimbwa haina maana za kwake na timu yake hazitaimbwa. Ikulu ya Dodoma wangeachiwa haya ingekuja 2050! Labda wajukuu zao ndio wangeweza kuthubutu! Kama kwa miaka arobaini walichofanikiwa ni kile kilichokuwepo kabla ya Magufuli basi hawa wangeendelea kutenga bajeti ya kula tu kwa kisingizio cha kupanga makao makuu.

Hili ni swali la kwani wakimpa sifa Magufuli wao watapungukiwa naamini bado linahitaji majibu muafaka kwa wakati huu. Ni swali ambalo kama halitajibiwa vyema basi tutajikuta tunaendelea kuliuliza hata kama ni kwa kung’ong’a. Lakini kama siyo wivu, kama siyo kisirani, kama siyo kukereka na kivuli cha Magufuli basi ndugu zetu hawa waanze kuwa wa kweli; mnyonge mnyongeni sifa zake mpeni; hata kama mnaona zinawapunguzia zenu. Siyo ndivyo haki yenyewe hiyo.

Kwa hiyo basi natangaza hadharani, Ikulu na uamuzi wa kuharakisha kuhamia Dodoma sasa hivi na maendeleo yote ya ujenzi tunayoyaona ni matokeo ya uthubutu, maono, na kujituma kwa Rais wa Awamu ya Tano John Joseph Pombe Magufuli. Mchango wake haulinganishwa na Rais mwingine yeyote kabla yake na baada yake. Anayebisha asimame. Wangekuwa na uwezo na uthubutu huo; wangekuwa wamehamia Dodoma miaka 40 nyuma!

Niandikie:klhnews@gmail.com
Najaribu kujiuliza hizi sifa mnazolazimisha nyerere angelazimisha ingekuaje????? Hivi vitu vipo kwa ajili ya watanzania na vimejengwa kwa kidi zetu. Mbaya zqidi tunazihudumia kwa kodi sasa cha ajabu nn??
 
Lakini pia it's not fair at all kutompa sifa katika maeneo aliyofanya vizuri. Mojawapo ni uamuzi wake wa kuuweka ktk vitendo uamuzi wa kuhamishia makao makuu (ikulu) ya serikali Dodoma ulioshindikana kwa miaka takribani 55 ya uhuru. Huu ulikuwa uamuzi sahihi na mzuri sana..

Yako mengine mengi mazuri ambayo serikali aliyoiongoza wakati wake ilichukua maamuzi ya kuyatekeleza. Mfano ujenzi wa reli ya SGR. Hili Mimi nampongeza sana huko alipo. It was a bold and good decision..
Uamuzi wa kuhamia Dodoma ni hasara kwa taifa. Fedha zinapotea bure kufanya jambo ambalo halina tija kwa sasa. Enzi za Nyerere kulikuwa na umuhimu wa makao makuu kuwa Dodoma lkn siyo ktk zama hz ambazo usafiri upo wa anga, reli na barabara nzuri.

SGR ni nzuri lkn alikuwa na pupa na papara nyingi. Kulikuwa hakuna haja ya kuanzisha miradi mingi mikubwa kwa pamoja:-SGR, JNHPP, kuhamia Dodoma , daraja la Busisi n.k.

Mm simkubali hata ktk angle moja.
 
Back
Top Bottom