Basi kifuatacho nadhani kusiwe na Rais kabisa nchi hii.
Kwasababu mnakwepa majukumu ya dhahiri kwa vijisababu vya kijinga tu wakati mnatumbua kodi za walalahoi kwa kazi hiyo.
Yaani pesa na treatment za kifahari zinazotokana na kodi za walalahoi mnataka ila majukumu yake HAMTAKI.
Mtanzania akipigwa marufuku kwenda nchi za ng'ambo anaweza kutatua vipi hali hiyo peke yake ?
( Je, Raia wa kawaida anaweza kurejesha confidence ya nchi kwa watu wa mataifa mengine )
Tunawalaumu China kwa kutodhibiti ugonjwa mpaka unausumbua dunia, leo tena wengine wanapambana, halafu sisi tupo tupo tu tumekaa, tunasubiri wakimaliza, tuwapelekee.
Je, mikusanyiko mikubwa kama shule raia wa kawaida ana nafasi gani hapo bila Mwongozo ??
Je, ukubwa wa Tatizo ukoje hizi taarifa mwananchi wa kawaida anazipataje ili ajilinde. Knowledge is power.
Wewe Jamaa ni mwehu. Magu huyo anaetandika watu risasi 36 na kutaka wakazikwe haraka haraka ndio mwenye imani ya Petro. Yuko wapi Azory Gwanda, Kanguye, Ben Saanane, enyi wacha mungu ??
Sasa kama imani ndio imekuwa kimbilio la Magufuli, hao maaskari wenye mabunduki na helkopter za ulinzi anatembeatembea nazo za nini ??
Anyway, sasa tuanze kutibu MARALIA, TYPHOID, KIPINDU PINDU, UKIMWI, kwa imani ya Petro.
Kila kitu cha wazungu ni kibaya na hakifai isipokuwa pesa zao, mabomu ya machozi, vifaru vya kijeshi, mabunduki, magari ya washa washa, , vx-v8