mama kubwa
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 6,230
- 9,889
Ili kulinda kaheshima kadogo ulikobakiza, ungeacha kuwa unanaandika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hakukukataza ila kasema yeye na serikali yake hawahusiki.Kuna watu wanaona chanjo ya 'corona' inawafaa, lakini hawawezi kuipata kwa sababu mkuu kaikataa!
Mkuu 'Jidu', wakati mwingine tusijitoe akili kirahisi namna hii.
Mwanzo unasema... "sijasoma hadi huko mwisho wa bandiko refu"... Lakini kwenye point na. 5 unasema mwisho amesema..... Sasa ikiwa wewe mwenyewe unajidanganya (halafu kwa akili yako unadhani unatudanganya sisi), nani atakayekyamini hapa??Sijasoma hadi huko mwisho wa bandiko refu.
Hii hapa inatosha kabisa kujua umeandika nini huko.
1. Mstari wa kwanza unajitambulisha kuwa wewe ni "shabiki", hii ina maana unawapotezea muda wasomaji wako wasiokuwa "mashabiki" kama wewe kuendelea kupoteza muda wao kwa kusoma mambo ya 'kishabiki'.
2. Una hakika "unaelewa malengo yake na mitizamo yake"? Huwezi kuwa umepofushwa na "ushabiki" tu ulioutangaza hapa?
3. Unajuaje kwamba hili ni "wimbi la pili la corona" na sio wimbi lile lile la kwanza kutokana na kusitisha juhudi zote za kupambana na corona huko nyuma kwa madai kwamba haipo nchini bila ya ushahidi wowote wa madai hayo.
4. Unaandika kuwa "...kile kinachodaiwa kuwa ni wimbi la pili la maambukizi..., ambayo 'yanasemekana'; kwa nini watu wajadili mambo ambayo huna uhakika nayo wewe mwenyewe. Hii ni sehemu ya kuwavuruga na kuwachanganya akili waTanzania kama anavyofanya huyo unayemshabikia?
5. Mwisho unaandika, kama mtu aliyezinduka toka kwenye ndoto mbaya: "Wapo wengi ambao wanamuangalia Rais awape mwongozo wa nini cha kufanya..." Kwani wewe ungependa wamwangalie kiongozi wao kama "mpotoshaji" kama anavyojipambanua sasa hivi kuwa ndiyo lengo lake hasa kwa haya anayoyasemea juu ya ugonjwa huu na kutaka waTanzania waamini kuwa 'wazungu' kwa ujumla wao lengo lao ni kuwaangamiza watu weusi?
Naona hii itakuwa ni 'awamu ya pili' ya mkataba ulioingia na huyo mtu wako kwa kzai hii chafu ya kuwavuruga akili waTanzania.
Nchi inaingia vitani, nyinyi mnasema watu wafanye ya kwao wasimsikilize Jemadari mkuu; hiyo itakuwa vita ya namna gani.
Kuna wengine wanamuona ni mungu kabisa.Sisi wengine tunaamini baada ya Mungu ni Magufuli, huyu ameweza yasiyowezekana, ametuomba Watanzania tumuondolee magunzi (Wapinzani) tumeyaondowa yote tumempa safu ya kijani tupu, bunge la kijani.
Tuna imani kubwa na jemedari wetu na tumekubali kumkabidhi maisha yetu awe na ubia nayo.
Je vipi wewe shabiki wake? Unashabikia lipi mpaka uwe na mawazo mbadala badala ya kuandika mapambio?
Hypocrite.
Watanzania ni maskini wa kutupwa, tusije kufa kwa njaa
Uko sawa kabisa, Mimi wasiwasi wangu ni uwezo wa Mwananchi kumudu kula yake ya kila siku akiwa locked ndani.Ninachoamini ni kwamba ikitokea Corona umechanganya (Mola apishie mbali) watu wakaanza kudondoka kila kona, watu watajifungia wenyewe bila shuruti...
[emoji706][emoji706][emoji706]Rais wetu mwanasayansi..sasa tusimsikilize?
Tuwasikilize mabeberu?
Hiyo ilikuwa ni kauli ya Kisiasa tu, hakuna lolote. Watanzania ni Maskini wa Kutupwa."Watanzania ni matajiri sana na tunapaswa kutembea vifua mbele" In Magu voice [emoji16][emoji16][emoji16]
Ili niyasimulie matendo makuu ya BWANA.Sitakufa bali nitaishi.
Wewe nawe anti-vaxxer kama Magufuli?Korona 2.0 Kwani Rais ana Ubia na Maisha Yenu?
Na. M. M. Mwanakijiji
Naandika kama shabiki wa Magufuli; naandika kama mtu ambaye nimeelewa malengo yake na mitazamo yake, na ninaandika kama mtu ambaye sijaegesha akili yangu mahali mwenyewe nikaondoka. Nimesoma na kufuatilia mijadala ya kile kinachodaiwa kuwa ni wimbi la pili (2.0) la maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) ambayo yanasemekana yanaendelea nchini mwetu. Wapo wengi ambao wanamuangalia Rais awape mwongozo wa nini cha kufanya na kwa kiasi kikubwa wanafanya hivyo kwa sababu Rais ndio kiongozi mkuu wa serikali na nchi.
Neno la Rais lina uzito wake, hofu za Rais zina uzito wake na ikumbukwe kuwa wengi wanachukulia kuwa kwa vile Rais ana watu wengi wanaomzunguka basi ana taarifa za mambo mengi ambayo labda watu nje ya serikali hawana. Aliposema watu wajifukize, mamilioni walijifukiza, aliposema watu wafunge na kuomba, watu walifunga na kuomba, aliposema watu waiage korona watu walifanya na send off! Na alipotangaza kuwa korona hakuna Tanzania na kuwa imekwisha watu waliamini hivyo.
Sasa hili wimbi la pili ni kweli? Kama ni kweli je Watanzania wafanye nini? Je, watu wanaokufa ni kweli wote wanakufa kwa korona au magonjwa mengine? Na kama wimbi hili kweli lipo kama nchi tufanye nini na kama mtu mmoja mmoja tufanye nini? Ni wazi msimamo wa serikali umetolewa na Rais jana huko Chato na kuwa hakuna mtendaji wa serikali atakayepingana na Rais kwenye hili isipokuwa kama yuko tayari kujiuzulu akipinga (resigning in protest). Kwa vile msimamo wa serikali unajulikana na kuwa serikali haitaleta lock down, na kuwa hata chanjo watu wafikirie mara mbilimbili basi sehemu ya nini kila mtu afanye ndio swali linalohitaji kujibiwa.
Ndugu zangu naandika kama shabiki; Watanzania msijitoe ufahamu na mkajifanya nyie fyatu! Rais si mbia wa maisha yenu, ya mababa na mama zenu, na wala si mbia wa maisha ya watoto wenu! Mnapougua, kuuguza na kuuguliwa yote hayo ni yenu; mauti yakiwafikia vilio ni kwenye nyumba zenu, jamaa, ndugu na marafiki zenu. Sasa kama hili ni kweli, kwanini watu wengine wafikiri wanaweza kuifanyia ibada imani ya mtu mwingine? Hivi, mnajua kwanini mitume wengine hawakuungana na Petro kujaribu kutembea juu ya maji japo wote walimuona Yesu akitembea juu ya maji na walimsikia Yesu akimwambia Petro atembee? (Mathayo 14:22-33).
View attachment 1687880
Rais Magufuli anaweza kuwa na imani kubwa kabisa hata ya kutembea juu ya maji na akatembea; lakini wangapi wanaamini kama yeye? Kama imani yako haijafikia ile ya Magufuli sasa unakanyaga maji ya nini?
Ndugu zangu kuna njia tatu/nne kubwa na za haraka za kupunguza maambukizi ya corona:
1. Vaa barakoa iliyotengenezwa na kitambaa cha pamba (siyo hariri). Kuvaa barakoa kuna kulinda wewe na kinamlinda mwingine. Ukivaa barakoa funika pua na mdomo (korona inaingia zaidi kupitia puani!)
2. Osha mikono kwa sabuni mara kwa mara; epuka kusalimiana na watu kwa kushikana mikono. Ikitokea hivyo hakikisha huingiza vidole midomoni au puani (jitahidi kuosha kabla ya kufanya hivyo na baada).
3. Jiweke umbali wa karibu mita moja kutoka kwa mtu mwingine ambaye si wa nyumbani mwako. Na hii inaendana na kuepuka misongamano isiyo ya lazima hasa mahali ambapo watu hawavai barakoa. Na wale wenye ndugu (wazazi, mababu wazee) waambieni wasiende makanisani au misikitini kwa wakati huu au makanisa na misikiti iweke taratibu za kuhakikisha watu wanakaa mbalimbali na wanavaa barakoa!
4. Jifukize nyungu; sijui ni kwa namna gani hii ilisaidie kuzuia wimbi la kwanza lakini kama watu watafanya tena na kwa wingi wao mnaweza kujikuta mnazuia tena wimbi hili la pili maana kama ni chanjo msijipe matumaini saini.
Njia hizo tatu ndio njia zitakazokinga maisha yako na maisha ya wale uwapendeo. Lakini kama unafikiria Rais ana ubia na maisha yako haya we. Kwa sababu lile swali la bahati nasibu ya Magufuli kama italipa bado linasimama.
Unataka tu tuendeleze majibishano yasiyokuwa na tija.Mkuu hakukukataza ila kasema yeye na serikali yake hawahusiki.
Hiyo "mwisho" umeelewa maana yake?Mwanzo unasema... "sijasoma hadi huko mwisho wa bandiko refu"... Lakini kwenye point na. 5 unasema mwisho amesema..... Sasa ikiwa wewe mwenyewe unajidanganya (halafu kwa akili yako unadhani unatudanganya sisi), nani atakayekyamini hapa??
Mbona mkuu amesha kuambia, wale wa kwenda wameenda na baada ya kuchanjwa walikokwenda wamerudi na covid21( waliikwepa covid19).Unataka tu tuendeleze majibishano yasiyokuwa na tija.
Hao wanaoitaka wataipata wapi iwapo mwenye nchi yake kaikataa?
Sawa mkuu ila mimi naamanisha hawa viongozi wetu ...Samahani mkuu 'Sem2708' naomba nikuulize swali:
Hivi kila aliyepo kwenye uongozi na katika vyama vinavyojitambilsha kuwa vya siasa ni lazima ajulikane kuwa ni "Mwanasiasa"?
Hakuna vigezo maalum vinavyohitajika kuwa navyo mhusika kutambulika kuwa yeye ni 'mwanasiasa'?
Akina Amin Dada, Bokassa, Mobutu, n.k., wote hawa wanajulikana kuwa walikuwa 'wanasiasa', kwa sifa tu ya kuwa kwenye nafasi ya uongozi wa nchi?
Hili neno "Mwanasiasa" ninaliona kuwa lina utata mkubwa. Mi nadhani kuna vigezo vinavyompambanua mhusika kuwa ni mwanasiasa, mbali ya yeye kuwa tu kwenye madaraka ya juu nchini.
Simwoni Magufuli kuwa ni mwanasiasa, kwa sababu haonyeshi dalili yoyote ya kuwa mwanasiasa.