KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Eeenh.Serikali ilichukua hatua kwa kufuata miongozo ya WHO ili kumlinda Rais wa nchi hivyo idara za usalama zilimpeleka Rais Chato kwa lock down isiyo rasmi kwa miezi mitatu, huku msisitizo ukitolewa wa tahadhari kubwa na njia mbadala yakupambana na Covid 19.
Mkuu BonT, umetusemea wengi kwa ufasaha kabisa.Maoni aina hii nimeyasikia sehemu nyingi sana kutoka kwa watetezi wa mfumo! Mnachoshau ni kwamba, maoni yenu ni applicable kwa watu wa mitandaoni hususani JF na Twitter ndio ambao wana access to mass information ya kile kinachoendelea duniani kote! Wale wenzangu mimi hata huo muda wa kusikiliza redio hawana! Halaiki hii hawana taaqrifa za kitaalamu kwa sabbabu wataalamu wetu hawawezi kwenda kinyume na matamko ya rais! Matokeo yake, kauli kama chanjo zawazungu ni uongo mtupu ndizo zinazowafikia wananchi wengi kwa sababu ndizo taarifa zinazosambazwa na traditional media! Taarifa kutoka kwa wana mamlaka kwamba hakuna korona ndizo zinawafikia wananchi walio wengi! Sasa hao huwezi kuwaambia eti watumie hizo suggestions zako wakati taarifa wanazopata wao ni kwamba mambo ni shwari, na hao mabeberu ni wivu wao tu wa kutaka kupigana nasi kiuchumi ndo maana wanasema kuna korona ukweli lakini ukweli ni kwamba WANAWATISHA TU, korona HAKUNA!!
Nimekuelewa vizuri tu, sijui hao washauri kama wamepita hapa.Basi kifuatacho nadhani kusiwe na Rais kabisa nchi hii.
Kwasababu mnakwepa majukumu ya dhahiri kwa vijisababu vya kijinga tu wakati mnatumbua kodi za walalahoi kwa kazi hiyo.
Yaani pesa na treatment za kifahari zinazotokana na kodi za walalahoi mnataka ila majukumu yake HAMTAKI.
Mtanzania akipigwa marufuku kwenda nchi za ng'ambo anaweza kutatua vipi hali hiyo peke yake ?
( Je, Raia wa kawaida anaweza kurejesha confidence ya nchi kwa watu wa mataifa mengine )
Tunawalaumu China kwa kutodhibiti ugonjwa mpaka unausumbua dunia, leo tena wengine wanapambana, halafu sisi tupo tupo tu tumekaa, tunasubiri wakimaliza, tuwapelekee.
Je, mikusanyiko mikubwa kama shule raia wa kawaida ana nafasi gani hapo bila Mwongozo ??
Je, ukubwa wa Tatizo ukoje hizi taarifa mwananchi wa kawaida anazipataje ili ajilinde. Knowledge is power.
Wewe Jamaa ni mwehu. Magu huyo anaetandika watu risasi 36 na kutaka wakazikwe haraka haraka ndio mwenye imani ya Petro. Yuko wapi Azory Gwanda, Kanguye, Ben Saanane, enyi wacha mungu ??
Sasa kama imani ndio imekuwa kimbilio la Magufuli, hao maaskari wenye mabunduki na helkopter za ulinzi anatembeatembea nazo za nini ??
Anyway, sasa tuanze kutibu MARALIA, TYPHOID, KIPINDU PINDU, UKIMWI, kwa imani ya Petro.
Kila kitu cha wazungu ni kibaya na hakifai isipokuwa pesa zao, mabomu ya machozi, vifaru vya kijeshi, mabunduki, magari ya washa washa, , vx-v8
Mfano wa Petro umenichekesha saaana 😃😃😃 kwamba wenzake walimtoa chambo kwanza
Hapo ndipo uone ubinafsi wa wana siasaEeenh.
Kumbe yeye yupo "lockdown", huku akiwatangazia waTanzania kinyume chake?
Samahani mkuu 'Sem2708' naomba nikuulize swali:Hapo ndipo uone ubinafsi wa wana siasa
Kuna watu wanaona chanjo ya 'corona' inawafaa, lakini hawawezi kuipata kwa sababu mkuu kaikataa!Leo mtu ukiona maisha yako yakuwa taken for granted, unaamua unavyoona inakufaa!
Ninachoamini ni kwamba ikitokea Corona umechanganya (Mola apishie mbali) watu wakaanza kudondoka kila kona, watu watajifungia wenyewe bila shuruti...Rais Magufuli anajua anachokifanya, pia anajua kuna Covid19 phase II. Ila ameona athari za kuruhusu lockdown ya Nchi nzima kama wengine wanavyofanya itaathiri Sana Raia wake kuliko kutoweka lockdown.
Watanzania ni maskini wa kutupwa, tusije kufa kwa njaa kabla ya Corona.
Muhimu alichosema ni kuchukua tahadhali za kujikinga. Tahadhari ulizosema hapo juu ni muhimu zikachukuliwa na kila mwananchi,
Ila kulikuwa na haja yeye Kama Amiri jeshi Mkuu aseme kwa kusisitiza kuhusu hilo.