Swali Gomvi: Korona 2.0 kwani Rais Magufuli ni mbia wa maisha yenu?

Hapo ndio serikali imetangaza kuna corona na inachukua hatua za kupunguza maambukizi ila wananchi wenye sasa walichokuwa wanafanya.
 
Siyo lazima kuwe na lockdown wala curfew kwa kila mtu. Serikali inaweza kuruhusu hata, upimaji, 'community awareness' na kuweka restrictions mipakani.
 
Siyo lazima kuwe na lockdown wala curfew kwa kila mtu. Serikali inaweza kuruhusu hata, upimaji, 'community awareness' na kuweka restrictions mipakani.
Uko sahihi, nadhani tukifanya hivyo itasaidia mno kuenea.

Swali ni Je, Waziri wa Afya haoni umuhimu wa haya uliyosema na akamshauri boss wake??

Hata Waziri mpendwa wa JPM bwana Kabudi haoni hilo na kumshauri wakati wa vikao vyao
 
Uko sahihi, nadhani tukifanya hivyo itasaidia mno kuenea.

Swali ni Je, Waziri wa Afya haoni umuhimu wa haya uliyosema na akamshauri boss wake??

Hata Waziri mpendwa wa JPM bwana Kabudi haoni hilo na kumshauri wakati wa vikao vyao
Magufuli HASHAURIKI na ameshakuwa sugu kutomsikiliza yeyote.

Kuwa mpendwa wa Magufuli maana yake ni kufanya kila anachotaka, au kufanya kile utakachoona kitamfurahisha.
 
Magufuli HASHAURIKI na ameshakuwa sugu kutomsikiliza yeyote.

Kuwa mpendwa wa Magufuli maana yake ni kufanya kila anachotaka, au kufanya kile utakachoona kitamfurahisha.
Basi ni hatari

Nakumbuka kwenye kitabu cha Yona kwenye agano la Kale tuliona adhabu ya Mungu kwa watu ambao wanashindwa kutii maagizo ya Mungu.

Ingekuwa enzi zile kwenye ugonjwa wa hatari kama huu wa Covid19, ilikuwa Mfalme anauguliwa na mpendwa wake mmoja au yeye mwenyewe, hapo ingemlazimu kubadilisha maamuzi na kuangalia Utaalamu.

Bahati Mbaya Jiwe huwa haliugui kwa sababu ni Non organism
 
Hujui kuna Toba?
 
Hujui kuna Toba?
Kikristo Toba haifanywi hivyo Mkuu.

Kwanza unapaswa kukiri kosa, kufanya toba na kuomba msamaha kwa uliowakosea na mwishowe ukubali kutorudia makosa.
 
Mwanakijiji you're talking nonsense, Magufuli should be made responsible for the majority of covid deaths in TZ because of his attitude towards the desease.
 
Ndugu Mwanakijiji,

Kwanza, nadhani hujamtendea haki Magufuli kwa kujiita SHABIKI wake. Shabiki wa kweli huwa mkweli kwa anachoshabikia. Shabiki wa kweli wa Simba, kwa mfano, hawezi kushangilia timu hiyo ikitaka kusajili mchezaji mbovu bali atajitahidi kupaza sauti ili wahusika wachukue hatua stahili.

Kwa mantiki hiyohiyo, laiti ungekuwa shabiki wa kweli wa Magufuli, mada yako isingelenga "kuwazodoa" wananchi anaowaongoza na badala yake ungejikita kwenye kauli za huyo unayedai kumshabikia.

Lakini pengine si vibaya kukumbushia kwamba mie na wewe tulikuwa "njia moja" mwaka 2015 kumnadi Magufuli kwa sababu zilizokuwa wazi kwa wakati huo. Hata hivyo, baada ya kumnadi mwanasiasa wakati wa kampeni hakumaanishi ubaki mfungwa wake milele hata anapokosea, baadhi yetu tulijiweka kando baada ya kubaini mwenendo usioridhisha wa mwanasiasa tuliemnadi kwenye kampeni. Lakini baadhi ya wenzetu sio tu mmebaki wafuasi watiifu wa Magufuli - na hili si kosa - bali pia mmejitoa ufahamu na kuwa kwenye "campaign mode" indefinitely. Nachomaanisha hapa ni kwamba wakati wa kampeni si mwafaka kumkosoa mgombea wako, lakini ni hujuma dhidi yake endapo mfuasi atakalia kimya "utopolo" wa mwanasiasa anayemuunga mkono.

Turejee kwenye bandiko lako. Usingejitoa ufahamu, usingekimbilia kuongelea watendewa (objects) badala ya mtendaji (subject). Wananchi "unaowalaumu" hawajatoa hotuba kudai kwamba "Rais Magufuli anatukwaza kwenye vita dhidi ya korona." Sote twafahamu - ikiwa ni pamoja na wenzetu mliojitoa ufahamu - kuwa Ni Rais Magufuli anayejibidiisha kuwavunja moyo wale wote wanaojaribu kuichukulia korona kama janga hatari. Na sasa ni kama amewaambukiza ninyi wafuasi wake, maana Mwanakijiji nayemjua mie si mtu wa kujifanya haelewi hali ya korona ikoje nchini Tanzania. Lakini hata kama angekuwa haelewi, ukaazi wake nchini Marekani ambako korona inatafuna uhai kama moto mkali kwenye nyasi ungempa uzalendo wa "kumtolea jicho" kila COVIDIOT, iwe huko Marekani au kwetu Tanzania.

Mnaweza kuendelea kuwa mashabiki wa Magufuli lakini pia mkamshauri, kama si kumkemea, bali anapokwenda ndivyo sivyo. Na position yake katika korona imekuwa na athari zaidi kuliko faida. Athari hizo hazifahamiki kwa sababu hakuna chombo cha habari kinachoruhusiwa kuripoti, kwa mfano, watu wangapi hadi sasa wana maambukizi ya korona au kutaja idadi ya vifo. Serikali inayoficha idadi ya vifo isivyohusika navyo haiwezi kuwa wazi kwa vifo vilivyosababishwa na serikali hiyo. Hii sio sayansi ya roketi. Serikali inayohadaa wananchi wake kwa janga ambalo sio kosa lake, haiwezi kuwa mkweli kwenye janga ilililosababisha.

Kwahiyo badala ya kuwazodoa wananchi kwamba Magufuli hana ubia na maisha ya Watanzania - kana kwamba sio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - ulipaswa kumshauri huyo unayedai kumshabikia kuwa kukaa kimya nako ni busara. Lakini pia ungeweza kumkosoa kwenye kauli yake fyongo kuhusu CHANJO. Kudai chanjo si salama, ilhali takriban kila Mtanzania - ikiwa ni pamoja na Magufuli mwenyewe - alichanjwa udogoni sio tu ni suala linaloweza kuzua taharuki bali pia laweza kuwa na athari kubwa kwa mamilioni ya watoto na akinamama. Najua mtamtetea kuwa "alimaanisha chanjo ya korona," lakini yeye kama si mdau wa uhai wa Watanzania -kama bandiko lako linavyojaribu kutushawishi - kwanini basi awashikie akili Watanzania wenzake zaidi ya milioni 59?

Nihitimishe kwa kuwashauri wapambe kindakindaki kuwa mwaweza kuwa na msaada zaidi kwa huyo mnayemshabikia endapo mtampongeza pale anapostahili na kummosoa pale inapobidi. Katika hili la korona, ushauri wenu unahitajika sana ili Magufuli aongozwe sio tu na busara bali pia kama mwanasayansi azingatie sayansi pia.

Niwie radhi endapo nitakuwa nimekukwaza.
 
Ahsante shabiki wa Magufuli
 

Mkuu ni haki yako kuwa shabiki wa Magufuli lakini si vyema kutaka kuhalalisha (rationalize) ubovu na mkanganyiko wa uongozi wake kwa kutuchokoza (provoke) kuwa Magufuli hana ubia na sisi wananchi wake katika afya zetu. Yaani unamaanisha hawajibiki kwa lolote kuhusu afya za wananchi wake! Tunachokiona ni leadership failure. Period.

Si Watanzania wengi wenye elimu na uelewa mkubwa kama tulio nao sisi wachache tunaosoma na kuchambua taarifa za media mitandaoni kimataifa. Watanzania hawa wanasikiliza sana na kuzingatia kauli za viongozi wao hasa za Mheshimiwa Rais wa wanyonge. Anapowasisitizia kuwa dawa kubwa ya corona ni maombi na kujifukiza; Tanzania tumeishinda corona haipo/ipo kidogo sana; barakoa hazizuii corona tena za kutoka nje zinaweza kuja na vidudu; anabeza wavaa barakoa na kuweka total blackout kuzuia taarifa za uwepo wa corona nchini zisitolewe wala kuzungumzwa, huo si uongozi.

Unapochaguliwa kuwa Rais wa nchi basi automatically una ubia na maisha ya wananchi wako. Wanatarajia uongozi makini dhidi ya majanga makuu ya kitaifa. You have to show leadership.

Mimi Drifter kama mtu binafsi nina nyenzo kibao za kupambanua na kupambana na matatizo yangu. Naweza hata kwenda nchi za mbali kutafuta masuluhisho ya matatizo yangu ikibidi. Lakini mimi si kielelezo cha Mtanzania wa kawaida ambaye kwake maendeleo ni kuwa na bomba la maji la kijiji, shule ya kata, umeme wa REA, nk. Anayetegemea sana kuwasilisha masuala yake binafsi kwa Mwenyekiti wa kijiji/mtaa.

It’s futile to attempt rationalising incoherence for the sake of justifying leadership failure. Huhitaji kututishia “ubia” ili tusihoji mambo muhimu ya kitaifa. We are intelligent sufficiently.
 
Nafikiri hapa swala siyo lock down bali ni conspiracy theories anazokuja nazo kila kukicha.
 
Hakuna anayedeka! Ni jukumu la serikali kupitia kwa waziri wa afya kuwaambia umma juu ya hali halisi na nn kifanyike. Siyo lazima lock down km Rais anavyojitetea kuwa watu baadhi wanalazimisha lockdown.
Itoshe kukiri kuwa kuna tatizo lenye ukubwa kidogo na mbinu za kushinda ni 1,2,3 nk. Kusema “Siyo kubwa, haipo ni chache sana” nikukanganya umma
 
Long lives Great Thinkers, long lives JF...
 
Erythrocyte huyu ndiye mwenye akili kuliko alilosema mbowe! Acha kushabikia watoa upupu kama Tundu Lissu
 
Kwanza hakuna anaetaka Lock down pia usisahau umaskini huo wao ndio wamewatengenezea watanganyika!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Huwa naandika Mara kwa Mara hapa ...mitachukua muda mrafu MzeeMwanakjiji kurudi katika ubora wake...kupitia andiko hili Leo nasems ...itachukua muda mrefu saana kwa MM kurudi katika ubora wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…