Swali Gomvi: Korona 2.0 kwani Rais Magufuli ni mbia wa maisha yenu?

Kwanza hakuna anaetaka Lock down pia usisahau umaskini huo wao ndio wamewatengenezea watanganyika!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Mkuu usitake kufukua makabuli kuhusu umaskini wetu, muhimu tumshinde adui wetu Corona.

Unajua viongozi wengine wamelala usingizi wa milele, you can do nothing to them
 
Kwa hiyo tuseme katika vita hii hatuna nahodha? Kuwa kila mtu awe na lwake?
Na je kazi za Rais wa nchi kipindi cha majanga ni zipi? Je mataifa mengine viongozi wao wanachukua hatua gani?.
 

hakuna nchi tam kama tanzania, yaaani tunajiamulia mambo yetu! kuna wale wanawake wa ufipa wao mpaka amsterdam awape mwongozo
 
Kuna watu wanadhania au wanaombea Magufuli abadilike.....JPM Yuko alivyo hawezi kuwa tofauti na alivyo...la maana ni watu kufanya maamuzi wakizingatia ukweli huu. Kawaambia hakuna lockdown, anabeza chanjo, hajakubali uwepo na ukali wa korona..Sasa leo mnataka aamke ale matapishi yake, Mara ya mwisho kukiri amekosea ilikuwa lini!? Amkeni msijitoe ufahamu...Linda maisha Yako, ya ndugu zako....we endekeza kumngojea Magufuli...
 
Wewe mleta mada hujui wajibu wa raisi kwenye issue ya collective effort ya kupambana na pandemic?

Kwamba raisi
1. Aendelee kuachia watalii wanaotoka nchi zenye korona waingie ndani ya nchi Lakini sisi tuendelee kujikinga tu na korona hiyo maana ni issue binafsi?

2. Aendelee kukandia na kudiscourage uvaaji wa barakoa kila apatapo nafasi ya kukutana na hadhara?
 
Tusaidie kumueleza ukweli.

Ushabiki wenu ambao ni unconditional ndiyo unampa nguvu kuendelea kuhatarisha maisha ya wananchi

Sisi wenye access ya mitandao tuna nafuu kujua hali ya korona inaendaje, bali mamilioni ya wananchi wanaotegemea channel za serikali na mainstream media kuelimika na janga hili wapo hatarini maana hawapati taarifa sahihi kutokana serikali kutotaka kutoa elimu sahihi na endelevu ya hili janga.

Raisi anaponda barakoa kila akipata nafasi na anareward tabia ya kutovaa barakoa kwa kuwapongeza wasiozivaa, hapo unaona hakuna shida?
 

Mwanakijiji naona mwaka huu wamekuombea na utaacha ushabiki urudi kama yule Mwanakijiji wa 2007 tunaye mjua
 

Maskini Mzee Mwanakijiji... amepoteza kabisa uwezo wa kufikiri.

Unamtenganishaje JPM Na Urais na majukumu yake .

Kauli ya Rais ni kauli ya kufanyiwa kazi na haiwezi kubezwa hata kidogo . Sasa Mh Rais anapobeza mambo muhimu muhimu kama ya kutoa data za Corona , Matibabu Na hata kubeza Vaccine ni kauli nzito ya kuangamiza jamii.

1. Kauli ya Rais ni Kauli ya Tanzania Na inapelekea watu kutengwa Na wengine duniani , unawezaje kuibeza kwamba iachwe tu .
2. Kauli ya Rais ni msimamo wa nchi unayopelekea watu Kuendelea kukusanyika Na maeneo kama Mashule , masoko Na viwanja vya mipira .. kunaleta maambukizi Na Vifo ambavyo vingeweza kuzuiwa , Tunaweza ku ignore tu eti kisa Mwanakijiji ni shabiki wa JPM .

3. Kauli ya kubeza Vaccine inatufanya tuonekane vituko na kunaweza kuathiri shughuli binafsi za wananchi eti tui ignore tu kisa Mwanakijiji ni shabiki wa JPM..

Sometime you need to be serious .. usije Na utopolo hapa jamvini
 
Magufuli ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika nchi ambayo kauli ya Rais ina nguvu kama Amri ya Mungu, kila litokalo mdomoni mwa Rais lina impact kubwa sana.

Suala hapa sio kuwa "Magufuli habadiliki" bali ninyi wapambe wake mchangie kuleta mabadiliko hayo. Akipita hapa JF na kuona mshauri wake mkuu unawalaumu wananchi kwa "kosa" la kutegemea Magufuli, badala ya kumkosoa yeye anayejaribu kuwaghilibu Watanzania kuwa Korona ni ugonjwa kama malaria tu, ni ngumu kwake kuona haja ya kubadilika.

Kama mnampenda kwa dhati basi msiwe waimba mapambio tu. Ifike mahala mumwambie "hapana, hii sio sawia."

By the way, sidhani kama kuna watu wanaosubiri Magufuli abadilike. "Jiwe halibadiliki" anyway. Kinachotarajiwa na wengine ni angalau kukaa kimya badala ya kuongea utopolo unaogharimu maisha ya watu.
 
Kwa hiyo tuseme katika vita hii hatuna nahodha? Kuwa kila mtu awe na lwake?
Na je kazi za Rais wa nchi kipindi cha majanga ni zipi? Je mataifa mengine viongozi wao wanachukua hatua gani?.
Kwenye Nchi yetu korona haijatangazwa kua ni janga la kitaifa, hata hivyo serikali kupitia wizara ya afya na wadau wengine wakiwepo HPSS walizunguka Tanzania nzima kutoa elimu ya korona, sasa nashangaa watu wanakazana Magufuli, Magufuli... Ndio maana nauliza hamuwezi kuchukua hatua mpaka nahodha aseme? Yaani Magufuli atoe muongozo wa korona ndio uchukue hatua?



Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Wizara ya afya ilishatoa muongozo jinsi ya kujikinga na korona, pia serikali ilitoa njia mbadala ikiwepo kujifukiza na kupiga nyungu. Si hivyo tu bali mashirika yasio ya kiserikali ikiwepo msalaba mwekundu, HPSS nk waliungana na wadau wengine wakiwepo akina mrisho mpoto kuzunguka nchi nzima na kutoa elimu ya korona ..

Katika hali isiyo ya kawaida watu wameziba masikio na kushinikiza Rais aseme, rais aseme... Watu wanaleta politics kwenye afya, ndio maana nikasema wanadeka.. mbona wanavaa kondomu wakienda kuzini? Nani anawafundisha? Ifike wakati siasa zikae pembeni na watu wajifunze kuwajibika. Lawama hazisaidii

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…