Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Umoja wa Kisovieti (USSR au CCCP) taifa lililozaliwa mwaka 1922-1991, lilikuwa ni moja ya taifa lenye nguvu sana duniani lakini lenye mwisho mbaya sana ambao ni aibu kwa watu wake mpaka leo.

Kiuchumi walikuwa wana nguvu sana, kiteknolojia walikuwa mbele, nguvu kubwa ya viwanda, kijeshi walikuwa mbele na mifumo yao ya kitamaduni iliyotokana na ukomunisti ilishawishi dunia kuanzia barani Marekani, Asia hadi Afrika na kubwa ziadi walikuwa na idadi kubwa sana ya watu ambapo takwimu zinasema kwamba walikuwa ni milioni 293.

Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli.

Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25?

CC: chige , FisadiKuu
Huu mjadala ni wa zamani kidogo ila swali kuu katika mada sio gumu kwa mtu ambaye ni mfuatiliaji wa historia na siasa za jiografia. Wachangiaji wengi wametaja sababu zao vile wanavyoona ila ukitaka kulifahamu jibu la swali hilo kwa urahisi zaidi fuatilia ama wasikilize Baltic states; kina Latvia, Lithuania pamoja na Estonia ambao ni members wa NATO hivi sasa.

Jibu lake ni sera ya Urusi ya Revanchism. Hiki ndicho kinachofanya West pamoja na NATO wawe makini nacho sana kuliko pengine kitu chochote kile kinachoihusu Urusi ya sasa.

Revanchism ni sera au mkakati unaotazamia kurejesha ushawishi, milki au maeneo ya kijiografia yaliyopotea kutokana na vita au mabadiliko ya kijamii.

Urusi ni nchi iliyopitia upotevu wa maeneo ya jiografia (territorial losses) kutokana na migogoro na vita kadhaa za kale zilizopelekea mabadiliko ya kisiasa, kijiografia pamoja na siasa za jiografia kwa ujumla wake. Kwa mfano, kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti kunatazamwa na Urusi hivi sasa kama pigo kubwa kwao katika siasa za jiografia (the most serious geopolitical catastrophe) katika karne ya 20.

Hivyo, moja ya mikakati ya Urusi katika karne ya 21 ni kurejesha katika ushawishi wake angalau maeneo kadhaa ya kimkakati yaliyokuwepo ndani ya Umoja wa Kisovieti. Najua baadhi ya watu humu wanaweza wasikubaliane na mimi katika hili ndio maana nilitangulia kusema ukitaka kulifahamu kwa urahisi zaidi jibu la swali lililopo mezani wasikilize Baltic states; kina Latvia, Lithuania pamoja na Estonia.

Kwa sababu gani nimesema Latvia, Lithuania pamoja na Estonia?

Hizo tatu ni miongoni mwa nchi zilizokuwa ndani ya Umoja wa Kisovieti na pia ni miongoni mwa nchi zilizopitia ubeberu ama ukoloni (imperialism) wa Urusi wa karne ya 20.

Estonia kwa mfano:
Tuanzie miaka ya 1910 mwishoni kipindi Estonia inapigania uhuru/utaifa wake dhidi ya Soviet Russia mara baada ya WWI na hatimaye kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka 1920 kati ya Estonia na Soviet Russia (The Treaty of Tartu, 1920). Estonia ilianza kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa kama nchi huru mwaka 1921.

Tuje miaka ya 30 baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Molotov-Ribbentrop kati ya USSR na Adolf Hitler. Kwa wasiofahamu, Stalin aliingia mkataba na Hitler mwaka 1939 ili kugawana [kiushawishi] sehemu kubwa ya Ulaya kupitia vita za kujitanua (expansionism), matokeo yake USSR ilizivamia kijeshi Latvia, Lithuania na Estonia na kuzitwaa ukiwa ni mkakati wa ziada wa kuzirejesha kwenye mipaka yake ya awali kabla ya 1920.

Miaka ya 40 (1944-1945):
USSR ilirejea kuitawala tena Estonia mara baada ya Hitler aliyeivamia USSR na pia aliyekuwa akiikalia kimabavu Estonia kushindwa Vita ya Pili ya Dunia hususani Operation Barbarossa.

Baada ya kuwa chini ya ukoloni wa Moscow (Soviet Union) kwa zaidi ya miaka 40, Estonia ilipata uhuru kwa mara nyingine tena mwaka 1991 (kuvunjika kwa USSR), na hatimaye ilijiunga EU kisha NATO mwaka 2004 kama mkakati wa kujihakikishia usalama wa utaifa na uhuru wake dhidi ya uvamizi mwingine wa Urusi kama ule wa miaka ya 40.

Huo ni mfano mmoja tu (Estonia). Kuna nchi kadhaa za NATO hasa upande wa Ulaya mashariki ambazo pia zimewahi kupitia mambo kama hayo yaliyoikumba Estonia katika historia ya utaifa wake. Ukitaka kupata picha nzuri zaidi kuhusu sera ya Urusi ya Revanchism na kwamba bado ina-exist, angalia kile kilichotokea Crimea mwaka 2014 na kile ambacho Urusi inakifanya mashariki mwa Ukraine hivi sasa. Huo ni mfano mzuri sana.
 
Sawa kabisa,

Lakini kuhusu hiyo sera ya Revanchism nadhani iko kwa kila taifa kubwa hapa duniani (Inherent to any Global and Regional Power) sema kwasababu wengi huwa hamuipendi Urusi kwasababu ambazo mnazifahamu wenyewe na hata kushindwa kukubali kwamba kinachofanywa na Urusi hufanywa na mataifa yote makubwa duniani, tena huenda vibaya zaidi kupita Urusi.

Hicho unachokiita Revanchism, kikawaida ni Imperialism tu sema tumeamua kutumia neno jingine. Haya hebu zingatia haya yafuatayo:
  • Kule Urusi inaitwa Revanchism ambapo kweli Urusi anavunja sheria za kimataifa na kuvamia mataifa halali kijeshi na kujimegea vipande vya nchi, akisingizia analinda usalama wake. Kuhusu Russian Revanchism hili ni kweli kabisa, kila taifa linatakiwa liheshimu Political Independence, Territorial Integrity and Sovereignty of other nations.

  • Kule Israeli wanaiita The Right to Return (Aliya) ambayo inasindikizwa na Genocide kabisa. Tena hiki wengi humu ndani mmekuwa mkikishabikia kwa nguvu kweli kwasababu za kidini na kisiasa. Wazungu wa Ulaya waliotokea Urusi, Poland na Ukraine wanaamini kabisa wana haki ya kuishi kwenye eneo linaloitwa Palestina kuliko jamii za Kiyahudi na kiarabu ambazo zimeishi pale kwa miaka zaidi ya 2000. Hili ni hatari kuliko hata anachokifanya Urusi. Kituko ni ule mfano anaoutoa mwanahistoria wa Israel Illan Pappe kwamba "Most Zionists don't believe in God, yet they believe that he has given them land in the Middle-East". Kituko kingine ni hiki, Hii Revanchism ya Israeli inaungwa mkono na mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa ambayo hayaungi mkono Revanchism ya Urusi kule Ulaya Mashariki. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)

  • Kule Marekani wanaiita Manifest Destiny/The Munroe Doctrine na wote tunajua nini kinazikuta nchi za Western Hermisphere pindi wanaenda kinyume na Marekani. Haijapita hata miaka 50, tangu serikali ya Ronald Reagan ifanye ambacho Vladmir Putin anakifanya leo kule Ulaya Mashariki. Mwaka 1983 alivamia Grenada na kumtoa Waziri Mkuu halali wa nchi Maurice Bishop na kuweka kibaraka wao. Ila zaidi ya hapo, Marekani alituma magaidi kuvamia Nicaragua hadi kupelekea The Contra-Affair. Yote hayo viongozi waandamizi wa Marekani kama William Casey walisema ni kwa ajili ya kulinda maslahi na usalama wa Marekani unaohatarishwa na nchi jirani. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)

  • Kule Uingereza wameipa jina zuri The Commonwealth of Nations ila malengo ni yaleyale, Restoration of the Influence of the British Empire through the backdoor. Ndiyo maana kipindi cha harakati za kupigania uhuru wa Northern Ireland almaarufu kama The Troubles, Uingereza inayojiita nchi ya kidemokrasia ilifanya mauaji ya kutisha ili Northern Ireland isijitoe kwenye The Commonwealth of Nations. Sababu hiihii ya kuamini katika Old Glory ndiyo inazuia harakati za Scotland na Australia kujipatia uhuru wao zenyewe bila kukutwa na mkono wa chuma wa mabwanyenye ya Downing Street. Gough Whitlam waziri mkuu wa Australia alipinduliwa kimabavu na MI6 na CIA pale alipotaka kuiondoa Australia kwenye kambi ya mabeberu na kuifanya isifungamane na upande wowote kwenye Vita Baridi. (Hili la kumtoa Whitlam kibabe halina utofauti na lile Urusi walimfanyia Raisi Viktor Yushenko wa Ukraine)
Mifano iko mingi sana hapa duniani, endapo tutachambua bila kuweka mizania ya upendeleo. Kule Ufaransa wanatumia Francophones System na CFA Franc kutawala nchi za Afrika, ambazo zimelazimishwa zisiwe na Central Bank, na akiba yao yote ya fedha za kigeni iko mikononi mwa Ufaransa ambaye ni lazima wamwombe ruhusa ili watumie akiba yao. Hata Uturuki naye anafanya hivyohivyo kule Cyprus, Greece, Azerbaijan-Armenia, Serbia na Albania, kwa kutumia waislamu wenye asili ya kituruki kuvuruga amani na kueneza ushawishi wake.

MWISHO KABISA: Ambacho Urusi anakifanya kule Ulaya Mashariki ni kinyume na sheria za kimataifa. It's simply Illegal, defies common precepts of decency and I don't condone it. Japo ukweli ni kwamba hakuna taifa kubwa duniani ambalo halifanyi ambacho kile Urusi wanakifanya kulinda maslahi yao aidha ya kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni hata kwa mbinu ambazo ziko kinyume na utaratibu wa sheria za kimataifa ambazo zina mzizi kwenye mkataba wa Westphalia (Treaty of Westphalia) wa mwaka 1648, uliomaliza vita mbaya ya kidini iliyopiganwa miaka 30 baina ya Waprotestanti na Wakatoliki ambao walikuwa wanavutana juu ya mambo hayahaya unayoyasema hapa (Catholic Revanchism and Imperialism).

Mkataba unasisitiza katika kuheshimu, State Sovereignty, Political Independence and Territorial Integrity hata pale ambapo taifa kubwa halikubaliani na falsafa za kisiasa na kidini za taifa dogo.

ENIWEI kwasababu tumeshaamua kuamini kwamba RUSSIA IS A BAD GUY with no legitimate security concerns and interests, na kila kinachofanywa na Wamarekani, Waingereza, Wafaransa na Wayahudi ni sahihi kwasababu ni GOOD-GUYS, basi sidhani kama hata tukifanya mjadala wa miaka 10,000 naweza kukubadilisha.

=====================================================
Ila uhalisia, ni ule ambao Professor John Mearsheimer amekuwa akiusema siku zote kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Kwamba hakuna taifa kubwa takatifu (Benign Hegemony), kwamba liwe na mabavu halafu lisijaribiwe kutumia hayo mabavu kujipatia kila linachokitaka, aidha kijeshi au kwa namna yoyote ile.

Haya Mkuu uwe na siku njema, I rest my case!
 
2024 hii bado mwamba anawanyanyasa tu!.
Ndugu yangu nakushukuru sana kwa haya masifa.

Japo nadhani ulichokisema hapa, kitaamsha maruani ya watu wengi mno ambao hupenda kubishana na mimi siyo kwa kujifunza bali kwa kutaka tu kubishana kwasababu wamebishana, na sababu nyingine wazijuazo wenyewe.

Siku zote huwa nasema kwamba muda ni mwalimu mzuri mno. Huu uzi niliuandika mwaka 2018, mwaka 2022 vita vya Ukraine inapoanza watu walinivamia sana wakinitafuta na kusema mimi napiga propaganda na nilidanganya ummah. Walisema kwamba Urusi inashindwa vita na ingeenda kuanguka kiuchumi na kupasuka vipande.

Nilikuwa natumiwa mamia ya NOTIFICATIONS za MENTION nyingi zikiwa zimejaa matusi, kejeli na kebhehi, lakini sikuweza kuwajibu sana na niliishia kucheka tu, nikifahamu fika kwamba hata ashuke malaika nisingeweza kuwashawishi chochote. Ikafika hata kipindi hadi baadhi ya MODERATORS wakawa wanafuta nyuzi zangu za majibu kwa maksudi kwasababu ambazo wanazifahamu wao (Jambo ambalo lilinishangaza mno).

Kiufupi kadiri muda unavyokwenda nadhani UKWELI kuhusu siasa za dunia watanzania wameanza kuufahamu vizuri. Kinachoendela kule URUSI na hasahasa kule GAZA vimebadilisha fikra siyo tu za watanzania bali mabilioni ya watu dunia wengi hapa duniani wakiwemo WAYAHUDI WA DIASPORA, wanaanza kuuona ukweli wa dunia jinsi ulivyo.

Binafsi nasema UKWELI na MUDA ndivyo vimewashinda watu na siyo hoja zangu. Maana mimi hata nisemaje, kama UKWELI na MUDA havitakuwa upande wangu basi ntaonekana kuwa ni mwongo. Lakini kama kutokea mwaka 2018, kila nilichokiandika kimethibitishwa na kinachoendelea hapa duniani, binafsi naishia kusema haya maneno:

WHAT A GOOD TIME TO BE ALIVE........!!!!!
 
Soviet haikuwahi kusambaratika kilichofanyika ni kiini macho tu, States zote zilikuwa zinareport Kremlin.
 
Mbona umoja wa Kisovieti (USSR) ulimalizwa bila kuleta madhara kwenye usalama wa dunia ???
Au hapa unamaanisha kumalizwa kivipi labda ???
Hata leo Russia anaweza akapakatwa na dunia ikabaki kuwa salama kabisa.
 
Usumbufu unaoletwa na Urusi ni sawa na ule wa kunguni au chawa tu kwa binadamu. Sababu za usumbufu huo ni tatu:

1. Urusi tofauti na USSR imegeuka kuwa "rogue state" isiyo na lengo kuu la kimfumo (strategic objective) zaidi ya kuwepo tu (mere survival/existence). USSR ilikuwa na lengo la kuigeuza dunia nzima kuwa ya kikomunisti kwa misingi la Marx/Lenin. Hiyo ilishindikana, USSR ikasambaratika na kupoteza ushawishi huo duniani kote. Leo hii Urusi inaongozwa na kikundi maslahi kilichokumbatia madaraka na kugawana fursa za kibepari kwa kubebana (cronyism & patronage). Ukomunisti ulishatupiliwa mbali; sasa ni ma-oligarchs tu yanayojuana na Kremlin. Kikundi hiki kinajua kabisa kuwa maslahi yake yanategemea Marekani na Ulaya. Huko ndiko kwenye uhakika wa uchumi wake. Leo hii nenda Central London utakuta wamiliki wakubwa wa ardhi na mali ni kutoka Urusi/Ukraine. Wamewekeza kweli huko Marekani na Ulaya. Hivyo kila wakati wanahangaika kuhakikisha watu rafiki (sympathetic) (Trump & co.) wanakuwa madarakani.

2. Muhimu sana hawa wahuni (akina Putin) wamerithi rasilimali nzito za kiteknologia ikiwa ni pamoja na za nyuklia, ardhi, maliasili na mifumo ya elimu ya hali ya juu toka USSR. Na hapo wanajitahidi sana kutoa upendeleo kwa watu wao wenye kuweza kuziendeleza rasilimali hizo ili wazitumia kupambana na Marekani na Ulaya. Kule kuwepo kwa miundombinu ya uhakika ya nyuklia na sayansi za anga ni kinga/tishio (deterrence) tosha kwa yeyote atakayefikiria kupambana na Urusi. Tena wakiwa "rogue state" hawajali hata kutoa mhanga idadi kubwa ya watu wao kwa maslahi ya kikundi tawala kilichopo Kremlin. Tofauti na Marekani na Ulaya ambao watu wao wana thamani kubwa sana, wanaojali maisha bora kwa kila mtu na kuna mifumo thabiti ya kusimamia haki za binadamu. Marekani wakijua wanapambana na "wehu" si rahisi kuwavamia Warusi huko Crimea, Syria na kwingineko bila kujihakikishia kutozuka vita ya nyuklia!

3. Marekani na Ulaya ni jamii zilizo wazi (open societies). Mambo yao ni hadharani. Marais wao wakifanya faulo wanapashwa hadharani. Wanachunguzwa hadharani (Robert Mueller on Russian collusion). Wateule wa Rais wanapigwa interview hadharani. n.k. Kwa urusi, hiyo ni sawa na kuanika nguo zao za ndani hadharani. Rais wao (Putin) ni sawa na mungu! Athari zake ni kuwa watu hatari wanapata mianya kibao ya kuendesha uhalifu Marekani na Ulaya. Warusi wanatumia fursa hiyo kujaribu kuhujumu nchi za jumuia ya NATO. Marekani na Ulaya wanalijua hilo lakini hawako tayari kujifungia ndani kama Urusi. badala yake wanajiimarisha kitaaluma kukabiliana na chokochoko za Urusi na wahuni wengine. Na kwa kweli wamefanikiwa. Karibu harakati zote za Warusi wanazijua. Kuna wakati wanajifanya hawana uhakika ili kuwaingiza kwenye mitego.

Akina Putin wanajua vizuri sana kwamba hawaiwezi Marekani na washirika wake wa Ulaya. Kwanza, huko ndiko wanakohifadhia utajiri wao wa kifisadi. Ndiko wanakosomeshea watoto wao na ndiko ambapo kila Mrusi aliyefanikiwa anaotea kuwa na makazi na kumiliki mali kama ilivyo kwa watu wengine wa dunia ya tatu. Kitu nachoamini ni kuwa Urusi wangekuwa na viongozi wenye maono ya hali ya juu, kwa uwezo na rasilimali walizo nazo, wangekuwa tishio sana kwa washirika wa NATO. Bahati mbaya, wanaongozwa na watu wenye tamaa ya mali, madaraka na sifa (ujiko) bila falsafa kuu ya taifa. Watu ambao wanategemea kubebwa na miundombinu iliyowekwa na USSR ambayo sujui kama wataweza kuiimarisha ishindane na ya magharibi huko mbeleni.
Maneno yako ni ukweli mtupu.
 
Sawa kabisa,

Lakini kuhusu hiyo sera ya Revanchism nadhani iko kwa kila taifa kubwa hapa duniani (Inherent to any Global and Regional Power) sema kwasababu wengi huwa hamuipendi Urusi kwasababu ambazo mnazifahamu wenyewe na hata kushindwa kukubali kwamba kinachofanywa na Urusi hufanywa na mataifa yote makubwa duniani, tena huenda vibaya zaidi kupita Urusi.

Hicho unachokiita Revanchism, kikawaida ni Imperialism tu sema tumeamua kutumia neno jingine. Haya hebu zingatia haya yafuatayo:
  • Kule Urusi inaitwa Revanchism ambapo kweli Urusi anavunja sheria za kimataifa na kuvamia mataifa halali kijeshi na kujimegea vipande vya nchi, akisingizia analinda usalama wake. Hili ni kweli kabisa, kila taifa linatakiwa liheshimu Political Independence, Territorial Integrity and Sovereignty of other nations.

  • Kule Israeli wanaiita The Right to Return (Aliya) ambayo inasindikizwa na Genocide kabisa. Tena hiki wengi humu ndani mmekuwa mkikishabikia kwa nguvu kweli kwasababu za kidini na kisiasa. Wazungu wa Ulaya waliotokea Urusi, Poland na Ukraine wanaamini kabisa wana haki ya kuishi kwenye eneo linaloitwa Palestina kuliko jamii za Kiyahudi na kiarabu ambazo zimeishi pale kwa miaka zaidi ya 2000. Hili ni hatari kuliko hata anachokifanya Urusi. Kituko ni ule mfano anaoutoa mwanahistoria wa Israel Illan Pape kwamba "Most Zionists don't believe in God, yet they believe that he has given them land in the Middle-East". Kituko kingine ni hiki, Hii Revanchism ya Isreli inaungwa mkono na mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa ambayo hayaungi mkono Revanchism ya Urusi kule Ulaya Mashariki. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)

  • Kule Marekani wanaiita Manifest Destiny/The Munroe Doctrine na wote tunajua nini kinazikuta nchi za Western Hermisphere pindi wanaenda kinyume na Marekani. Haijapita hata miaka 50, tangu serikali ya Ronald Reagan ifanye ambacho Vladmir Putin anakifanya leo kule Ulaya Mashariki. Mwaka 1983 alivamia Grenada na kumtoa Waziri Mkuu halali wa nchi Maurice Bishop na kuweka kibaraka. Ila zaidi ya hapo, Marekani alituma magaidi kuvamia Nicaragua hadi kupelekea The Contra-Affair. Yote hayo viongozi waandamizi wa Marekani kama William Casey walisema ni kwa ajili ya kulinda maslahi na usalama wa Marekani unaihatarishwa na nchi jirani. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)

  • Kule Uingereza wameipa jina zuri The Commonwealth of Nations ila malengo ni yaleyale, Restoration of the Influence of the British Empire through the backdoor. Ndiyo maana kipindi cha harakati za kupigania uhuru wa Northern Ireland almaarufu kama The Troubles, Uingereza inayojiita nchi ya kidemokrasia ilifanya mauaji ya kutisha ili Northern Ireland isijitoe kwenye The Commonwealth of Nations. Sababu hiihii ya kuamini katika Old Glory ndiyo inazuia harakati za Scotland kujipatia uhuru, na hata nchi kama Australia kuwa huru zenyewe bila kukutwa na mkono wa chuma wa mabwanyenye ya Downing Street. Gough Whitlam waziri mkuu wa Australia alipinduliwa kimabavu na MI6 na CIA pale alipotaka kuiondoa Australia kwenye kambi ya mabeberu na kuifanya isifungamane na upande wowote. (Hili la kumtoa Whitlam kibabe halina utofauti na lile Urusi walimfanyia Raisi Viktor Yushenko wa Ukraine)
Mifano iko mingi sana hapa duniani, endapo tutachambua bila kuweka mizania ya upendeleo. Kule Ufaransa wanatumia Francophones System na CFA Franc kutawala nchi za Afrika, ambazo zimelazimishwa zisiwe na Central Bank, na akiba yao yote ya fedha za kigeni iko mikononi mwa Ufaransa ambaye ni lazima wambombe ili watumie. Hata Uturuki naye anafanya hivyohivyo kule Cyprus, Greece, Azerbaijan-Armenia, Serbia na Albania, kwa kutumia waislamu wenye asili ya kituruki kuvuruga amani na kueneza ushawishi wake.

MWISHO KABISA: Ambacho Urusi anakifanya kule Ulaya Mashariki ni kinyume na sheria za kimataifa. It's simply Illegal, defies common precepts of decency and I don't condone it. Japo ukweli ni kwamba hakuna taifa kubwa duniani ambalo halifanyi ambacho kile Urusi wanakifanya kulinda maslahi yao aidha ya kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni hata kwa mbinu ambazo ziko kinyume na utaratibu wa sheria za kimataifa ambazo zina mzizi kwenye mkataba wa Westphalia (Treaty of Westphalia) wa mwaka 1648, uliomaliza vita mbaya ya kidini iliyopiganwa miaka 30 baina ya Waprotestanti na Wakatoliki ambao walikuwa wanavutana juu ya mambo hayahaya unayoyasema hapa (Catholic Revanchism and Imperialism).

Mkataba unasisitiza katika kuheshimu, State Sovereignty, Political Independence and Territorial Integrity hata pale ambapo taifa kubwa halikubaliani na falsafa za kisiasa na kidini za taifa dogo.

ENIWEI kwasababu tumeshaamua kuamini kwamba RUSSIA IS A BAD GUY with no legitimate security concerns and interests, na kila kinachofanywa na Wamarekani, Waingereza, Wafaransa na Wayahudi ni sahihi kwasababu ni GOOD-GUYS, basi sidhani kama hata tukifanya mjadala wa miaka 10,000 naweza kukubadilisha

=====================================================
Ila uhalisia, ni ule ambao Professor John Mearsheimer amekuwa akiusema siku zote kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Kwamba hakuna taifa kubwa takatifu, kwamba liwe na mabavu halafu lisijaribiwe kutumia hayo mabavu kujipatia kila linachokitaka, aidha kijeshi au kwa namna yoyote ile.

Haya Mkuu uwe na siku njema, I rest my case!
Duh!Barikiwa sana mkuu.
 
Ndugu yangu nakushukuru sana kwa haya masifa.

Japo nadhani ulichokisema hapa, kitaamsha watu wengi maruani ya watu wengi mno ambao hupenda kubishana na mimi siyo kwa kujifunza bali kwa kutaka tu kubishana kwasababu wamebishana, na sababu nyingine wazijuazo wenyewe.

Siku zote huwa nasema kwamba muda ni mwalimu mzuri mno. Huu uzi niliuandika mwaka 2018, mwaka 2022 vita vya Ukraine inapoanza watu walinivamia sana wakinitafuta na kusema mimi napiga propaganda na nilidanganya ummah. Walisema kwamba Urusi inashindwa vita na ingeenda kuanguka kiuchumi na kupasuka vipande.

Nilikuwa natumiwa mamia ya NOTIFICATIONS za MENTION nyingi zikiwa zimejaa matusi, kejeli na kebhehi, lakini sikuweza kuwajibu sana na niliishia kucheka tu, nikifahamu fika kwamba hata ashuke malaika nisingeweza kuwashawishi chochote. Ikafika hata kipindi hadi baadhi ya MODERATORS wakawa wanafuta nyuzi zangu za majibu kwa maksudi kwasababu ambazo wanazifahamu wao (Jambo ambalo lilinishangaza mno).

Kiufupi kadiri muda unavyokwenda nadhani UKWELI kuhusu siasa za dunia watanzania wameanza kuufahamu vizuri. Kinachoendela kule URUSI na hasahasa kule GAZA vimebadilisha fikra siyo tu za watanzania bali mabilioni ya watu dunia wengi hapa duniani wakiwemo WAYAHUDI WA DIASPORA, wanaanza kuuona ukweli wa dunia jinsi ulivyo.

Binafsi nasema UKWELI na MUDA ndivyo vimewashinda watu na siyo hoja zangu. Maana mimi hata nisemaje, kama UKWELI na MUDA havitakuwa upande wangu basi ntaonekana kuwa ni mwongo. Lakini kama kutokea mwaka 2018, kila nilichokiandika kimethibitishwa na kinachoendelea hapa duniani, binafsi naishia kusema haya maneno:

WHAT A GOOD TIME TO BE ALIVE........!!!!!
Mkuu mimi nisema tu kuwa upo vizuri sana.
 
Nchi kama Russia ktk elimu yao wameangalia nini wanahitaji kama taifa na waka-design curriculum yao mahsusi kulenga hicho na ndio maana wana bajeti kubwa sana inayotengwa kwa ajili ya Research kwani pasipo Research hakuna Innovation.

Russia wana kila sababu ya kuendelea na watazidi tu kuendelea kwani wanawekeza ktk maendeleo na wana sera thabiti zinazolenga ktk dhana nzima ya maendeleo. Sisi ngoja tuendelee kuwawinda wale wapinzani wanaokataa sera yetu ya kuunga juhudi.

Ulichokisema hapa juu 👆🏽👆🏽👆🏽 kinatofautiana kabisa na unachokisema hapa chini 👇🏽👇🏽👇🏽
Au wewe unaona kauli zako hazipishani mkongwe!?

IMG_1272.jpeg
 
Sawa kabisa,

Lakini kuhusu hiyo sera ya Revanchism nadhani iko kwa kila taifa kubwa hapa duniani (Inherent to any Global and Regional Power) sema kwasababu wengi huwa hamuipendi Urusi kwasababu ambazo mnazifahamu wenyewe na hata kushindwa kukubali kwamba kinachofanywa na Urusi hufanywa na mataifa yote makubwa duniani, tena huenda vibaya zaidi kupita Urusi.

Hicho unachokiita Revanchism, kikawaida ni Imperialism tu sema tumeamua kutumia neno jingine. Haya hebu zingatia haya yafuatayo:
  • Kule Urusi inaitwa Revanchism ambapo kweli Urusi anavunja sheria za kimataifa na kuvamia mataifa halali kijeshi na kujimegea vipande vya nchi, akisingizia analinda usalama wake. Kuhusu Russian Revanchism hili ni kweli kabisa, kila taifa linatakiwa liheshimu Political Independence, Territorial Integrity and Sovereignty of other nations.

  • Kule Israeli wanaiita The Right to Return (Aliya) ambayo inasindikizwa na Genocide kabisa. Tena hiki wengi humu ndani mmekuwa mkikishabikia kwa nguvu kweli kwasababu za kidini na kisiasa. Wazungu wa Ulaya waliotokea Urusi, Poland na Ukraine wanaamini kabisa wana haki ya kuishi kwenye eneo linaloitwa Palestina kuliko jamii za Kiyahudi na kiarabu ambazo zimeishi pale kwa miaka zaidi ya 2000. Hili ni hatari kuliko hata anachokifanya Urusi. Kituko ni ule mfano anaoutoa mwanahistoria wa Israel Illan Pappe kwamba "Most Zionists don't believe in God, yet they believe that he has given them land in the Middle-East". Kituko kingine ni hiki, Hii Revanchism ya Israeli inaungwa mkono na mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa ambayo hayaungi mkono Revanchism ya Urusi kule Ulaya Mashariki. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)

  • Kule Marekani wanaiita Manifest Destiny/The Munroe Doctrine na wote tunajua nini kinazikuta nchi za Western Hermisphere pindi wanaenda kinyume na Marekani. Haijapita hata miaka 50, tangu serikali ya Ronald Reagan ifanye ambacho Vladmir Putin anakifanya leo kule Ulaya Mashariki. Mwaka 1983 alivamia Grenada na kumtoa Waziri Mkuu halali wa nchi Maurice Bishop na kuweka kibaraka wao. Ila zaidi ya hapo, Marekani alituma magaidi kuvamia Nicaragua hadi kupelekea The Contra-Affair. Yote hayo viongozi waandamizi wa Marekani kama William Casey walisema ni kwa ajili ya kulinda maslahi na usalama wa Marekani unaohatarishwa na nchi jirani. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)

  • Kule Uingereza wameipa jina zuri The Commonwealth of Nations ila malengo ni yaleyale, Restoration of the Influence of the British Empire through the backdoor. Ndiyo maana kipindi cha harakati za kupigania uhuru wa Northern Ireland almaarufu kama The Troubles, Uingereza inayojiita nchi ya kidemokrasia ilifanya mauaji ya kutisha ili Northern Ireland isijitoe kwenye The Commonwealth of Nations. Sababu hiihii ya kuamini katika Old Glory ndiyo inazuia harakati za Scotland na Australi kujipatia uhuru wao zenyewe bila kukutwa na mkono wa chuma wa mabwanyenye ya Downing Street. Gough Whitlam waziri mkuu wa Australia alipinduliwa kimabavu na MI6 na CIA pale alipotaka kuiondoa Australia kwenye kambi ya mabeberu na kuifanya isifungamane na upande wowote kwenye Vita Baridi. (Hili la kumtoa Whitlam kibabe halina utofauti na lile Urusi walimfanyia Raisi Viktor Yushenko wa Ukraine)
Mifano iko mingi sana hapa duniani, endapo tutachambua bila kuweka mizania ya upendeleo. Kule Ufaransa wanatumia Francophones System na CFA Franc kutawala nchi za Afrika, ambazo zimelazimishwa zisiwe na Central Bank, na akiba yao yote ya fedha za kigeni iko mikononi mwa Ufaransa ambaye ni lazima wamwombe ruhusu ili watumie akiba yao. Hata Uturuki naye anafanya hivyohivyo kule Cyprus, Greece, Azerbaijan-Armenia, Serbia na Albania, kwa kutumia waislamu wenye asili ya kituruki kuvuruga amani na kueneza ushawishi wake.

MWISHO KABISA: Ambacho Urusi anakifanya kule Ulaya Mashariki ni kinyume na sheria za kimataifa. It's simply Illegal, defies common precepts of decency and I don't condone it. Japo ukweli ni kwamba hakuna taifa kubwa duniani ambalo halifanyi ambacho kile Urusi wanakifanya kulinda maslahi yao aidha ya kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni hata kwa mbinu ambazo ziko kinyume na utaratibu wa sheria za kimataifa ambazo zina mzizi kwenye mkataba wa Westphalia (Treaty of Westphalia) wa mwaka 1648, uliomaliza vita mbaya ya kidini iliyopiganwa miaka 30 baina ya Waprotestanti na Wakatoliki ambao walikuwa wanavutana juu ya mambo hayahaya unayoyasema hapa (Catholic Revanchism and Imperialism).

Mkataba unasisitiza katika kuheshimu, State Sovereignty, Political Independence and Territorial Integrity hata pale ambapo taifa kubwa halikubaliani na falsafa za kisiasa na kidini za taifa dogo.

ENIWEI kwasababu tumeshaamua kuamini kwamba RUSSIA IS A BAD GUY with no legitimate security concerns and interests, na kila kinachofanywa na Wamarekani, Waingereza, Wafaransa na Wayahudi ni sahihi kwasababu ni GOOD-GUYS, basi sidhani kama hata tukifanya mjadala wa miaka 10,000 naweza kukubadilisha.

=====================================================
Ila uhalisia, ni ule ambao Professor John Mearsheimer amekuwa akiusema siku zote kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Kwamba hakuna taifa kubwa takatifu (Benign Hegemony), kwamba liwe na mabavu halafu lisijaribiwe kutumia hayo mabavu kujipatia kila linachokitaka, aidha kijeshi au kwa namna yoyote ile.

Haya Mkuu uwe na siku njema, I rest my case!
Darasa tosha mkuu, 💪

Mungu akubariki na akupe maisha Marefu mkuu, tunakuhitaji sana kwenye hili jukwaa tupate madini.
 
Ulichokisema hapa juu 👆🏽👆🏽👆🏽 kinatofautiana kabisa na unachokisema hapa chini 👇🏽👇🏽👇🏽
Au wewe unaona kauli zako hazipishani mkongwe!?

View attachment 3023275
Ni ukweli kwamba hatua ya kimaendeleo iliyokwisha fanyika nchini Russia ukilinganisha na kiwango cha elimu waliyonayo na raslimali walizonazo haziendani kabisa.

Katika nchi tano zenye wasomi wengi duniani Russia ni moja wao na Russia ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na raslimali lukuki lakini bado ukienda ktk vijiji vyao huko ndani ndani bado unakuta wanahangaika kupata maji safi na salama ya uhakika na unakuta bado kuna kaya zingine zenye vyoo vya shimo (Pit Latrines) kama Afrika...!!!
 
Umoja wa Kisovieti (USSR au CCCP) taifa lililozaliwa mwaka 1922-1991, lilikuwa ni moja ya taifa lenye nguvu sana duniani lakini lenye mwisho mbaya sana ambao ni aibu kwa watu wake mpaka leo.

Kiuchumi walikuwa wana nguvu sana, kiteknolojia walikuwa mbele, nguvu kubwa ya viwanda, kijeshi walikuwa mbele na mifumo yao ya kitamaduni iliyotokana na ukomunisti ilishawishi dunia kuanzia barani Marekani, Asia hadi Afrika na kubwa ziadi walikuwa na idadi kubwa sana ya watu ambapo takwimu zinasema kwamba walikuwa ni milioni 293.

Lakini baada ya kusambaratika nchi hii ilipoteza kila kitu ambacho ilikuwa nacho kuanzia Idadi ya watu, jeshi, viwanda na teknolojia maana kila nchi iliondoka na watu wake, majeshi yake na sehemu kama Ukraine ikapata viwanda vya bure kabisa, Poland na Georgia nao hawakuwa nyuma kabisa. Ikawa nchi dhaifu na masikini kweli.

Sasa najiuliza kwanini taifa hili dhaifu ambalo lililoshindwa vita baridi linaendelea kumsumbua Marekani (The Only Super Power) pamoja na washirika wake kijeshi ambao ni zaidi ya 25?

CC: chige , FisadiKuu
Hakuna anayesumbuliwa na Russia wewe sijui upo dunia gani, juzi Russia ameenda kuomba msaada wa kuunga na North Korea kuunganisha nguvu ya pamoja mana US peke yake haiwezi na hata North Korea haikutosha kaenda tena Vietnum ni russia anatapa tapa alijinata yeye ni superpower Ukrean tu imemtoa mavi sasa mwaka 3
 
Back
Top Bottom