Sawa kabisa,
Lakini kuhusu hiyo sera ya Revanchism nadhani iko kwa kila taifa kubwa hapa duniani (Inherent to any Global and Regional Power) sema kwasababu wengi huwa hamuipendi Urusi kwasababu ambazo mnazifahamu wenyewe na hata kushindwa kukubali kwamba kinachofanywa na Urusi hufanywa na mataifa yote makubwa duniani, tena huenda vibaya zaidi kupita Urusi.
Hicho unachokiita Revanchism, kikawaida ni Imperialism tu sema tumeamua kutumia neno jingine. Haya hebu zingatia haya yafuatayo:
Kule Urusi inaitwa Revanchism ambapo kweli Urusi anavunja sheria za kimataifa na kuvamia mataifa halali kijeshi na kujimegea vipande vya nchi, akisingizia analinda usalama wake. Kuhusu Russian Revanchism hili ni kweli kabisa, kila taifa linatakiwa liheshimu Political Independence, Territorial Integrity and Sovereignty of other nations.
Kule Israeli wanaiita The Right to Return (Aliya) ambayo inasindikizwa na Genocide kabisa. Tena hiki wengi humu ndani mmekuwa mkikishabikia kwa nguvu kweli kwasababu za kidini na kisiasa. Wazungu wa Ulaya waliotokea Urusi, Poland na Ukraine wanaamini kabisa wana haki ya kuishi kwenye eneo linaloitwa Palestina kuliko jamii za Kiyahudi na kiarabu ambazo zimeishi pale kwa miaka zaidi ya 2000. Hili ni hatari kuliko hata anachokifanya Urusi. Kituko ni ule mfano anaoutoa mwanahistoria wa Israel Illan Pappe kwamba "Most Zionists don't believe in God, yet they believe that he has given them land in the Middle-East". Kituko kingine ni hiki, Hii Revanchism ya Israeli inaungwa mkono na mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa ambayo hayaungi mkono Revanchism ya Urusi kule Ulaya Mashariki. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)
Kule Marekani wanaiita Manifest Destiny/The Munroe Doctrine na wote tunajua nini kinazikuta nchi za Western Hermisphere pindi wanaenda kinyume na Marekani. Haijapita hata miaka 50, tangu serikali ya Ronald Reagan ifanye ambacho Vladmir Putin anakifanya leo kule Ulaya Mashariki. Mwaka 1983 alivamia Grenada na kumtoa Waziri Mkuu halali wa nchi Maurice Bishop na kuweka kibaraka wao. Ila zaidi ya hapo, Marekani alituma magaidi kuvamia Nicaragua hadi kupelekea The Contra-Affair. Yote hayo viongozi waandamizi wa Marekani kama William Casey walisema ni kwa ajili ya kulinda maslahi na usalama wa Marekani unaohatarishwa na nchi jirani. (Hakuna utofauti wowote na anachofanya Urusi)
Kule Uingereza wameipa jina zuri The Commonwealth of Nations ila malengo ni yaleyale, Restoration of the Influence of the British Empire through the backdoor. Ndiyo maana kipindi cha harakati za kupigania uhuru wa Northern Ireland almaarufu kama The Troubles, Uingereza inayojiita nchi ya kidemokrasia ilifanya mauaji ya kutisha ili Northern Ireland isijitoe kwenye The Commonwealth of Nations. Sababu hiihii ya kuamini katika Old Glory ndiyo inazuia harakati za Scotland na Australia kujipatia uhuru wao zenyewe bila kukutwa na mkono wa chuma wa mabwanyenye ya Downing Street. Gough Whitlam waziri mkuu wa Australia alipinduliwa kimabavu na MI6 na CIA pale alipotaka kuiondoa Australia kwenye kambi ya mabeberu na kuifanya isifungamane na upande wowote kwenye Vita Baridi. (Hili la kumtoa Whitlam kibabe halina utofauti na lile Urusi walimfanyia Raisi Viktor Yushenko wa Ukraine)
Mifano iko mingi sana hapa duniani, endapo tutachambua bila kuweka mizania ya upendeleo. Kule Ufaransa wanatumia Francophones System na CFA Franc kutawala nchi za Afrika, ambazo zimelazimishwa zisiwe na Central Bank, na akiba yao yote ya fedha za kigeni iko mikononi mwa Ufaransa ambaye ni lazima wamwombe ruhusa ili watumie akiba yao. Hata Uturuki naye anafanya hivyohivyo kule Cyprus, Greece, Azerbaijan-Armenia, Serbia na Albania, kwa kutumia waislamu wenye asili ya kituruki kuvuruga amani na kueneza ushawishi wake.
MWISHO KABISA: Ambacho Urusi anakifanya kule Ulaya Mashariki ni kinyume na sheria za kimataifa. It's simply Illegal, defies common precepts of decency and I don't condone it. Japo ukweli ni kwamba hakuna taifa kubwa duniani ambalo halifanyi ambacho kile Urusi wanakifanya kulinda maslahi yao aidha ya kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni hata kwa mbinu ambazo ziko kinyume na utaratibu wa sheria za kimataifa ambazo zina mzizi kwenye mkataba wa Westphalia (Treaty of Westphalia) wa mwaka 1648, uliomaliza vita mbaya ya kidini iliyopiganwa miaka 30 baina ya Waprotestanti na Wakatoliki ambao walikuwa wanavutana juu ya mambo hayahaya unayoyasema hapa (Catholic Revanchism and Imperialism).
Mkataba unasisitiza katika kuheshimu, State Sovereignty, Political Independence and Territorial Integrity hata pale ambapo taifa kubwa halikubaliani na falsafa za kisiasa na kidini za taifa dogo.
ENIWEI kwasababu tumeshaamua kuamini kwamba RUSSIA IS A BAD GUY with no legitimate security concerns and interests, na kila kinachofanywa na Wamarekani, Waingereza, Wafaransa na Wayahudi ni sahihi kwasababu ni GOOD-GUYS, basi sidhani kama hata tukifanya mjadala wa miaka 10,000 naweza kukubadilisha.
=====================================================
Ila uhalisia, ni ule ambao Professor John Mearsheimer amekuwa akiusema siku zote kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Kwamba hakuna taifa kubwa takatifu (Benign Hegemony), kwamba liwe na mabavu halafu lisijaribiwe kutumia hayo mabavu kujipatia kila linachokitaka, aidha kijeshi au kwa namna yoyote ile.
Haya Mkuu uwe na siku njema, I rest my case!