Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?



Imeloa kabla ya kulogwa😂😂
 
Kweli umekataa kutumia akili.ukraine huku akisaidiwa na NATO nzima wameshindwa kuwapiga Russia Ukraine.hizo nchi Amekwenda kuimarisha mahusiano hana sababu ya kuomba silaha kwa sababu anatengeneza mara 3 ya NATO
 
Kwa ukubwa wa Russia, geographically haishangazi sana kuona baadhi ya vijiji vina changamoto mbalimbali katika maendeleo. Lakini sidhani kama ni Russia pekee wana changamoto kama hizo ulizozitaja.
Lakini pia mkongwe, Russia inaishi kwa vikwazo lukuki, hauoni kama walipo kama taifa wanastahili pongezi pamoja na vikwazo vya kiuchumi walivyonavyo?
 
Ukubwa au udogo sio sababu, Burundi/Rwanda ni mataifa madogo madogo sana lakini wenyewe pia wana changamoto hizo hizo.

Russia pamoja na kwamba waliharibiwa na akina Vladmir Lenin kwa kuwaletea mfumo wa hovyo wa kikomunisti lakini kutokutambua vipa umbele vyao kama taifa ni sababu nyingine kubwa inayosababisha iwe hapo ilipo.

Pia hiyo inasababishwa na utawala wa kiimla ambapo rais ndiye anayeamua kipa umbele kiwe nini na kwa rais wao wa sasa kipa umbele chake ni Russia yenye nguvu kijeshi tofauti na maendeleo ya kiuchumi.
 
Shukrani kwa uchambuzi wako.

Nafahamu vyema wazo kuu la uchambuzi wako kwamba mataifa makubwa huwa na sera, mikakati na matendo mbalimbali [halali na haramu kulingana na sheria za kimataifa] kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya taifa/kitaifa. Hii hoja uliyoisema hapa nimewahi kuisema pia humu jukwaani miaka kadhaa iliyopita kwa maneno tofauti kidogo.

Pitia uchambuzi huu hapa chini:

Kwa vile mada iliyoletwa jukwaani (natambua ni ya zamani kidogo) haihusu mfumo wa uhusiano wa kimataifa wa dunia yetu kwa ujumla wake unaozingatia "maslahi ya taifa/kitaifa" bali ni mahususi kwa ajili ya Urusi/USSR, nimeamua kujikita zaidi kuizungumzia Urusi ama USSR pekee na sera au matendo yake ya kihistoria ambayo yamepelekea athari au mabadiliko makubwa katika siasa za jiografia na uhusiano wa kimataifa.

Mambo mengi uliyosema ikiwemo mifano uliyoambatanisha na hoja yako kuu (maslahi ya taifa/kitaifa) ni masuala ambayo yanahitaji mijadala mipya kabisa (separate) na tunaweza tusikubaliane katika baadhi ya masuala hayo uliyoyasema.

Lakini, kwa kiasi kikubwa nakubaliana na wewe kwenye msingi mkuu wa hoja yako kwamba mataifa makubwa, yenye ushawishi mkubwa katika masuala ya kijeshi, kisiasa na kiuchumi yamekuwa na sera, tabia au mienendo fulani ndani na nje ya mipaka yao kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya taifa/kitaifa ambayo wakati mwingine ni kinyume na maslahi ya wengine ama sheria za kimataifa.

Kimsingi, dunia imekuwa ikiendeshwa kwa nguvu na ushawishi wa kitu kinachofahamika kama "maslahi binafsi" ili kujihakikishia survival. Hilo lipo tangu zamani [karne nyingi zilizopita] na hata ukisoma vitabu vya dini zinazoaminika hivi sana duniani, utakutana na matendo kama haya yaliyopo hivi sasa kwa jina lilelile la kulinda maslahi ya taifa ama jamii ya watu fulani walioishi zama za kale.

Nadhani hata John Mearsheimer analifahamu hilo vyema ingawa amekuwa akikosolewa vikali na wasomi wenzake wa masuala ya siasa za kimataifa kutokana na baadhi ya misimamo yake na vilevile kwa kutokuwa consistent kwenye masuala kadhaa mahususi yahusuyo geopolitics hususani za Mashariki ya Kati na issue ya Ukraine na Urusi.

Kwa kusema hayo, nafikiri mada kuu iliyowasilishwa jukwaani imepatiwa jibu/jawabu. Shukrani!
 
It seems time has vindicated me.​
 
Wasichokijua Wengi Kuwa Urusi ni taifa tajiri kinishati na kiteknologia..

Bila gesi ya Urusi chi nyingi za Ulaya watu watakufa kwa baridi, mfano Italia inategemea Gesi ya Urusi kwa asilimia 80%
Muda ni mwalimu mzuri sana.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…