Swali hili hii ni kwa wasomi wa na wabobezi wa dini ya Kikristo na sio washabiki

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Umhimu wa Kujua Historia

Mtume Muhammad ﷺ alisema: "Mtu ambaye hana historia, hana maisha" (Abu Dawood).
  • Hii hadithi inasisitiza umuhimu wa kujua na kuelewa historia ili kuwa na mtazamo kamili wa maisha na maendeleo ya kijamii.
Hapa kuna orodha ya manabii waliotajwa katika Agano la Kale na Qur'an, pamoja na maeneo ambapo walizaliwa
Manabii Katika Agano la Kale:
  1. Nabii Ibrahim (Abraham)
    • Nchi: Mesopotamia (sasa Iraq)
    • Mahali pa Kuzaliwa: Uru, Mesopotamia
  2. Nabii Musa (Moses)
    • Nchi: Misri
    • Mahali pa Kuzaliwa: Misri (katika eneo la mji wa Gosheni)
  3. Nabii Daudi (David)
    • Nchi: Palestina
    • Mahali pa Kuzaliwa: Bethlehemu, Israeli
  4. Nabii Sulemani (Solomon)
    • Nchi: Palestina
  5. Nabii Isaya (Isaiah)
    • Nchi: Palestina
  6. Nabii Yeremia (Jeremiah)
    • Nchi: (inayokaliwa na, Israeli)
  7. Nabii Ezekieli (Ezekiel)
    • Nchi Palestina(inayokaliwa na, Israeli)

Manabii Katika Qur'an:

  1. Nabii Ibrahim (Abraham)
    • Nchi: Mesopotamia (sasa Iraq) na Kanaani (sasa sehemu ya Israeli na Palestina)
    • Mahali pa Kuzaliwa: Uru, Mesopotamia
  2. Nabii Musa (Moses)
    • Nchi: Misri
    • Mahali pa Kuzaliwa: Misri (katika eneo la mji wa Gosheni)
  3. Nabii Daudi (David)
    • Nchi: Palestina
  4. Nabii Sulemani (Solomon)
    • Nchi: Palestina
    • Mahali pa Kuzaliwa: Palestina
  5. Nabii Isa (Jesus)
    • Nchi: Palestina
    • Mahali pa Kuzaliwa: Palestina
  6. Nabii Muhammad ﷺ
    • Nchi: Arabia (sasa Saudi Arabia)
    • Mahali pa Kuzaliwa: Makka, Saudi Arabia
  7. Nabii Yunus (Jonah)
    • Nchi: Ninawi (sasa Iraq)
    • Mahali pa Kuzaliwa: Ninawi, Iraq
  8. Nabii Hud (Heber)
    • Nchi: Arabia (sasa sehemu ya Saudi Arabia)
    • Mahali pa Kuzaliwa: Aadil, Saudi Arabia
  9. Nabii Salih (Methuselah)
    • Nchi: Thamud (sasa sehemu ya Saudi Arabia)
    • Mahali pa Kuzaliwa: Thamud, Saudi Arabia
Katika waislam misikiti mikuu 3
Msikiti wa Al-Haram (Masjid al-Haram)- Mahali: Makkah, Saudi Arabia
Msikiti wa Al-Masjid an-Nabawi (Masjid al-Nabawi)- Mahali: Madinah, Saudi Arabia
Msikiti wa Al-Aqsa (Masjid al-Aqsa)-Mahali: Yerusalemu, Palestina

WAKIRISTO MAKANISA MAKUU
Kanisa la Mtakatifu Petro (St. Peter's Basilica) -Mahali: Vatican City, Roma, Italia
Kanisa la Mitume watatu (Trinity Church)- Mahali: Boston, Massachusetts, Marekani
Kanisa la Hagia Sophia (Aya Sofya)- Mahali: Istanbul, Uturuki
Kanisa la Westminster (Westminster Abbey)- Mahali: London, Uingereza
Kanisa la Martin Luther (Lutherkirche)-Mahali: Wittenberg, Ujerumani

KWANINI MAKANISA MAKU YAPO ULAYA? NA SIO MASHARIKI YA KATI?
 
Unahitaji kujifunza mengi zaidi ya elimu ya madrasa.

Kwanza katika dini za Ukristo na Uyahudi Ibrahim, Daud na Suleiman na wengine wengi uliowataja hapo hawakuwa manabii.

Pili, Ukristo unaanza na Yesu Kristo katika agano jipya, hao wengine wote uliowataja ungewauliza Waisraeli wa dini ya Uyahudi wanaobondona na Hamas huko Gaza wakati huu.
 
YESU HANA DINI YEYE NI BABA WA WOTE WAFANYAO AMRI YAKE KUU AMBAYO NI UPENDO.

TUKIISHI KWA KUPENDANA KWA DHATI HATUTAULIZANA MASWALA YA DINI BALI TUTAKUWA TUMEITIMILIZA AMRI KUU "UPENDO"

UPENDO HUSITIRI, UPENDO HUSAMEHE, UPENDO HUSAIDIA
 
Sintojibu maswali yako hadi uandike kwa usahihi.Ni Palestina au Israeli?🤣🤣🤣🤣🙏
 
Ukristo ulizaliwa mashariki yakati ukaenezwa na wazungu,kumbuka kipindi hicho Roman Empire ilikuwa inatawala dunia,hata nashariki ya kati ilikuwa chini ya Roman Empire.
Ni kama Tanganyika ilivyokuwa koloni la waingereza na leo tunaongea kiingereza,mitume hasa Paul alifanya kazi kubwa kueneza ukristo,kipindi hicho dini ya ukristo ilifunganamishwa na serikali ya kirumi

Yesu hakuwa mkristo,alizaliwa jatika familia ya Jews

Dini ya kikristo ilianza baadae baada ya Yesu kufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…