Ile sio pension Wala ajira ni kazi ya mkataba na mifuko ya pension haihusiki nayo
Mifuko ya pension inashusika na waajiriwa tu wa Sekta binafsi na serikali sio wabunge au watupu waliojiajiri wenyewe
Tatizo hiyo formula binafsi Kwa faida ya mstaafu akichukua asilimia 100 nakuhakikishia baada ya miaka miwili utamkuta kachakaa kama mbwa wa porini
Watu waliochukua mkupuo miaka ya nyuma wako na maisha magumu wengi hatari Tatizo wengi hawaombi huko mitaani Kwa wastaafu wawape maoni Yao
Lakini Mimi ushauri wangu pension ya mwezi iwe kubwa mtu hata kama nyumba Hana aweza panga nyumba Mzuri bila kujenga na akaishi vizuri
Kosa kubwa la kwanza linafanywa na wastaafu wengi kuchukua pension na kwenda kujenga nyumba na Kununua gari .Hela ya mkupuo inakatikia hapo.Ikikata ya mwezi ndio unatakiwa imbebe kuendesha gharama za gari na nyumba umeme,maji na yeye kula nk hapo sasa ndipo Unakuta kibibi au kibabu kinaanza kelele ohh pension ya mwezi mdogo watu timetumikia nchi Kwa uaminifu ona kipension Cha mwezi ninacholipwa na kuanza kusumbua watoto na ndugu na jamaa kulia Lia njaa
Hayo mambo ni very serious mtu mbishi atakiona Cha mtema Kuni akistaafu pesa ya mkupuo ikikata ya mwezi ikiwa ndogo lazima atungue kilio
Tunaongea humu ku saidia wazee
Mzee mstaafu sio mtu mzima ni Mzee mzima kwenye utu uzima alishapita ndio maana anastasfishwa kuwa wewe utu uzima ulishapita wewe ni Mzee mzima kikongwe ondoka nenda hivyo kakipato ka Kila mwezi kanatakiwa kawe kakubwa akichukua asilimia 100 pension hailipi Tena pension ya mwezi ni mauaji ya kimbari Kwa wazee .Kazee kaweza anzisha tuniashara twake Koko Kwa umri wa uzee maradhi mengi na tubiashara tunahitaji usimamizi makini kakiumwa tu na kulazwa kakitoka biashara imeenda na maji Vijana wamefanya Yao kanakufa na pressure mapema lakini kama kale ka mwezi ka pension kako kakubwa kanaendelea kusukuma siku zake
Binafsi hiyo asilimia 40 sijaridhika wameweka asilimia 10 au 20 ili pension ya Kila mwezi iwe kubwa