Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,943
Kuna kipindi fulani nilikuwa nafanya kazi kwenye chombo kimoja cha habari, ilikuwa usiku naendesha kipindi cha mahusiano ghafla sms ikaingia kwenye simu ya studio ikitaka niwasiliane nae kupitia namba yangu.
Basi baada ya kipindi nikachukua namba ya yule dada na kumtext, tulichat na baadae nikaomba nimpigie nisikie Sauti yake. Mashalah mtoto alikuwa na sauti kama kinanda cha Parokia ya Mt. Martha jimbo kuu la Mbezi.
Nikamwambia rafiki yangu ambae tulikuwa tunakaa nae eneo moja (kila mtu alikuwa na chumba chake) jamaa akaniambia wasikilizaji wengi wa radio hasa wadada huwa sio wazuri akatoa mfano na kusema hivi dada mzuri atakuwa na muda wa kusikiliza radio kweli? Nikabisha sana na kumwambia nitamwambia aje ili nionane nae, jamaa akasema yeye ni mzoefu sana wa media anajua wasikilizaji walivyo.
Basi siku moja mchana jamaa akawa anaenda kazini nikaona huu ndio muda wa kumwita yule manzi kama atakuwa hayuko sawa basi nitakuwa nimeshuhudia mwenyewe, Nikampigia simu na kumtaka achukue pikipiki imlete sehemu nayokaa na kweli dada akaniambia yuko safarini anakuja.
Msela nikavaa pamba za kuvutia kumsubiri dada wa watu aje mwenye sauti ya kumtoa mtu pangoni, Baada ya nusu saa pikipiki moja nikaiona kwa mbaliiii inakuja nikajua mzigo huo unakuja (Awali aliniambia ni mwembamba na mwenye macho mazuri) Napenda sana wadada wa wembamba.
Basi pikipiki ilipofika pale ikasimama na nikaonana uso kwa uso na mgeni wangu! Aiseee hasira zikapanda alikuwa kavaa hijabu afu ni mfupi kwangu sasa tumeongozana kwenda napokaa kama mtu na mtoto wake. (Kichwani nikawa najiuliza hivi Mama Ali akiona demu niliyeingia na ndani si atanicheka wiki nzima) Mama ali ni mpangaji mwenzetu alikuwa ila alikuwa na matani sana kwani alikuwa anajua demu wangu na demu wa mshikaji wangu kwahiyo kuna muda alikuwa analinganisha wapenzi wetu.
Nilijua akiona yule dada itakuwa so endapo mshikaji wangu akirudi basi atamwambia kila kitu, Ile nafika tu nyumbani Mama Ali yupo mlangoni kwake nikapata Akili ya haraka nikaingia na yule demu ndani kwa mshikaji wangu, Sikutaka kuingia nae kwangu ili nizibe aibu ile.
Nimekaa kidogo yule demu anaanza kusifia ooh huwa nakupenda hasa kwenye kipindi chako, weeee nilimwambia nataka kwenda kazini naomba jiandae tusindikizane wakati wewe unarudi.
Nilienda Ofisini pasipokuwa na ratiba siku hiyo.
Nilikoma kuchukua namba, Mama Ali aliuza yule nani nikamwambia ni demu wa mshikaji wangu alikuja kumwona mtu wake akamkosa.