Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

😄😄😄😄😄😄😄 eti paskali hanunulik!!!!!
 
Kuendelea kushiriki hizi chaguzi ni kuwapotezea wananchi muda wao, ukweli ni kwamba ccm imesha wadharau wananchi kupita kiwango, jambo muhimu kwa chama mfu kama ccm ni kujitafakari walipo kosea, na kubaki kuiba kura na kuidanganya dunia kuwa watanzania bado wanakipenda hicho chama ni upuuzi ulio pitiliza, Bashiru na Polepole wana uwezo mdogo sana was kisiasa.
 
Mayala wewe ndo maana ulitukanwa wazi wazi na magufuri ukashangilia. Ccm inavyofanya na dola unaona ni sawa??? Acha upambaf, watu wanauawa na kuteswa sana, mbona huhoji wala kuandika chochote?


Hivi kwanini wachangia hoja wengi hatumuelewi huyu Mayala mpaka wengine wanamwita njaa? ndugu yangu kama umesoma hoja zote alizoziweka Pasco kwenye bandiko hili basi utaona kuwa maswali yako kaweka majibu mazuri tu ambayo si ya kutunga....lakini swali la msingi linabaki palepale kuwa "Tabia ya Kususa, kuzira au kugomea" nafikiri Pasco anajua jibu lake ila anataka watu nao wachangie
 
 
Watu wale wenye moyo wa dhati kupigania demokrasia na maendeleo wamekatishwa tamaa jinsi walivyo vunjwa moyo na viongozi wa vyama vya upinzani kwa sarakasi za mgombea uraisi 2015.

Wengi waliobaki ni wapiga zumari na kutetea maslahi binafsi tu. Haki wanayoililia akina Mbowe ilisombwa na mafuriko ya kutengenezwa na fedha za babu Laigwanoni ile 2015.
 
Mjumbe arrowhead kweli wewe ni kichwa Mkuki.Ulimsikiliza Mbowe vizuri? Au umejump kumuunga mkono Paschal na kumcriticise kidogo km ingekuwa Bungeni ungeuka mkono hoja.
Point ya msingi Mbowe alicodemix kwa kusema namnukuu" ku retreat sio ku surrender" Hilo peke ake linatosha na amesema wanajipanga kuongeza nguvu ya Chama kwa kutumia mbinu mbadala kwanza kwasasa.Which is merely right and logical in normal common sense really in unfairly current competitive political ground.
 
Huoni kuwa wataokoa fedha nyingi,yaani unashiriki kitu ambacho huwezi tangazwa mshindi!
 
Mkuu tabia hatuipimi kwa kauli au tendo moja. Mazoea ndiyo hujenga tabia. Tabia ya kususa kwa vyama pinzani haijaanza katika chaguzi hizi ndogo, ilokuwepo hata katika chaguzi kuu zilizopita. Hoja Hapa ni kutaka kujua éndapo njia hii ya kununa ina mashiko au ndo itakuwa kumsusia ngedere shamba la mahindi. Sipingi alichokesema Mbowe, Kweli wanahitaji njia mbadala kupambana na raisi wetu ambaye hajali wala hana muda na demokrasia
 
Sasa wapinzani awajaungana na hakuna mpinzani wa kuwaunga mkono chadema kwa hivyo ukisusa ,umesusa peke yako
Kwanza mbowe angeanza kufanya ushawishi kwa wapinzani wenzake kisha wangekuwa wote kwa pamoja kama wapinzani wangetoa tamko la pamoja
Mbowe na chadema yao ni wabinafsi sana wana umimi
hivyo kususa kwao hakuta athiri jambo lolote
Wapinzani wengine wamepata uwanja wa kujitangaza
Ukiwa mwanaume wa kweli kama bobi wine unatakiwa upambane kweli kweli upinzani sio lelemama kama mbowe anavyodhani.
 
I due respect your foolish advertisements,let your foolishness prevails out of my content!!
 
Kumbe kuna tabia za kike wao wamesusia we hujakatazwa kushiriki kama tuko 10 tunapiga 100 je kwanini ashiriki we shiriki tu wala ucjali kususa kwao huna haja ya kupayuka we sema UTASHIRIKI au wasipo shieiki na wewe ushiriki wako unapotea cjui bac sawa
 
Mkuu nakuelewa sana ila ni vigumu kukubaliana na hoja yako. Huwezi kulinganisha majukumu mazito ya tume ya uchaguzi na kazi ya majaji mahakamani kuamua mashauri hata km yanagusa kiasi gani maslahi ya nchi. uchaguzi ni mchakato wa kuamua nani anastahili kushika dola, kuongoza nchi, unaamua ni nani/chama gani imepewa ridhaa ya wananchi kuunda serikali. Ni mchakato unaoamua mustakabadhi wa nchi kisiasa, kiuchumi, kidiplomasia nk Utalinganishaje haya? Mkiti huyu na wakurugenzi wake wa tume wote ni wateule wa mgombea ambaye ni mshindani ktk uchaguzi. Tunaambiwa kila siku wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wengi ni makada wa chama tawala na ushahidi ulionyeshwa , haya hayatokei bahati mbaya. HATA KWA AKILI YA KITOTO viongoz wa tume ni watu wenye masilahi na aliyewateuwa. Na wakishapokea matokeo lazima wamweleze hali halisi km kuna anguko wtaanza kutafuta mbinu za kulifix. TETEENI MUTETEAVYO LKN INAHITAJIKI TUME HURU YA UCHAGUZI na kikubwa katiba ya Warioba inahitajika ili kuweka uwanja sawa wa kiushindani.
Pili unaposema huyo bwana ni game changer ni sawa sababu hakuna uwanja sawa na kibaya zaidi si mtu anayefuata sheria za nchi. Yeye ndiye katiba, mahakama bunge ndiye bodi ya zabuni, ndiye mamlaka ya manunuzi. Angekuwa game changer ktk misingi ya katiba ya nchi akitumia mbinu za kiushindan zilizo za haki ktk mfumo wa vyama vingi vya siasa .Mwambie arejeshe bunge mubashara na kikubwa aruhusu mikutano ya kisiasa km zamani apo ndipo utajua ni nini watanzania wanawaza. Washindani wake wote wamefungwa midomo na mikono imefungwa nyuma. Anajidai yeye pekee na chama chake. Huyo si game changer. Sifa ya kijinga.
Huyo bwana hana kasi yoyote ile, umenyamazisha wengine wote, hukosolewi huambiwi alafu mtu unasifu ana kasi. Kasi ipi? Kuuwa demokrasia, kuuwa uchumi na watu kuzidi kuwa maskini, kuteka na kutesa hii ndio kasi unayozungumzia. Uchumi umekufa, umesambaratika tunaishi ktk propaganda za kijinga
 
Bwana P nataka nikuambie kabisa km kwa sasa hutumiki basi umeamua kujitumikisha labda ukiwa na matarajio fulani, Hebu nikuulize ni nini kisaikolojia kilichokusukuma kuchagua maneno uliyotumia ktk post yako, ''tabia za kike''. Unadai huna chama, lkn ulikusudia kufikisha ujumbe gani kwa jamii dhidi ya wale unaowakosoa.
 
Wewe nadhani unatatizo la mapokeo,ndiyo mana umetumia neno eti kususa ni tabia za kike!Inamana wewe wanawake umewaweka kundi la mataahira?Acha mfumo dume,pia Acha akili za mapokeo,acha kudhalilisha mama zetu,labda kama hao wanawake uliotolea mfano ni wa ndani ya familia yako tu.Jambo la pili ambalo linaashiria wewe unatumia akili za mapokeo badala ya uyakinifu ni pale uliposema kuwa chadema wanasusa bila kutoa ufumbuzi,hii si kweli.Mbowe ameeleza kuwa wanasheria wa chama wanaendelea na hatua mbalimbali za kisheria na taratibu nyingine pia zinaendelea.Sasa wewe waliokufundisha kuongea ulichoongea mbona wamekudhalilisha?You better use your brain properly. Heri kufa na mawazo yanayoishi kuliko kuishi na mawazo yaliyokufa.Upumbavu ni ile hali ya kuujuwa ukweli,kuuona ukweli,lakini unaendelea kuamini katika uongo.
 
Jaimee unaamini njia zinazotumika na vyama pinzani zinaweza wapatia haki zao katika chaguzi zijazo ? Kwa kuzingatia matukio ya nyuma na njia chadema walizotumia kudai haki zao, unadhani njia hizo ni sahihi ? Ikiwemo kususia chaguzi, kutoka katika vipindi vya bunge, kutohudhuria kuapishwa kwa raisi n.k. njia hizi zimewapa manufaa gani ? Na unadhani zikiendelea zitawapa manufaa yapi ? Kwa mtazamo wako, ukivaa viatu vya mheshimiwa mbowe, ungeweza tumia njia gani tofauti na hizi ili kupata haki za kisiasa ?
 
Naweza nikahisi kuwa ile kamati ilipokuita ilikupa ToR za kuandika haya Maswali yako. Na nakumbuka yule Mzee aliposema Jina lako kwa Lugha ya Kisukuma linamaanisha njaa alimaanisha alichokuwa amemaanisha. Kwa platform ile na kwa swali ulilomuuliza kujibu kuwa wewe jina lako la ukoo maana yake njaa alikufahamu vizuri. Sasa ni wakati wako wa kuitibu njaa. itibu salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…