Mkuu ninaamini kuwa ukiingia vitani kwenye mapambano yasio kuwa na faida, ni busara kujitoa kwenye mapambano hayo ili usipoteze muda wako na resources zako. Haswa ikiwa ni dhahiri kuwa kwa namna yoyote utakavyopambana hutapata ushindi. Ni mpumbavu tu ambaye ataingia kwenye vita ambayo ana uhakika kuwa hawezi kushinda. Kujitoa kwenye mapambano inakupa muda wa kujijenga upya, kwa maana ya kudai fair play katika nyanja zote za mchuano, pasipo na mshiriki yoyote kubebwa na msamamizi au chombo chochote cha dola. Kudai mazingira kamili ya usawa kwa washiriki wote wa mchuano kwenye uwanja wa mapambano. Kususa kwa maana niliyoielezea huwezi kuiita ni tabia ya kitoto au ya kike. Kususa kwa maana yako mkuu kuna lenga zaidi, kugomea jambo, kwa sababu umeudhiwa, japo jambo hilo huwa mara nyingi na faida kwako, na hayo hufanywa na watoto na labda wakina dada kama ulivyoeleza. Hivi mkuu unaweza kuingia darasani na kufanya mtihani ambao dhahiri unajua kwamba hutafaulu? Si utapoteza energy yako na muda wako bure. Ni vema kutafakari kwa undani sababu za mtu kujitoa au kususia jambo fulani, kuliko kukimbilia kumhukumu.