Mkuu Retired, kwanza asante, nimeguswa na hoja ya mtu kuwa respected, hivyo kufanya mambo to the expectations of the majority hata unajua kama, that is wrong move.
Mimi nimeisha jitanabaisha humu kuwa sina chama, hivyo kazi yangu ni just as an observer na kushauri, kwenye haya ya kuhusu uchaguzi nimeisha tumia busara za aina zote na kuelimisha jinsi ya kupinga kwa, kwa busara na kwa kutumia logic na sio kutumia nguvu. Mara nyingi ninatofautiana na wengi, na kuamua kukubalina kutokubaliana, hata kwenye hili la kususa, its a political suicide kwa Chadema kama ilivyo kwa CUF.
Rais Magufuli ni dikiteta, amepiga marufuku mikutano ya siasa kidikiteta tuu, kinyume cha katiba, this is very serious issue. Chadema badala ya kudeal nayo seriously, wao wakaamua kujenga UKUTA, kuhamasisha maandamano na mikutano.
Angalia niliwashauri nini
Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe! - JamiiForums
Sasa kama watu kama hawa, walioshauriwa the right thing to do, the right path to follow, lakini hawafanyi, leo wakigoma au kususa utawaelewa?.
Chadema wanasusia kwa kuilaumu Tume, akina sisi tumewaeleza humu tatizo sio Tume bali sheria
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!. - JamiiForums
Kuhusu intellect, kwa vile intellect sio kitu constant, inaweza kupanda na kushuka, hivyo ile siku nilipouliza swali Ikulu, intellect yangu ilikuwa juu, lakini leo ninapouliza kuhusu kususa, sasa imeshuka.
Kwa vile wengi wanapingana na hoja zangu kwenye bandiko hili, na mimi pia nimelazimika kujisoma tena huku nikijiuliza, nimejiridhisha, hakuna kitu cha kubadilisha. Hivyo pia inawezekana kilichoshuka ni intellect jf members wengine, jee wewe umelisoma kwa makini hili bandiko lote?. Lina hoja ya msingi au halina hoja?.
P