Swali kuhusu uwezo wa CCM kuongoza nchi

Swali kuhusu uwezo wa CCM kuongoza nchi

dumuzi

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2007
Posts
1,050
Reaction score
868
Wakuu kuna sehemu nimekuta hili swali, na likanifikirisha sana. "Kama CCM imeshindwa kusimamia bandari ambayo hata haizidi kilometa 10 mpaka wanaamua kubinafisisha je wataweza kweli kutuongoza watanzania ambao tuko mil 60 hadi tupate maendeleo tunayostahili?"
 
Wakuu kunasehemu nimekuta hili swali, na likanifikirisha sana. "Kama ccm imeshindwa kusimamia bandari ambayo hata haizidi kilometa 10 mpaka wanaamua kubinafisisha je wataweza kweli kutuongoza watanzania ambao tuko mil 60 hadi tupate maendeleo tunayo sthili?"
Think tank wa CCM humu johnthebaptist anakuja na majibu!!
 
Somo la private na public enterprises inabidi lianze kuimbwa kila Kona ya kijiji watanzania waelwe, CCM kutoa kipaumbele Kwa private sector si kwamba umeshindwa kuongoza nchi Ila imepima kipi chenye manufaa na kuamua kwenda nacho
 
Alieuliza swali hilo ni mjinga sana!

Yeye kaona Bandari TU!!?hajaona MADINI,mbuga za wanyama n.k!!?

Kwani tangu ubinafsishaji uanze ni leo ndio kaona mikataba inaingiwa!!?
 
Mimi nandika kitabu fikirisha cha ujasiamli kitaweza kuisadia jamii maana kinajadili kwa kina mjasiriamali ambavyo anatakiwa aenende kwenye biashara na jinsi ya kukabiriana na yanayomzunguka. Kwenye ujasiriamali tunajifunza kwamba asilimia 80 ya mafaniko yanamtegemea mjasiriamali mwenyeye na hiyo asilimia nyingine ni mjasiriamali na yanayo muzunguka na hapo ndiyo patamu, samahani lakini nimekianadika kwa kimombo japo haitachukua muda mrefu kuandika kwa lugha aushi lugha mama ya kiswahili.Stay tuned coming out soon
 
Wakuu kunasehemu nimekuta hili swali, na likanifikirisha sana. "Kama ccm imeshindwa kusimamia bandari ambayo hata haizidi kilometa 10 mpaka wanaamua kubinafisisha je wataweza kweli kutuongoza watanzania ambao tuko mil 60 hadi tupate maendeleo tunayo sthili?"
Kwa hiyo siku hizi kwenye ubinafsishaji maana yake vyama vimeshindwa kuongoza?
Umeishia darasa la ngapi?
 
Mimi nandika kitabu fikirisha cha ujasiamli kitaweza kuisadia jamii maana kinajadili kwa kina mjasiriamali ambavyo anatakiwa aenende kwenye biashara na jinsi ya kukabiriana na yanayomzunguka. Kwenye ujasiriamali tunajifunza kwamba asilimia 80 ya mafaniko yanamtegemea mjasiriamali mwenyeye na hiyo asilimia nyingine ni mjasiriamali na yanayo muzunguka na hapo ndiyo patamu, samahani lakini nimekianadika kwa kimombo japo haitachukua muda mrefu kuandika kwa lugha aushi lugha mama ya kiswahili.Stay tuned coming out soon
Safi kabisa tusaidizane kufundisha na kuelimisha jamii Kwa manufaa ya nchi yetu.
 
Samia anashangaza sana anauza bandari kwa kigezo kwa kisingizio cha kuwekeza

Na watanganyika wanamchekea kuiuza nchi kwa waarabu
 
Kwa hiyo siku hizi kwenye ubinafsishaji maana yake vyama vimeshindwa kuongoza?
Umeishia darasa la ngapi?
Usimbeze ndugu, kwani we husikii pale wasemapo tunatekeleza sera? Mara kila mtumishi awe na sera za chama ofisini maana ndio zinazotekekezwa......bla bla nyingi. Kwa maana hiyo hata bandarini ni sera za CCM zinatekelezwa..ndo sasa hoja yake hii inapopata mashiko!
 
Dhumuni la ubinafsishaji ni kuongeza ufanisi na mapato
 
Maswali muhimu sana ya leo kutoka kwa wadau wawili.

1. Uwezo wa Ccm kuongozw nchi?

2.Wazanzibar kutoilalamikia fursa ya Dp world🤣🤣?
 
Alieuliza swali hilo ni mjinga sana!

Yeye kaona Bandari TU!!?hajaona MADINI,mbuga za wanyama n.k!!?

Kwani tangu ubinafsishaji uanze ni leo ndio kaona mikataba inaingiwa!!?
Mkuu hayo yote mengine alishayaona, ya Loliondogate, na wanyama hai kusombwa namikataba mibovu na makampuni ya madini, lakini hili la bandari lmimkera kupita kiasi.
 
CCM kuna viongozi wazuri sana na wenye elimu na maarifa makubwa sema tatizo ni katiba
Na kwa kuwa kuna unafki, kuvizuana, visasi na kuogopana inabidi Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake tu!
,unafikiri nani asiyependa mwanaye asiende kusoma feza
 
Kwamba ccm ni chama la mafisadi hilo halina ubishi. Ila kwenye hili la bandari hata kama ccm wamekula rushwa kama jadi Yao ni bora mara mia kuliko ubabaishaji uliokua unaendelea bandarini
 
Usimbeze ndugu, kwani we husikii pale wasemapo tunatekeleza sera? Mara kila mtumishi awe na sera za chama ofisini maana ndio zinazotekekezwa......bla bla nyingi. Kwa maana hiyo hata bandarini ni sera za CCM zinatekelezwa..ndo sasa hoja yake hii inapopata mashiko!
Sera ambazo hazina muelekeo chanya
 
Duu hats Raisi anafungwa Speedgavana Bongo Nyoso sihami

Mwana kulitafuta Mwana kulifaindi pole Raisi Mpendwa

Haya ni mapito tuu kaza Buti
 
Kwamba ccm ni chama la mafisadi hilo halina ubishi. Ila kwenye hili la bandari hata kama ccm wamekula rushwa kama jadi Yao ni bora mara mia kuliko ubabaishaji uliokua unaendelea bandarini
Mkuu hapo ndio swali, imekuwaje miaka yote serekali inayotokana na ccm miaka yote, tokea uhuru ishindwe kukomesha huo ubabaishaji wa bandari. Uteuzi wa uongozi wa bandari na usimamizi ulikuwa chini ya nani, kama si serekali ya ccm.
 
Dhumuni la ubinafsishaji ni kuongeza ufanisi na mapato
Unaona sasa! Ndo maana tunahoji ufanisi na mapato ni mpaka tuwape wageni tu. Hata CCM Bashiru aliona madudu mengi kwenye mikataba, kwanini isichukuliwe na wawekezaji ili kuongeza ufanisi wake?
 
naona swali lingekua, je wananchi wameshindwa kuchagua viongozi wa kuwaongoza?
 
Back
Top Bottom