Swali kwa Jaji Mkuu: Je, ni haki kwa kina Rostam Aziz kutozwa faini badala ya kifungo lakini kina Mbarikiwa kupewa kifungo badala ya faini?

Unachanganya mambo!! Suala la Prof Juma kuendelea kuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama ni kitu tofauti na huyo mwehu wenu mnamuita "Mbarikiwa".

Mimi nasema TUIPONGEZE Serikali kwa inachofanya KUDHIBITI hizi madhehebu za kishenzi za akina Mwakilesile maana hata akina Kibwetere au Mackenzie walianza hivi hivi.
 
Aziz anatoka sero anacheka kabisa huku anapiga picha kwa mapozi ya video.

Rostan Aziz aliposema bongo hakuna mahakama bali kikundi cha upigaji tu aliambiwa aombe msamaha ila alisema ukweli.
 
"Individual prophylaxis operation" ndiyo nimeijua leo. Yaani mtu anapewa "operation" ili kuzuia magonjwa, ushaona wapi hiyo? Ni oxymoron kama "fighting for peace".
 
Acha urongo! Mpaka Ruto anaingia madarakani Rostam alikuwa hajaanza kufanya biashara na Kenya.
Sikiliza dada yangu kiwanda kilizinduliwa muda mfupi baada ya Rostam kurudi. Kwanini mwendazake asingekizindua kiwanda ?
 
Unaongelea kiwanda gani, kilichozinduliwa lini, na wapi?
Hujui kitu wewe, unaropoka tu. Kwanza Akram alihukumiwa siyo kwamba aliachiliwa hivi hivi. Kitendo cha kukubali kusaini plea bargain ni kukubali makosa
 
"Individual prophylaxis operation" ndiyo nimeijua leo. Yaani mtu anapewa "operation" ili kuzuia magonjwa, ushaona wapi hiyo? Ni oxymoron kama "fighting for peace".

Elimika:. Chanjo ni operesheni inayomlenga mtu mmoja mmoja kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya kibayolojia ("Individual prophylactic operation"). Kutibu maji ya bomba yanayotoka mto Ruvu na kuingia Dar ni operesheni inayowalenga umma kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya mlipuko ("mass prophylactic operation").

Kwa kutumia mantiki hiyo hiyo tunaweza kukubaliana kuhusu kuwepo operesheni ya kuzuia magonjwa ya kiusalama, katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, yaani "Individual prophylactic operation". Kwa kutumia mantiki hiyo hiyo unaweza kukubaliana kuhusu kuwepo operesheni ya kuzuia magonjwa ya kiusalama katika ngazi ya kimakundi, yaani "mass prophylactic operation".

Katika operesheni za kiusalama, tunapoongelea "Individual prophylactic operation" tunamaanisha "operation" ya kumdhoofisha mtu ambaye tayari tumempa hadhi ya kuwa "tishio la kiusalama." Ni "operaion" ya kumwondolea nguvu indirectly ili asiendelee kuwa tishio.

Mfano, kama wewe tumekutafsiri kama tishio, tutafuatilia mwenendo wako wote. Tukijua umeandika barua ya kuomba kazi mahali, tuseme kwenye kampuni ya Dangote, sisi tunapeleka barua rasmi kwa Dangote yenye dokezo la kiusalama kusema kwamba, "Mwombaji wa kazi XYZ aliyeleta maombi kwenu tunamchunguza kwa tuhuma za ugaidi, kwa hiyo kuweni makini msije makaajiri gaidi."

Hakuna mwajiri angependa kujitumbukuiza kwenye matatizo kama hayo. Kwa njia hiyo, huweza kupata ajira kwake. Kwa kukosa ajira hutapata nguvu ya kifedha. Kwa kukosa nguvu ya kifedha hutaweza kuendeleza kile ambacho sisi tumeshakiita "tishio.'

Pia tunaweza kuchukua hatua ya kukuchafua kijamii. Tutapita kwenye mtaa wako unakoishi na kusambaza taarifa kila kijiwe, kwamba, "Huyu jirani yenu anayeitwa XYZ ni shoga, kwa hiyo kuweni makini naye asije akawalawiti watoto wenu wa kiume." Mara unashangaa kila jirani anakunyima ushirikiano, hata bila kukwambia sababu.

Mfano huu wa pili ni mbinu ya propaganha chafu. Mara nyingi inatumia mkakati unaoitwa "fallacy of association." Kwenye siasa, mbinu hii hutumiwa na kamati za fitina. James Mbatia aliwahi kuwa mhanga wa fitina za aina hii, kwa kupakwa matope ya kwamba yeye ni "shoga" kisa aliwahi kuonekana akiwa katika gari moja la mtu ambaye ni shoga.

Hii ndiyo maana ya "Individual prophylactic operation" niliyoikusudia. Mifano hii miwili inatosha kukufungua macho. Hivyo sasa utaelewa ninaposema kwamba kitendo cha kuua mtoto wa Mchungaji Mbarikiwa kilikuwa ni "Individual prophylaxis operation." Ukifiwa na mtoto wako, ratiba zako zote zinabadilika, uchumi wako unayumba, kisaikolojia unatikisika, na kelele zako dhidi ya watawala zinatulia kwa muda.

Tanzania tulikuwa hatutumii mbinu hii mpaka hivi karibuni baada ya kupatikana kwa baadhi ya wakuu wa vyombo vya usalama wasioamini katika ukuu wa tunu ya uhai wa watu wasio na hatia.
 
Niko hapa kujifunza sheria

cc: Pascal Mayalla
Samahani mkuu kwa kutumia lugha kali ila" sheria na wanasheria hasa wa tz ni usenge mtupu" vifungu vinatafsiriwa kutokana na ni nani anashtakiwa.
 
Maelekezo kutoka juu.

Eananchi hawapaswi kujitambua wala kudai haki zao. Tanzania ni uhaini kuwakosoa watawala.

Yapo makanisa na huduma za kiroho nyingi sana hawana usajili na wanaendesha huduma zao namna hiyo.

Madikteta waoga huishia pabaya sana. Sonona itawafuata maisha yao yote labda watubu
 
Mimi nimetafsiri literally kwa Kiingereza. Basi hii phrase itakuwa made in Tz lingo sbb haileti maana kwa Kiingereza cha kawaida. Mama Amon wee kumbe ni usalama wa taifa?
 

Hata sijaelewa umeongea nini! Lakini, chini ya ibara ya 27 na 28 ya Katiba ya Tanzania (1977) kila mtu na wato wote ni walinzi wa usalama wa Taifa. Jisomee:



Kwa maarifa zaidi jisomee vitabu vifuatavyo (attached) kuhusu maana ya maneno "Ulinzi wa Taifa" yanayosomeka kwenye ibara ya 28 ya Katiba ya Tanzania (1977):

1. David Omand (2010), Securing the State (New York:OUP)

2. David Omand (2020), How Spies think: Ten Lessons in Intelligence (Penguin Books Ltd)
 

Attachments

Sawa. Huu msemo “Individual prophylaxis operation” wapi chanzo chake? Google phrase search nimeambulia sifuri.

Mara ya kwanza niliusikia kutoka kwenye kinywa cha mwalimu wangu wa masuala ya statecraft, Peter Nyamanchi Tyienyi. Sasa ni mrehemu. Lakini, ufafanuzi ufuatao utakufaa.

 
Sheria huwa haina jicho linalofanana. Unapoona sheria haitoi adhabu moja basi ujue hapo macho yanaweza kutofautiana. Sababu ziko nyingi kila mtu anaweza kuwa na yake.
 
Sheria huwa haina jicho linalofanana. Unapoona sheria haitoi adhabu moja basi ujue hapo macho yanaweza kutofautiana. Sababu ziko nyingi kila mtu anaweza kuwa na yake.

Lakini kazi ya sheria ni kuisaidia jamii kujua kesho kutatokea nini, yaani kutabirika kwa maisha ya watu, au tuseme predictability. Unasemaje kuhusu sifa hii muhimu inayopswa kuwa sifa mojawapo ya sheria zote duniani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…