The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Yeye Mama kanumba kasema mahakama imetenda haki kwa hukumu iliyotolewa wala hajaongelea swala la uhusiano wa Kanumba na lulu
Halafu kuhusu lulu kuwa mtoto Hakimu alisema hivi nanukuu
"Kuhusiana na umri mdogo wa Lulu wakati tukio hilo linatokea mwaka 2012, Jaji Rumanyika amesema sheria ya kumlinda mtoto haimpi kinga Lulu kwa sababu huo alikuwa akifanya mambo ya watu wazima."
Sijajua kisheria hii kauli kwamba alikua mtoto lakini anafanya mambo ya watu wazima imemaanisha nini?
Kinachoamua utoto wa mtu ni matendo au umri? Hapo tunaangalia kwa upande wa kisheria. Mtu mzima anaweza kufanya mambo ya kitoto akaepushiwa hukumu kwamba ni mtoto licha ya umri wake?