Swali: kwa nini Harrier, Vanguard ( 2AZ engine ) 2400 cc zinakula mafuta kuliko Mark X ( GRX engine ) 2500 cc?

Swali: kwa nini Harrier, Vanguard ( 2AZ engine ) 2400 cc zinakula mafuta kuliko Mark X ( GRX engine ) 2500 cc?

Complex

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
4,119
Reaction score
4,779
Kwa nyakati tofauti nimepata kuendesha hizi gari mbili. Harrier na MarkX. Harrier nnayoizungumzia hapa ni tako la nyani yenye engine ya 2AZ na CC 2400. Na mark X nnayoizungumzia hapa ni 250G yenye engine yenye code GRX. Kilichonileta hapa niulaji wa mafuta wa hizi engine mbili.

Kitaka uchunguzi wangu kupitia uendeshaji wa magari haya, nimeona harrier yeny 2AZ inakula mafuta sana kulinganisha na MarkX yenye GRX ilhali mark X ni ina CC kubwa kuliko Harrier. Mark x iliweza kunipa range mpka ya 8Km per liter kwa town trips huku harrier best range niliyopata ni 6.5 km per liter.

Wataalamu nini kinasababisha hili, ukizingatia GRX ni V6 yenye 6 Cylinder huku 2AZ ni VVTi yenye 4 cylinders. Perfomance ya 2AZ pia niliinote kwenye Vanguard na Rav4 na mwote range ni hiyohiyo.
 
Kwa nyakati tofauti nimepata kuendesha hizi gari mbili. Harrier na MarkX. Harrier nnayoizungumzia hapa ni tako la nyani yenye engine ya 2AZ na CC 2400. Na mark X nnayoizungumzia hapa ni 250G yenye engine yenye code GRX. Kilichonileta hapa niulaji wa mafuta wa hizi engine mbili...
Mkuu kuna jamaa yangu alinihusia kuwa miliki kifaa kilicho katika uwezo wako! Mfano hela yako ya nyanya unatafuta girlfriend! Wewe size yako ni wa buku mitaani na maisha yanasonga. Hivyo ukianza kuona gari linakula mafuta jua unajibebesha Mizigo wa bure pengine saizi yako ni baiskeli na daladala.

Na Ukiona mtu anamiliki gari analalamika kuwa gari halina mafuta juwa ni wale wale wanaobeba vifaa vinavyowazidi uwezo. Aidha kwa kujibu swali lako, ulaji wa mafuta hutegemea na uchakavu wa injini n.k. Huwezi kulinganisha matumizi ya mafuta ya gari la 2020 na la 1980 kwa leo.
 
Harrier ina uzito wa 1,800kg while Mark X ina uzito wa 1,500 kg.. So kuna increment ya kama 300 kg.. Engine ya Harrier inafanya kazi zaidi.
Ni sawa na Pajero Mini ya 660cc inatembea hadi km 15 kwa lita wakati Vitz ya 1000cc inatembea hadi km 20 kwa lita ihali zote zina uzito wa 1000kg.
Hii inasababishwa na factors mbali mbali kama umbo la gari ambalo lina affect wind resistance etc... Pia engine ya Pajero Mini
inaoperate at higher RPM compared na Vitz ili kuzalisha the same amount of Horsepower.
 
Ukisema inatumia umeme mwingi unakua unamaanisha nini mkuu?
Tukisema umeme mwingi ni Ile namna engine za kisasa zinazotumia mfumo wa ECU (engine control unit) au zile engine zenye mfumo wa start stop engine
Screenshot_2020-08-22-18-52-54.png
 
Mkuu kuna jamaa yangu alinihusia kuwa miliki kifaa kilicho katika uwezo wako! Mfano hela yako ya nyanya unatafuta girlfriend! Wewe size yako ni wa buku mitaani na maisha yanasonga. Hivyo ukianza kuona gari linakula mafuta jua unajibebesha Mizigo wa bure pengine saizi yako ni baiskeli na daladala. Na Ukiona mtu anamiliki gari analalamika kuwa gari halina mafuta juwa ni wale wale wanaobeba vifaa vinavyowazidi uwezo. Aidha kwa kujibu swali lako, ulaji wa mafuta hutegemea na uchakavu wa injini n.k. Huwezi kulinganisha matumizi ya mafuta ya gari la 2020 na la 1980 kwa leo.

Mzee sijalalamika kuhusu ulaji wa mafuta, na hilo si tatizo bali nahitaji uelewa wa hicho nilichokiuliza ili watumiaji wa vyombo vya moto haswa madereva tupate kuwa na uelewa wa mambo mbalimbali yahusuyo magari na changamoto ama faida zake kama ilivyo lengo la jukwaa kuhabarishana.

Kuhusu muda Mark X ni ya zamani kuliko Harrier. HARRIER ni ya 2006 wakati Mark X ni ya 2006.

Na nimeuliza hili swali kwa kuwa nilishaona mahali humu jukwaani wadau walikuwa wanaelekezana kuwa Alteza ya 6 cylinder ni economy na ina ulaji mzuri wa mafuta kuliko alteza ya 4.

Hivyo nilihitaji uelewa zaidi juu ya haya maswala ya engine na ulaji wa mafuta.
 
Factors za kula mafuta si CC za engine tu. Labda huwa unakamua sana unapokua na hizo 2AZ

Kuhusu uendeshaji wangu ni ule ule, pattern ya ukanyagaji wangu wa mafuta nikiwa katika Vitz, Harrier, passo ni ule ule. So sidhani kama hii ni sababu.

Kwa msaada wa jukwaa, unaweza eleza hizo factors nyingine zinazochangia ulaji wa mafuta.?
 
Lkn hii haina mahusiano yoyote ya maana na ulaji wa mafuta,nilidhani ukisema umeme mwingi unamaanisha hio gari ina mfumo wa hybrid au Plug-in.
Swali lako gumu kidogo Ila pengine mafundi-nyundo wa Temeke watakuja kutusaidia
 
Kuhusu uendeshaji wangu ni ule ule, pattern ya ukanyagaji wangu wa mafuta nikiwa katika Vitz, Harrier, passo ni ule ule. So sidhani kama hii ni sababu.

Kwa msaada wa jukwaa, unaweza eleza hizo factors nyingine zinazochangia ulaji wa mafuta.?
Nyingi mno, underinflated tyres (matairi kuwa na upepo chini ya kiwango chake kinachostahili), ‘poor coil conduction, (coil za kuchoma mafuta zimekuwa weak na hazichomi ipasavyo, ‘Uchafu kwenye throttle body’ au ‘uchafu kwenye exhaust, na mengine mengi kama EFI miss timing na mengine ya Engine Control unit malfunction (ECU)
 
Mzee sijalalamika kuhusu ulaji wa mafuta, na hilo si tatizo bali nahitaji uelewa wa hicho nilichokiuliza ili watumiaji wa vyombo vya moto haswa madereva tupate kuwa na uelewa wa mambo mbalimbali yahusuyo magari na changamoto ama faida zake kama ilivyo lengo la jukwaa kuhabarishana...
Ukichukua mwaka uliotengenezwa haitakuwa sahihi bila kulinganisha na matumizi (Imetembea kilomita ngapi) na services, cruising etc. Ni factor nyingi sana.
 
Ukichukua mwaka uliotengenezwa haitakuwa sahihi bila kulinganisha na matumizi (Imetembea kilomita ngapi) na services, cruising etc. Ni factor nyingi sana.

Harrier imetembea KM 77000 mpaka sasa, Mark X inakaribia 100,000 KM mpaka sasa.
 
Mkuu kuna jamaa yangu alinihusia kuwa miliki kifaa kilicho katika uwezo wako! Mfano hela yako ya nyanya unatafuta girlfriend! Wewe size yako ni wa buku mitaani na maisha yanasonga. Hivyo ukianza kuona gari linakula mafuta jua unajibebesha Mizigo wa bure pengine saizi yako ni baiskeli na daladala. Na Ukiona mtu anamiliki gari analalamika kuwa gari halina mafuta juwa ni wale wale wanaobeba vifaa vinavyowazidi uwezo. Aidha kwa kujibu swali lako, ulaji wa mafuta hutegemea na uchakavu wa injini n.k. Huwezi kulinganisha matumizi ya mafuta ya gari la 2020 na la 1980 kwa leo.
We unaonekana magari umeyajulia ukubwani afu mshamba fulani hivi.

Ingekua utumiani wa mafuta sio ishu mbona MABEBERU kila siku wanaumiza kichwa watengeneze magari yenye low fuel cosumption??? Au na wao hawana uwezo wa kununua mafuta?

Tatizo upeo.
 
Back
Top Bottom