Huyu jamaa kwa sasa, amekuwa ni mmoja wa watu wa hovyo sana kwenye siasa za Tanzania, enzi za Mwamba, JPM, jamaa alikuwa very strong politician, nilimuoja ni mmoja wa mashujaa, Chadema walipohukumiwa faini, JPM akatoa pesa akamtuma Msigwa, wakamlipia faini, Msigwa na Mashinji tuu, Mashinji aliishamfuata Ngosha mwenzake, wakitegemea na Msigwa akitoka ange cross, jamaa akatoka, akashukuru kulipiwa faini, kisha akakomaa kusalia Chadema, huu ni ushujaa, fedha za Msigwa zikamlipia Heche!.
Baadaye sijui kikamkuta nini, mara ghafla huyu Shujaa Msigwa, akalainika na kutepeta, akahama Chadema na kujiunga CCM!, akaanza kuwatukana Chadema!, tukampa angalizo
Angalizo kwa Wanasiasa hamahama; Japo ni haki yenu lakini msisahau fadhila. Kuweni watu wa shukrani, mtabarikiwa sana, vinginevyo karma Itawahusu! humo nilisema
Kitendo cha Mch. Msigwa kurejea Chadema, huu ni uthibitisho, huyu ni mwanasiasa kama anavyoelezewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere
View: https://youtu.be/E79zLqNM7yg?si=CGNyiDr9FyEyROn3
Huyu ndio Mchungaji Msigwa, alikwenda CCM akitegemea, uteuzi, kakosa uteuzi, karudi kwa bwana wake wa zamani!.
Poor him!.
P