britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,295
- 33,994
Hofu yote hii ni ya nini? Mmeondoa "local chanels" kwenye ving'amuzi vyote ikiwemo Dstv l, mmebakiza TBC tu. Mmelazimisha nchi nzima itizame TBC. Hamjaridhika, sasa mmehamia kwenye radio. Mnatunga kanuni za kuzuia watu kusikiliza radio za nje? Lengo ni nini?
Yani sasa hivi Dira ya Dunia ya BBC, Meza ya duara ya DW na habari za ulimwengu za VOA hatutazisikia tena hadi kibali kutoka TCRA? Ujinga gani huu?
Halafu hizi radio za nje zinazotangaza kwa kiswahili zimesaidia sana kukuza Kiswahili kimataifa. Zilianza BBC, DW na VOA lakini leo radio zenye idhaa ya Kiswahili ni nyingi sana duniani. Radio Japan, Radio Tehran, Radio China International, Idhaa ya Kiswahili ya umoja wa mataifa, Radio France Internationale etc.
Na watanzania wengi wamepata ajira kwenye vyombo hivi vya habari. Kupitia radio hizi Kiswahili kinasikilizwa sana nchi za jirani. Nenda Burundi uone watu wanavyosikikiza matangazo ya mchana ya DW, nenda Uganda uone watu wanavyosikiliza Dira ya dunia ya BBC. Kiswahili kinakua sana. Lakini leo kwa sababu ya ubinafsi tunazuia vyombo hivyo kusikika hapa nchini. Tunataka watu wote wasikilize kuhusu reli ya SGR na Flyover za Ubungo.
Hii si sawa hata kidogo. Tunakoelekea ni pabaya sana. Dalili mojawapo ya kupoteza uhuru wa habari ni kulazimisha kila mtu asikilize mawazo yako, na kukataa kusikiliza mawazo mbadala. Tuendelee kukaa kimya hadi siku tutakayoambiwa huruhusiwi kukohoa hadi kibali cha Muhimbili. Labda ndo tutapata akili.!