Uchaguzi 2020 Swali kwa Rais Magufuli: Hofu ya nini juu ya Vyombo vya Habari?

Uchaguzi 2020 Swali kwa Rais Magufuli: Hofu ya nini juu ya Vyombo vya Habari?

Mwanamke mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,,,na nyinyi ccm naona kabisa ndoa mliyofunga na watanzania mwaka 1961 mnaenda kuivunja nyinyi wenyewe kutokana na uoga wenu unaowapelekea kufanya maamuzi ya kipumbavu kama haya ya sakata la vyombo vya habari.
 
Hawa wanaojipendekeza kizembe wanasababisha matatizo makubwa sana kwa wafuatao watoto wao wakiwepo kwa kupenda sifa za kijinga kutwa kubariki maamuzi ya hovyo utadhani wataishi ktk nyadhifa hizo milele, Uzee wao utakuwa mgumu sana. Simaanishi kufurahia lkn wengi wao tuko nao baba zetu huku wakipiga story unajua tu upuuzi walioufanya ila ndio hawana namna tena.

Wengine wa awamu zilizopita tunawaona na tunaishi nao huku yani huwezi kuamini alikuwa kiongozi ila historia imemsahau kwa kuwa alidhani na yeye ataishi kama maraisi wastaafu na watoto wao wamevurugika hata hawana msingi tena.

Kuna wabunge wanapiga makofi ku support upuuzi na sheria kandamizi lkn narudia tena wabunge wa awamu tatu za mwanzo tayari wengine wapo huku mtaani hata serikali haiwakumbuki wamejawa na magonjwa ya utu uzima hata watoro hao hawana msaada.
 
I think tunarudi enzi za Nyerere kila mtu kusikiliza tbc, mnapangiwa mpaka Cha kutazama na ni mwendo wa kusifia tu. Na hao walikuwa wanafanya kazi kwenye idhaya za kiswahili pole kwao
 
Tena maamuzi haya yalipaswa yafanywe mapema zaidi, maana Kama wanatumia vyombo vya habari za kimataifa Bora tubaki na RTD tu hakuna namna😂🤣😂! Hakuna kucheka na nyani😠! Msioweza kuishi bila hivyo vyombo vya habari vya nje nendeni huko xilipo mzifuate!
Ukisikia mtu anaambiwa ana akili za kuendea chooni tu basi ndio hizi 😁😁!
 
Mbona radio zinazotangaza kwa kiswahili huko japan zinabalance story?
Wakiwamaliza wapinzani wotee watahamia uko uko kwa ccm wenzenu iyo ndo zambi ya ubaguzi haiach mtu kama mla nyama za watu akianza kula kidog tu utamu wake hauchoshi,wakiisha wapinzani na tusio na vyama watahamia kwa ccm wa kisukuma,wagogo na wamakonde amka mkuu.
 
Tena maamuzi haya yalipaswa yafanywe mapema zaidi, maana Kama wanatumia vyombo vya habari za kimataifa Bora tubaki na RTD tu hakuna namna😂🤣😂! Hakuna kucheka na nyani😠! Msioweza kuishi bila hivyo vyombo vya habari vya nje nendeni huko xilipo mzifuate!
Nashangaa sana kama vilikuwa vinarusha matangazo bila vibali.
 
Hofu yote hii ni ya nini? Mmeondoa "local chanels" kwenye ving'amuzi vyote ikiwemo Dstv l, mmebakiza TBC tu. Mmelazimisha nchi nzima itizame TBC. Hamjaridhika, sasa mmehamia kwenye radio. Mnatunga kanuni za kuzuia watu kusikiliza radio za nje? Lengo ni nini?

Yani sasa hivi Dira ya Dunia ya BBC, Meza ya duara ya DW na habari za ulimwengu za VOA hatutazisikia tena hadi kibali kutoka TCRA? Ujinga gani huu?

Halafu hizi radio za nje zinazotangaza kwa kiswahili zimesaidia sana kukuza Kiswahili kimataifa. Zilianza BBC, DW na VOA lakini leo radio zenye idhaa ya Kiswahili ni nyingi sana duniani. Radio Japan, Radio Tehran, Radio China International, Idhaa ya Kiswahili ya umoja wa mataifa, Radio France Internationale etc.

Na watanzania wengi wamepata ajira kwenye vyombo hivi vya habari. Kupitia radio hizi Kiswahili kinasikilizwa sana nchi za jirani. Nenda Burundi uone watu wanavyosikikiza matangazo ya mchana ya DW, nenda Uganda uone watu wanavyosikiliza Dira ya dunia ya BBC. Kiswahili kinakua sana. Lakini leo kwa sababu ya ubinafsi tunazuia vyombo hivyo kusikika hapa nchini. Tunataka watu wote wasikilize kuhusu reli ya SGR na Flyover za Ubungo.

Hii si sawa hata kidogo. Tunakoelekea ni pabaya sana. Dalili mojawapo ya kupoteza uhuru wa habari ni kulazimisha kila mtu asikilize mawazo yako, na kukataa kusikiliza mawazo mbadala. Tuendelee kukaa kimya hadi siku tutakayoambiwa huruhusiwi kukohoa hadi kibali cha Muhimbili. Labda ndo tutapata akili.!
Propaganda na ukweli halisi unaenda kujitenga hofu ya kufichuliwa uongo na madudu.
 
Hiyo ni lazima, cha muhimu ni kujua tu watakapofungia tuhamie wapi. Wakati ule wa mizengwe tulihamia kenya talk.

Haijalishi,mkoloni aliondoka bila uwepo wa media na taarifa zilifika kila mahali,
wanakimbiza upepo na siku ya kufa nyani.

TUKIRUDIA KOSA ATALIPIZA KISASI SANA,MEDIA ZOOTE KWA PAMOJA ZINGEUNGANISHA NGUVU YA UMMA KWA PAMOJA TUNASHINDA TUKATAE TUPINGE UDHALIMU TUPINGE UKOMUNISTI PINGA UDIKTETA HAKUNA ALIYE SALAMA KESHO UTAUMIA ZAMU YAKO JAPO LEO UNACHEKa
 
Tena maamuzi haya yalipaswa yafanywe mapema zaidi, maana Kama wanatumia vyombo vya habari za kimataifa Bora tubaki na RTD tu hakuna namna😂🤣😂! Hakuna kucheka na nyani😠! Msioweza kuishi bila hivyo vyombo vya habari vya nje nendeni huko xilipo mzifuate!

We unaota ndoto za mchana🤣😂🤣!

We endelea kuota ndoto, usiote tu unakunya😂🤣😂!
kuukimbiza upepo tu still habari zinafika ,hatupo kwenye zama za ujima
 
Wanajichosha tu.. Tv za Kenya zote zipo..
 
Back
Top Bottom