Swali kwa Tundu Lissu: Kama Corona ipo Tanzania, kwanini toka alipoingia Tanzania na kipindi chote cha kampeni miezi mitatu hakuvaa Barakoa?

Njia gani ya kujikinga? distancing alikuwa hafanyi, mikona alikuwa akipeana na watu kama kawaida hadi kukubatiana huku akiwa anazongwa na watu kila kona!
Ulikuwa una lala nae? Sio kila jambo ujifanye unajua, mambo mengine kaa kimya tu
 

Unachanganya kati ya uwepo wa ugonjwa na kuchukua tahadhari ya ugonjwa. Wote sisi tunajua kuwa ukimwi upo, je ni wangapi wanavaa kondomu kwakuwa ukimwi upo? Usidhani watu wanaovuta sigara kuwa hawajui inaleta cancer.
 
Tumuulize lissu yeye angekuwa raisi angefanyaje
 
Unachanganya kati ya uwepo wa ugonjwa na kuchukua tahadhari ya ugonjwa. Wote sisi tunajua kuwa ukimwi upo, je ni wangapi wanavaa kondomu kwakuwa ukimwi upo? Usidhani watu wanaovuta sigara kuwa hawajui inaleta cancer.
Kwa hiyo Lisu alikuwa akifanya kusudi akiwa Tanzania ili aambukizwe corona? Mbona hakuambukizwa sasa kama ipo? Ukimwi upo ukivunja masharti unakuvaa je Lisu mbona pamoja na kuvunja masharti ya kujikinga na Corona mbona haikumpata ingekuwepo si angekiona cha mtema kuni
 
Kwani YEHODAYA . Corona (Covid 19) haipo Tanzania? Kwani aibu ya nini na Corona haijaanzia Tz?!

Tundu ndiyo unaemuona? Waulize viongozi wenye dhamana wamewaandaa wananchi namna gani.

Waulize wengine waliofanya dhihaka na Corona, leo wanajuta.
Muulize Maalim Seif alipata wapi na hajakwenda nje ya nchi kupata chanjo na kurudi nayo.
 
Swali la kitoto, mbona huko kwenye Korona inayoua watu 1,000 kwa siku baadhi ya watu hawavai barakoa.
Fikiri kabla haujaandika, usiandike kwa sababu tu unamchukia mhusika.
Ila hilo sio jibu mkuu,ina maana kama kuna watu wanaona corona ni uzushi tu katika hizo nchi ndio tuwatumie hao na sisi kusema hakuna corona?

Hapa Bongo serikali inalalamikiwa kwa kudanganya kuwa hakuna corona na hivyo watu wanakuwa hawachukui tahadhari za kujikinga na corona na ndio maana wengi unakuta hawavai hata barakoa.

Sasa Lissu nae anapofanya kama hao wanaomini hakuna corona kwa kutochukua tahadhari za kujikinga na corona hiyo inaleta maana gani hasa ukizingatia watu walikuwa wanakusanyika kumsikiliza yeye pasina tahadhari zozote huku akijua jambo hilo ni hatari kwa maambukizi ya corona.
 
Sawa Corona hamna; sasa kwa nini mnawataka watanzania wapige nyungu!!
 
Korona ilikuwepo kidogo tu wakati ule.

But sasa imerudi kwa nguvu zote na watu wanakufa left right and centre goddamn it!!
 
ukiwaskiliza sana hawa upinzani unaweza kua na akili kama zao, naskia wanasema tanzania kuna corona na wanaita watu kwenye kampeni, hizi ndo akili za ufipa bana!
 
Corona ilikuwepo ikapungua sana tu kama ikapotea sababu ya heard immunity hii ni second wave kutoa SA mdudu kajigeuza ipo sana temebelea Hosp ndio utajuwa hali sio shwari.

wewe hujiulizi kwanini viongozi wanatumia nguvu sana kukana. jana katibu kafanya ziara yeye anaonesha havai barakoa watumishi wote barakoa sababu wanaona wagonjwa daily wanajuwa hatari mbele yao. Ipo sana tuombe Mungu hii nalo lipite kama la kwanza lakini sio kukataa hakuna.
 
Natoka Muhimbili JKCI sasa hivi hakuna kuingia kumuona daktari kama hujavaa barakoa na wateja wamepungua sana kwa kuogopa maambukizi.
Jitu linaropoka eti hakuna Corona ilihali hana research,facts wala figures.
Huko huko Muhimbili kuingia wodini kuona wagonjwa kuna zuio kubwa sabb ya covid19.

Death rate inatisha huko.

Uongo na MATAGA ni sawa na kidole na kucha
 
Swali kwake, Kama Corona ipo Tanzania kwa nini toka alipoingia Tanzania na kipindi Chote cha kampeni miezi mitatu hakuvaa Barakoa na hakuugua Corona yeye na umati wote ule uliokuwa unafurika mikutano yake?
Kama corona haipo, kwa nini majuzi jiwe na waziri wake walitoa wito kwa watz wote kupiga NYUNGU kwa siku 7 ?!!!
 

Ili ugonjwa ufahamike kuwa upo Tanzania ni sharti kila mtanzania aupate? Kama huna hoja za kutetea huu utoto wako ni vyema ukakaa kimya we dogo.
 
Kila mtu humu kwa judgement zao wameona ni swali la kijinga

Naenda nao,siwezi kwenda na wewe
Si suala la kwenda na mimi au nani hoja hapa ni kwamba swali lililoulizwa ni la msingi na nimeeleza kwanini hilo swali ni la msingi,sasa kama kuna mtu anaona si swali la msingi aeleze ni kwanini anaona si swali si la msingi lakini huwezi kuniambia kwamba umewafuata watu fulani ambao wamesema si swali la msingi bila kutoa maelezo.
 
Ilipunguaje hiyo corona hapa Tz mkuu au ndio yale maombi? mimi hili jambo la Corona kupungua linanitatiza sana.
 
Korona ilikuwepo kidogo tu wakati ule.

But sasa imerudi kwa nguvu zote na watu wanakufa left right and centre goddamn it!!
Hata kama ilikuwepo kidogo kama unavyodai mkuu ina maana ndio ilikuwa sahihi watu kukusanyana vile bila tahadhari zozote kipindi cha kampeni? kilichofanyika si ndio kuongeza maambukizi.
 
Maalimu Seif anaumwa nini tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…