Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,772
Korona sio suala la Tundu Lissu bali wewe na familia yako. Korona ni suala la afya, ila kwa akili za kuokoteza na MATAGA, mmegeuza kuwa ishu ya kisiasa.Tundu Lissu amekuwa akidai kuwa Corona Tanzania ipo akiwa Ubelgiji ukimbizini. Akiwa Tanzania hakusema toka siku ya kwanza alipotua tu uwanja wa ndege alivua barakoa na hakuivaa tena kipindi chote cha miezi mitatu aliyokaa Tanzania akifanya kampeni akizungukwa na umati wa watu wasiovaa barakoa.
Alipokuwa akiondoka nchini kurudi ubelgiji akiwa Airport ndio akavaa barakoa ya kuondoka nayo kwenda Ubelgiji.
Swali kwake, Kama Corona ipo Tanzania kwa nini toka alipoingia Tanzania na kipindi Chote cha kampeni miezi mitatu hakuvaa Barakoa na hakuugua Corona yeye na umati wote ule uliokuwa unafurika mikutano yake?
Nadhani hata wazungu sasa watamuona hayuko sawa na kuwa taarifa zake si za kuaminika na yeye si wa kuaminika, akiwa Tanzania anakuwa kivingine akiwa kwao kivingine.