Swali kwa upinzani: Je, tatizo lenu ni Magufuli au CCM?

ASIWAJU

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
1,938
Reaction score
1,632
Ningependa kuwa karibisha wafuasi wote wa siasa za upinzani hapa nchini katika hili swali langu fupi kwa majibu yao.

SWALI:
Tatizo sugu la wapinzani wa hapa nchini je ni Magufuli na utawala wake wa awamu iliyo pita [ awamu ya tano ] au tatizo ni CCM yote ?

KARIBUNI
 

Vyote kwa pamoja.
 
Hivi kwa mfano nikuulize Ole sabaya kafungwa na chadema? Leo mnyeti kapandishwa kizimbani Chadema ina serikali? Kwanini mnapenda kuihusisha Chadema kwenye matendo maovu yaliyofanywa na utawala wa awamu ya 5 chini ya Marehemu magufuli aliyekuwa mwenyekiti wa CCM?
 

Hao hawajui wanachokitaka kwa ajili ya wananchi.
 
Kwenye swali umeona nime izungumzia Chadema hapo ? tubaki kwenye msingi wa swali karibu kwa majibu yako tena.
 
Maridhiano ilikuwa , maiti ina nguvu kuliko Sisi CCM na ina nguvu kuliko nyie Chadema , inabidi tuunngane kupambana nayo
Naomba jibu lako tena upya linalo eleweka vizuri kwa kila mmoja kutokana na swali lilivyo uliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…