Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Hapa naona umegusia suala la Mufhuum, al Mukhalafah, suala hili hutakiwi kuliingia kichwa kichwa, sababu ndani yake kuna khilafu, mahanafi wanapinga suala hili, kwa hoja ya kuwa lazima iwepo dalili ya kuonyesha maana hiyo ya kinyume
Hata kama zipo khilaafu haifanyi mimi niache kutumia mafhum mukhaalafa kwa kuwa tu kuna ikhtilaafu.

Ikhtilaafu zipo na nazikubali lakini kwa hoja zenye nguvu upande wangu ni kuwa mafhum mukhaalafa ipo.

Hapa naona unataka kunilazimisha kama kawaida yako nifuate ule upande unaoutaka wewe,yani kwa kuwa katika hili unaona kuna dhehebu wanapinga basi na wewe ndugu yangu unataka kunilazimisha nikatae kama wao.

Wao wana hoja zao ila kwa upande wangu mimi lenye nguvu ni kuwa mafhum mukhaalafa yapo kwa dalili zilizonitosheleza.

Kwa hiyo bado nashikilia mafhum mukhaalafu kuwa ipo kwa upande wangu,wao kama wanaona hivyo ni wao kwa upande wao huo.


wewe huna dalili hiyo ya kuwa kinyume chake ni Wanawake watoke
Unatakiwa kusema hivi ikiwa kama nimekubali kuwa mafhum mukhaalafa haipo.

Ila nasema kuwa mafhum mukhaalafa ipo kwa hoja zilizonishiba kwangu,usilazimishe kuwa mafhum mukhaalafa haipo wakati mimi nimetosheka na hoja za kuwa IPO.

Kwa hiyo hapo dalili ninayo kama ambavyo nimesema kuwa mafhum mukhaalafa hapo inahusika KWA UPANDE WANGUna hoja nilizoangalia.

Kwa hiyo dalili hapo ipo.


na aya aya haikuonyesha mwanamke atoke kwenda kutafuta hela,

na aya aya haikuonyesha mwanamke atoke kwenda kutafuta hela, sababu athari zimenukuliwa kwa wingi mwanamke alitoka katika mambo fulani. Sasa ndiyo maana suala la mwanamke kutoka kwenda kwenye kutafuta ugali bado suala ni la dharura, na ndiyo maana Ulamaa wamelikadiria kwa kurejea misingi ya aya na hadithi.
Aya haikuonesha sawa ila kutokuonesha kwake bado sio dalili kwa sababu kuna mengi hayajaoneshwa na bado ni halali.

Kama ambavyo hakuna dalili ya kuwa mwanaume anakatazwa kukaa nyumbani na kulea familia basi ndivyo hakuna dalili ya kumkataza mwanamke kutoka na kwenda kutafuta.

Ama dalili hiyo ipo ?

Nimeshaandika sana kuhusu hilo suala na nikakuambia kuwa kutafuta mahitaji ama mwanamke kufanya kazi kiasili ni jambo lenye kujuzu.

Inajuzu hayo lakini utambue kuwa katika uwanja wa ndoa sasa kwa mwanamke inajuzu na kwa mwanaume inakuwa ni wajibu kwake.

Kwa hiyo kuhusu kujuzu hilo halina shaka kwa sababu asili ya hili jambo hakuna katazo la mwanamke kutoka kwenda kwenye haja zake anazoziona za muhimu na za halali.

Bado haujawa na dalili ya kukataza hili.

Hadithi pia zinakugeuka namna ambavyo unazichukua jumla jumla ndugu zurri.


Kadhalika watu wa madhehebu ya Shafi, wana mapito yao juu ya hili.
Leo ndo unatambua kuwa kuna ikhtilaafu,hayo mapito yao na mimi nina mapito yangu ambayo ndo nahoji hapa.

Ukiniletea kauli za watu fulani sizikubali mpaka ziwe zimebeba hoja zenye nguvu sio za kulazimisha kitu kiwe haramu.
 
Sasa ndiyo uone hakuna haja ya wao kusoma udaktari kwa sasa sababu hao waliosoma wanakidhi hilo,
Sasa hapa nakuuliza tokea hapo kuwa kuwepo kwa wanaokidhi hizo haja ni dalili kuwa hawa ambao hawajasoma ni haramu ?

Yani kuwepo kwa watu ambao watamswalia maiti ina maana kuwa wengine wakitaka kuswalia ni haramu kwa kuwa kuna ambao wameshatosha kukidhi jambo hilo ?

Alafu pia haja ipo.suala sio kutibiwa suala ni kuwa unatibiwa na nani ?

Huwezi kusema kuwa wanakidhi wakati idadi ya madaktari wa kike ni chache kuliko wa kiume na hii hupelekea munkari wa wanaume kuwatibu wanawake.

Na hii ya wanaume kuwatibu wanawake katika uislamu haifai kwa sababu hii ya mwanamke kuonwa tupu yake na daktari athari ni kubwa kuliko mwanamke kuchanganyika na wanaume.

Sasa ajabu unakubali dharura ya mwanamke kuwa chumbani na dokta akifunuliwa maungo,alafu hapo hapo unakataa mwanamke kukaa darasa moja na wanaume akiwa amejistiri anasoma udaktari ili aje kupunguza wanawake kutibiwa na wanaume ?


hasa ukiangalia mazingira si rafiki kwao hao wanawake na wasio kuwa wanawake.
Huwezi kusema mazingira ya wanawake sio rafiki alafu hapo hapo unakubali dharura ya mwanamke kukaa chumbani na dokta wa kiume akitibiwa na pengine kufuniliwa maungo,hili unasema dharura.

Madhara ya dokta wa kiume kukaa chumbani na mwanamke akimtibu na kuona maungo yake,hili lina madhara zaidi kwa sababu linakusanya mambo mawili.

1.mazingira ya ufalagha baina ya dokta na mgonjwa ambayo kisheria hayafai.

2.kuona maumbile ya mgonjwa wa kikeyasiyotakiwa kuonekana na mwanaume wa kando. hili pia halifai.

Sasa ukiangalia kusoma chuo mazingira yake hayazidi uhatari wa mazingira ya dokta na mgonjwa kwa sababu kwa docta huingia mmoja mmoja na chuo watu hukaa kwa vikundi zaidi.

Alafu pia kukaa faragha ndio hatari kuliko kuchanganyika kwa sababu faragha watu hubakwa na kuzini wakiwa peke yao.hili la ufaragha linapatikana kwenye utibuji ambao wewe unautia kwa jina la dharura.

Lakini pia kwenye mchanganyiko wa mavyuo hakuna kufunuana maungo baina ya mwanamke na mwanaume kama ambavyo dokta humfunua maungo binti chumbani.

Sasa kusoma mchanganyiko huwezi kusema mazingira yake sio rafiki wakati kule kwa daktari mazingira ndo sio rafiki zaidi.

Lakini ajabu huku unasema dharura,na huku unaharamisja wakati ambao hii dharura unayoidai itaendelea kuwepo kwa sababu ya wewe kukataza mchanganyiko ambao madhara yake sio makubwa ukilinganisha na madhara ya mgonjwa na daktari wa kike.

Sasa ukipima maslahi utaona kuwa kutibiwa na daktari wa kiume mwanamke ni jambo la hasara zaidi kuliko mwabamke huyu kusoma mchanganyiko.

Kwa sababu faragha baina ya mwanamke na mwanaume ina madhara makubwa zaidi ya mchanganyiko baina ya wanawake na wanaume.

Lakini pia mchanganyiko wa watu ni jambo gumu kuliepuka kwa sababu..

1.masokoni kuna michanganyiko.

2.kwenye madaladala kuna michanganyiko.

3.njiani kuna michanganyiko.

Hii michanganyiko uhatari wake ni mdogo kuliko ule mchanganyiko wa mgonjwa wa kike na daktari wakiwa peke yao chumbani.

Kwa hili huwezi kuwa na hoja ambao itaweza kushawishi haya madhara yakawa madogo na kule yawe makubwa.
 
Ama kufanya kazi katika maeneo yanayohusiana na wanaume, hilo halijuzu kwake kufanya hivyo; kwa namna ya kwamba inamlazimu yeye kuchanganyika na wanaume, na hiyo ni fitnah kubwa sana ambayo ni wajibu kujihadhari nayo.
Haya ni maneno ya mtu ambayo nimekuwa nikiyapinga tokea mwanzo kwamba hayana hoja ya kusapoti makatazo haya kwa sababu madhara ya mchanganyiko ni madogo kuliko madhara ya faragha ya daktari wa kiume na mgonjwa wa kike.

Watu hawa hawa wanaruhusu mwanamke kutibiwa faragha na mwanaume kwa kusema kuwa ni dharura,mbona kule kwenye mchanganyiko hawasemi ni dharura kama huku kutokana na mazingira ya Nchi zetu na sheria zake ?

Mchsnganyiko hauwezi kuzuia watu kusoma fani kama udaktari kwa sababu huu mchanganyiko unaofanya madaktari wa kike wapatikane unakuja kuondoa munkari mkubwa wa wanawake kutibiwa na wadaktari wa kiume.

Hivyo haina mantiki kuendelea kusema kuwa ati kutibiwa na mwanamke ni dharura wakati sisi wenyewe ndo tunazuia wanawake wasisome.

Sijaacha baada yangu fitnah yenye kudhuru wanaume zaidi kuliko (fitnah ya) wanawake, na kwamba baniy Israaiyl walifitiniwa na wanawake.”
Hii hadithi haikataliwi kuwa ni ipo,lakini usitake kutia maana yako hapa unayoitaka.

Hapo hadithi imetaja fitina ya wanawake kwa ujumla wake sasa wewe tia sherhe zako ambazo mtume wa Allah mwenyewe hakuziona.

Mwanamke ni fitina kubwa ndio maana sheria ya uislamu imekataza mwanamke kukaa faragha na mwanaume kama dokta wa kiume na mgonjwa wa kike.ila kwenu mnasema dharura.
Ni juu ya mwanamme kumuepusha Ahli wake (mkewe) na sehemu za fitnah na kumuepusha na sababu zake (sababu za fitnah) kwa kila hali." (Mwisho wa kunukuu).
Hakuna namna ya kunishawishi kuwa mchanganyiko pekee ni fitina kubwa bila kujali faragha ya watu wawili.

Siwezi kukubali kuwa ati mchanganyiko wa kwenye madisco ni sawa na ule mchanganyiko wa walimu wakiwa ofisini wametulia kila mmoja na pahala pake kwa ustaarabu kabisa.

Huwezi kuniambia kuwa mchanganyiko wa kwenye baa ni sawa na mchanganyiko ule wa shuleni,hili sio sawa sawa.

Michanganyiko yenye munkari ndani yake ndio yenye fitina zaidi katika mujitamaa.
Usalama uko humo.
Usalama ni kujizuia na machafu katika kila sehemu haijalishi ni mazingira gani.

La mwanzo kujizuia na uchafu katika hali yeyote itakayokuwa,huo ndo usalama wa kwanza.
 
Mambo ya dini yanaeleweka waachen wadada waje walete sababu kwanza huu mjadala unawahusu wadada 85% hzo zilizobaki 15% wanaume kwa kuleta challenge ili mada ishibe RUDINI KWENYE MADA au tuombe Moderator wapeleke uzi jukwaa la dini

Kiufupi sana umeeleweka Chief!

Japo maumbile yanaenda sambamba na Imani ambayo ina jumuisha changamoto za kidunia na muenendo wake!!

Chief Jurjani hebu toka nje ya box! Ingia dunia halisi zitambue changamoto then tumia ufahamu wako kuzitambua na kuzitatua!

Stop enforcing your beliefs on other people!!
 
Kiufupi sana umeeleweka Chief!

Japo maumbile yanaenda sambamba na Imani ambayo ina jumuisha changamoto za kidunia na muenendo wake!!

Chief Jurjani hebu toka nje ya box! Ingia dunia halisi zitambue changamoto then tumia ufahamu wako kuzitambua na kuzitatua!

Stop enforcing your beliefs on other people!!
Imeandikwa mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu pia mwanamke n sehemu ya ubavu wa mwanaume hvyo mwanamke yampasa kuwa mnyenyekevu na mtii kwa mumewe ila hii haina maana kama kuna ulaxima wa mwanamke kujishughulisha ukamzuia ila kama hamna ulazima mwanamke lea watoto wako mfariji mpe mawazo mema mumeo mjenge familia Bora ili ije iwe msaada kwenu baadae pindi mtakapo hitaji msaada wao pia nyumba ni Baba Mama na Watoto upendo kusikilizana ndio nguzo kuu ya familia tofauti na hapo ni nyumba kukosa muelekeo
 
Tunataka kusikia vitu toka moyoni kwa wanawake alafu kuna hawa jamaa wanabishana tuu mapeji kibao n Bora watafutane PM wabishane huko na hapa waache watu waseme ya moyoni mwao labda tuwaelewe kidogo yan mke wangu aende kikazi eti meeting two weeks halali kitandani labda tukifika huko kwenye 50+
 
Nanukuu....

" Mtazamo Linganishi Wa Kila Mmoja

• Mwanaume ni mtumwa wa matamanio yake; mwanamke ni mtumwa wa mapenzi.
• Mwanaume humpenda mwanamke aliyempenda, mwanamke humpenda mwanaume aliyeitambua thamani yake (ya mwanamke huyo) na kutamka upendo wake kwake.
• Mwanaume hutaka kummiliki mwanamke, mwanamke hutaka kuutawala moyo wa mwanaume.
• Mwanaume hutaka kumzidi nguvu madaraka mwanamke, mwanamke hutaka kupenya katika moyo wa mwanaume.
• Mwanaume hutaka kumteka mwanamke; mwanamke hutaka kutekwa. • Mwanamke hutaka mwanaume awe jasiri na shujaa na anayemjali, mwanaume hutaka mwanamke mwenye sura nzuri na mcheshi.
• Mwanamke hutaka ulinzi wa mwanaume, na huchukulia ulinzi huo kuwa ni kitu cha thamani zaidi anachoweza kukimiliki. Anaweza kuyadhibiti matamanio yake. Hisia za ngono za mwanaume ni kali na zenye nguvu za mwanamke ni baridi na zenye kusisimka. "(Mwisho wa kunukuu)
 
Tunataka kusikia vitu toka moyoni kwa wanawake alafu kuna hawa jamaa wanabishana tuu mapeji kibao n Bora watafutane PM wabishane huko na hapa waache watu waseme ya moyoni mwao labda tuwaelewe kidogo yan mke wangu aende kikazi eti meeting two weeks halali kitandani labda tukifika huko kwenye 50+
Mke yuko chini yako.

Unaweza kumruhusu ama kumkataza,na ni wajibu wake mke akusikilize wewe mumewe.
 
Kelele nyingi tukae majumbani haya mwisho wa mwezi huu sasa uje unilipie kodi, bili za maji na umeme uniwekee chakula kwenye fridge na unipe pesa ya matumizi yangu binafsi.
 
Kelele nyingi tukae majumbani haya mwisho wa mwezi huu sasa uje unilipie kodi, bili za maji na umeme uniwekee chakula kwenye fridge na unipe pesa ya matumizi yangu binafsi.
Kwa mke wangu hili ni wajibu wangu, wala hana haja ya kuuliza.
 
Imeandikwa mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu pia mwanamke n sehemu ya ubavu wa mwanaume hvyo mwanamke yampasa kuwa mnyenyekevu na mtii kwa mumewe ila hii haina maana kama kuna ulaxima wa mwanamke kujishughulisha ukamzuia ila kama hamna ulazima mwanamke lea watoto wako mfariji mpe mawazo mema mumeo mjenge familia Bora ili ije iwe msaada kwenu baadae pindi mtakapo hitaji msaada wao pia nyumba ni Baba Mama na Watoto upendo kusikilizana ndio nguzo kuu ya familia tofauti na hapo ni nyumba kukosa muelekeo

Chief
soma vizuri manake hakuna nukta wala koma! Ila nimekuelewa!!

Swali langu kwako;...kama Muumba wa vyote (mbingu na arshi’ (Universe) sio Ardhi ‘!)....angedhamiria yote haya kulikua na ulazima gani wa kuumbwa kwa “Mwanamke?!”

Msimamo wangu, Muumba wa vyote hakosei hata chembe!

Yeye ni mkamilifu na kiongozi Mtimilifu!

Hivi leo hii tunapata wapi Haki ya kutenganisha kati ya viumbe wake (Mume & Muke) katikati ya changamoto na vikwazo vilivyopo kwa ridhaa yake??

#HikiNdichoKipimoChaImaniYetuKwake!!!!
 
Tunataka kusikia vitu toka moyoni kwa wanawake alafu kuna hawa jamaa wanabishana tuu mapeji kibao n Bora watafutane PM wabishane huko na hapa waache watu waseme ya moyoni mwao labda tuwaelewe kidogo yan mke wangu aende kikazi eti meeting two weeks halali kitandani labda tukifika huko kwenye 50+

Chief, wewe unaweza kusafiri more than 7 days na kumwacha mkeo kitandani?
 
Kwa mke wangu hili ni wajibu wangu, wala hana haja ya kuuliza.

Lakini huyu siyo “Mkeo “ Chief!!

Vipi kuhusu jinsia ya kike kama yeye?? Hana Mume (mfano) hana ndugu wa “kumsitiri (mfano) “.....!?

Yeye (na jamii yake) wanaelekea wapi??
 
Kwa mke wangu hili ni wajibu wangu, wala hana haja ya kuuliza.
Usitoe hukumu kwa kumuangalia mke wako tu.

Yani kwa kuwa mkeo unamvisha na kumvalisha hujui kama kuna wimbi kubwa la wanawake ambao hawajaolewa na wengine hawana wazazi yatima wanasoma kwa shida.

Hawa wasipojishughulisha watakula wapi kama sio kuwa omba omba na kufa njaa tu.

Mwishowe mwanamke ambae anajishughulisha kupata riziki ni bora kwake kuliko mwanamke ombaomba ambae watu wanaweza kutumia nafasi hiyo kumlaghai na kumfanyia matendo maovu.

Lakini pia mtume kakataza tabia ya mtu kuwa ombaomba bora ajitafutie kuliko kukaa kila siku na kuomba.

Maana yake hata mwanamke haipendezi kwake kuwa omba omba bora akajitafutie mwenyewe kwa sababu akikaa ndani hawezi kupata chakula na kutimiza haja zake.

Hapa ndipo suala la kujishughulisha halikwepeki kwa mwanamke.

Ila kwa mkeo maadamu anahudumiwa na wewe basi unaona kuwa wanawake wote wanahudumiwa wakati wengi hawana waume na wanaishi katika mazingira magumu.
 
Lakini huyu siyo “Mkeo “ Chief!!

Vipi kuhusu jinsia ya kike kama yeye?? Hana Mume (mfano) hana ndugu wa “kumsitiri (mfano) “.....!?

Yeye (na jamii yake) wanaelekea wapi??
Jamaa anaona kuwa wanawake wpte wameolewa na wote hawana shida.
 
Lakini huyu siyo “Mkeo “ Chief!!

Vipi kuhusu jinsia ya kike kama yeye?? Hana Mume (mfano) hana ndugu wa “kumsitiri (mfano) “.....!?

Yeye (na jamii yake) wanaelekea wapi??
Hawa tuliwazungumzia huko mwanzo,baada ya binti fulani kuuliza swali kama hili.
 
Back
Top Bottom