Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Mambo ya dini yanaeleweka waachen wadada waje walete sababu kwanza huu mjadala unawahusu wadada 85% hzo zilizobaki 15% wanaume kwa kuleta challenge ili mada ishibe RUDINI KWENYE MADA au tuombe Moderator wapeleke uzi jukwaa la dini
 
Sijasema kuwa utumwa ni asili.angalia maneno yangu vizuri,sizungumzii utumwa kama utumwa,nazungumzia utumwa kwa watu maalumu.
Sasa kuna tofsuti kati ya kauli yako "asili ya waaftika huko.... " na hiki ulichokiandika hapa "sijasema utumwa ni asili" ?

Ili uone kwamba tamko lako ulipoliweka halikai pale, bali unalazimisha maana, na hili halipo.
 
Hiyo ni ada yako usilazimishe watu kuona hivyo.

Wapo watu hawaoni kuwa hiyo ni safari ya kusafiri bali hiyo ni safari ya kawaida tu ambayo kisheria sio ile ya kusafiri.

Lakini pia kama wewe unaona ni safari ya kusafiri basi haulazimishwi kuwa usione ni safari ya kusafiri,utafanya wewe kwa uoni wako yale ambayo yanaambatana na usafiri.

Ila usilazimishe mpaka sisi wengine ambao hatuoni kuwa hiyo ni safari ati tuone kuwa ni safari ile ya kusafiri.

Ukilazimisha hivi utakuwa unazidi kuchochea kuni ile tabia yako ya kutaka watu wote wafuate mtazamo wako jambo ambalo sio sahihi.

Safari ya mwanamke kutoka na mahrim ni ile ambayo mwanamke hutoka akihisabika kuwa amesafiri,yaani safari hiyo hadi mwanaume akitoka awe anahisabika kuwa amesafiri.
Sasa nalazimisha vipi wakati sisi Waswahili tuna jua hivyo ?

Naona unanizushia tabia ambayo sina, tena uzuri unabishana na ushahidi wa wazi. Sasa nani analazimisha safari iwe safari kwako, kwetu sisi tukisema safari unadai nalazimisha ? Kijana jenga hoja achana na tuhuma.
 
Ndo mana nakuambia kuwa safari ile ya mahrim ni ile safari ya KUSAFIRI na sio safari ya kwenda tu kama kutoka mbagala kwenda kawe.

Hii kutoka mbagala kwenda kawe huwezi kusema ni safari ya mwanamke kutoka na mahrim wake kwa sababu kwa ada ya watu wengi wa daressalam hii sio safari ya kusafiri ni safari ya kwenda tu umbali wa kawaida.

Unapotaka kujaalia kuwa kila safari ni ya kusafiri hili litadhihirisha tena kuwa namna gani dalili unaziweka pahala ambako sio pake.

Safari inafahamika ni ile ya kwamba ukienda watu wa mji huo wanahesabu kuwa umesafiri haswa.

Sasa mwanamke kutoka ndani kwenda kwenye mahitaji yake haihitaji mahrim kwa sababu hiyo sio safari ya kusafiri ,jambo hili unatakiwa ulitoe katika masharti,sio sawa ndugu unafanya ugumu mambo ambayo sheria haikuyazungumza.
Inauwaje unaandika mambo mengi yadiyo na msingi ?
 
udharura wa hilo unakuja kutokana na makatazo na fadhila alizo wekewa mwanamke akiwa nyumbani,
Makatazo unayadai wewe wala hujayaonesha katika aya ama hadithi.aya imeeleza kule kuwa watoke lakini wasitoke ile mitoko ya kijaahiliya,aya imeeleza wazi kabisa kuwa kutoka wanaruhusiwa.

Mafhum mukhaalafa inaonesha hivyo.

Aya iliposema wasitoke mtoko wa kijaahiliya ,mafhum mukhaalafa yake ni kuwa watoke kwa mtoko ambao sio wa kijaahiliya.

Sasa mpaka hapo aya haijasema kuwa watoke kwa dharura,aya inaonesha kuwa mpaka hapo watoke ila kwa mtoko usiokuwa wa kijaahiliya.

Miongoni mwa yale ambayo yalikuwa ya kijaahiliya ni yale ambayo yamekatazwa na Qurani

mfano kutoka hajajistiri
Kutoka kajipiga manukato
Kutoka na kupiga chini miguu
Kutoka na kulegeza sauti

Haya yaliyokatazwa kwa mwanamke ndio ambayo yalifanywa zama za ujaahiliya na ndio maana yakakatazwa bwana mkubwa.

Hata sheikh Abdallah saleh al farsiy ndio maana katika tafsiri yake chini akaweka maelezo haya..

"Wanaambiwa wakae majumbani mwao wasitoke ovyo ovyo,watoke kwa dharura na HAJA tu.ikiwa sio hivyo basi wajikalie majumbani mwao wachunge murua wao "

Hili la dharura na haja hulitaki unalitaka la haja tu.

Haja ni kama kwenda kwenye kibarua chake,kwenda kwenye darsa labda na mitoko mingine.

Kwako wewe haja hutaki hasa kuiskia.
kwa maana kuziacha fadhila hizo mpaka iwepo haja ya kufanya hivyo,
Haja zipo ndugu,au haja ziwe kwa mujibu wa unavyoona wewe ?

Mwanamke anaetoka kwenda kazini kutibu watu huyu anahaja ya kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili.

Kwanza atapata mshahara wa kukidhi mahitaji yake.hii huwezi kuitoa katika haja.

Pili atakuwa anawatibu watu hasa wanawake wenzie,hii ni haja kubwa jamii inahitajia hasa waislamu.huwezi kutoa haya mambo katika haja.

Kwa hiyo haja zipo na sio kuwa wanatoka tu kiholela kama ambavyo unataka kutuaminisha.


kwa maana kuziacha fadhila hizo mpaka iwepo haja ya kufanya hivyo
Lakini pia uislamu ni mpana sana hasa katika mlango wa fadhila.

Mwanamke tabibu anaweza kukosa fadhila za kukaa nyumbani lakini akienda hospitali akitibu watu kwa huruma na uchamungu basi pia hupata malipo tena.

Kwa hiyo anaweza akakosa malipo ya kukaa nyumbani na akapata malipo ya kutibu watu.

Anaweza kukosa malipo ya kukaa nyumbani akapata malipo ya kwenda kuwatembelea wazazi.

Anaweza kukosa malipo ya kukaa nyumbani na akapata malipo ya kuwalea watoto yatima.

Kwa hiyo usione na kufikiri kuwa fadhila za mwanamke zinapatikana kwa yeye kukaa nyumbani tu,anaweza kutoka na bado akapata fadhila tele.
na hiyo haja hukadiriwa kwa makadirio yake ya kukidhi vigezo. Hii ndiyo dharura.
Hayo makadirio ni yepi shekhe sio wasema tu makadirio makadirio.

Weka hayo makadirio ambayo yapo kwa mujibu wa sheria ya uislamu na sio kwa mujibu wa mtazamo wa shekhe fulani.

Weka hayo makadirio alafu tuyapime tuone tujadili kwa pamoja.
Alhaafidh Abubakr al Bazzar amesimulia hadithi toka kwa swahaba Anas Ibn Malik, ya kuwa kuna mwanamke alienda kwa mtume, na kumuleleza mtume ya kuwa wanaume wamepewa vitu vyenye kuwafanya wapate fadhila nyingi sana, kama vile kupigana jihadi na mfano wake, mtume akamwambia mwanamke yule ya kuwa "Mwanamke atakae tulizana nyumbani kwake miongoni mwenu basi huyo atalipwa ujira na yule mwanaume anae pigana jihadi.
Sawa hatukatai hilo lakini unatakiwa utambue kuwa huyo mwanamke alienda kuuliza masala ambayo moja kwa moja ni ibada kama vile jihaad n.k

Na sio masala ambayo sio ya kiibada moja kwa moja.

Uislamu umeweka yale ambayo khaaswa mwanaume awe mshiriki mkuu na yale ambayo mwanamke ni mshiriki mkuu katika MAMBO YA IBADA.

Sasa hizi kazi za kidunia sio mambo ya ibada ya moja kwa moja kwamba usialmu labda ulibainisha kwamba afanye mwanaume tu ama mwanamke tu.hapana.

Haya mambo ya kidunia hayatazamwi kwa ule muono wa kiibada moja kwa moja.

Na tambua kuwa hayakuepo hapo kabla hayo mambo ya kufundisha mashule na udaktari,hivyo lazima utumie uoni wa hali ya juu kutizama hilo.



Hii ni kutokana na fadhila nyingi apatazo mwanamke akitulizana nyumbani, ikapelekea ya kuwa jambo la kutoka kwake nje ni mpaka iwepo haja kubwa saa, na hii ndiyo dharura yenyewe sasa.
Unaposema haja kubwa sana unataka kuikuuza ili ugumu uzidi kwa mwanamke kutoka nje ya kwake.

Mwanamke anaweza kutoka kwenda dukani kununua kitunguu tu ambacho sio ishu sana katika mchuzi.

Hii huwezi kusema haja kubwa sana na wala huwezi kusema kuwa anapata madhambi ati kwa kuwa katika kwa haja isiyokuwa kubwa sana.sio.

Hiyo haja kuubwa unaiweka wewe mkuu.
Sasa kama anaweza kutoka kwenda kununua kitunguu vipi asiweze kutoka kwenda kutibu wanawake wenzie.

NB :mwanamke kulea familia ndio bora zaidi ikiwa baba ataplay part yake vizuri katika kuhudumia.na hili liko wazi kabisa.

Ninachokataa ni wewe kuharamisha kabisa juu ya mwanamke kufanya kazi.
Kadhalika mwanamke anapata fadhila kubwa akisalia nyumbani,
Ndio maana nikakuambia kuwa dharura hasa inakuwa asili yake kuwepesisha zito.

Mfano kula mchana wa ramadhani kwa mgonjwa kunamuwepesishia uzito wa kufunga.

Kusali rakaa mbili kwa msafiri kunamuwepesishia uzito wa kusali rakaa nne.

Kula nguruwe kwa mwenye njaa kunamuwepesishia uzito wa kukaa na njaa.

Kutibiwa mwanamke na dokta wa kiume kunamuwepesishia uzito wa yeye kukaa na maradhi.

Sasa kama mwanamke kusali msikitini ni dharura jee huyu kusali msikitini(dharura)kunamuwepesishia mwanamke na uzito upi ?

Uzito wa kusali nyumbani au kusali nyumbani kwake ndo wepesi ?
hii ni kuonyesha ya kuwa Mwanamke mahala pake ni nyumbani na kutoka kwake ni dharura, yaani kwa haja na si vinginevyo.
Kusali msikitini kwa mwanamke sio dharura kwa sababu haijatengua katazo lolote kwa mujibu wa sifa yako kuu ya dharura itengue katazo,na mwanamke kusali msikitini hakujakidhi yafuatayo ili iwe dharura.

1.hakujatengua katazo lolote ambalo lilikuepo mwanzo la mwanamke kutoruhusiwa kusali msikitini bali limeweka msisitizo kuwa wanaume hatutakiwi kuwakataza.

2.hakujawepesisha uzito wowote kama ilivyokuwa ada ya dharura.

Mfano mgonjwa anaweza kusali amekaa ili kuepuka uzito wa kusimama.

Sasa mwanamke anaweza kusali msikitini kwa kuepuka uzito wa wapi ?
 
Pinga kwa hoja na mifano ambayo nimetoa kuonesha tofauti hizo.sio unapinga kwa kusema wanachuoni wamesema wanachuoni wamesema hivi na vile,hiyo kwangu katika hili sio hoja
Sasa mifano yako unayoitoa ni mifano mfu na haikai.

Sasa unataka niseme wewe umesema nini au mimi nimesema ? Nacheka sana.

Wewe toa hoja usilete mambo huku huna marejeo zaidi ya akili yako finyu na maarifa machache, inapelekea mpaka kushindwa kutofautisha kati ya asili, ada na desturi.
Nimekupa mifano na wewe toa mifano kupinga hiyo yangu kuwa nilichosema sio sahihi,huku ndiko kujadili kuzuri,sio kwa hivi unavyomwenda.
Kwanza kutoa mifano si hoja, hoja ni kutoa maana ya kile ambacho mifano hufata kwake. Nilikupa maana ya asili na uhusiano wa ada na desturi. Hivi ndiyo vya msingi.
 
Inauwaje unaandika mambo mengi yadiyo na msingi ?
Kwa hiyo ukataa kuwa kuna safari ya kusafiri ambayo kisheria unaweza kupunguza sala.

Na safari ya kawaida ambayo huwezi kupunguza sala.

Mfano mtu kutoka mbagala kwenda kurasini kiada anaweza kusema anasafari ya kwenda kurasini.

Lakini kiada hiyo hiyo ni ngumu kusema kuwa ANASAFIRI kwa sababu sio kila safari ni kusafiri.

Au unakataa kuwa kuna safari ya kawaida na kuna safari ya kusafiri ?
 
Kwanza kutoa mifano si hoja, hoja ni kutoa maana ya kile ambacho mifano hufata kwake. Nilikupa maana ya asili na uhusiano wa ada na desturi. Hivi ndiyo vya msingi.
Pinga mifano yangu kwa mifano yako alafu tione kama kweli unachokisema kiko na usahihi ndani yake.

Hujatoa mifano ambayo itatufundisha utofauti huo,bila shaka hayo ni mambo yenye kuendana.
Wewe toa hoja usilete mambo huku huna marejeo zaidi ya akili yako finyu na maarifa machache,
Mimi kuwa na maarifa machache ndio sifa yangu binadamu,nyie ndio tunawaachia maarifa mengi.

Hakuna definition ya sesturi ama ada katika hadithi ama Qurani,definition tutazitoa katika akili zetu.

Bali katika qurani ama hadithi utakuta mfano wa ada ama desturi,kwa hiyo maana yeyote ile itakayokuwa basi ni jitihada za mtu tu.

Kwa hiyo lazima kuwe na mifano hai kama ambavyo nimekupatia.
 
Sasa nalazimisha vipi wakati sisi Waswahili tuna jua hivyo ?
Waswahili gani wakati wengi hawazingatii kuwa wanasafiri ?

Nina shemeji yangu anakaa magomeni anafanya kazi kibaha na wala hapunguzi sala kwa kuitakidi kuwa hiyo kwake sio safari,na anasema hasa "nina safari ya kwenda kibaha"
sasa huyu ni mzungu ?

Nina ndugu wapo mbagala wanafanya kazi kariakoo hawapunguzi sala kwa kuitakidi kuwa sio kusafiri na husema kuwa "wana safari ya kariakoo"

Hawa nao wazungu sio waswahili sio ?

Nina ndugu wapo kijitonyama wanafanya kazi posta na hawapunguzi sala wakiwa posta kwa kuitakidi kuwa hizo sio aafari.

Hawa nao wazungu sio waswahili ?
Kusema mtu anasafari sio kwamba amemaanisha anasafiri ndugu.

Inaonesha hili ni geni kwako,pengine ukisikia mtu anasema anasafari ya kwenda karume basi unadhani anamaanisha anasafiri ?

Hili jambo pengine ni geni kwako.

Safari ya kisheria ni ile ambayo kwa ada za watu ni kusafiri.

Ingekuwa safari ni safari tu basi wakazi wengi wa dar wasingefunga kwa sababu wapo wanaokaa mbagala wanafanya kazi posta hawa ingekuwa wana ufahamu kama wako wa kuw ahiyo ni safari basi wakiend kazini wasingefunga wangekula mchana.

Wapo wanaokaa mkuranga wanafanya kazi mbagala na wanafunga,wangekuwa na uswahili unaoudai wewe bila shaka wangekula mchana wakazi wengi wa mkuranga pale wanapoenda kazini kwa sababu wanasafiri.

Huo uswahili unao wewe na huo sio uswahili ni ufahamu ambao hauko katika usawa.

Mimi nikisema kuwa kuwa nina safari ya kwenda magomeni na hapo nipo mbagala kwa mujibu wa bwana zuri hii safari ni ya kupunguza sala,na ya kula mchana wa ramadhani.

Yani bwana mkubwa haya maajbau
 
Hii huwezi kusema haja kubwa sana na wala huwezi kusema kuwa anapata madhambi ati kwa kuwa katika kwa haja isiyokuwa kubwa sana.sio.

Hiyo haja kuubwa unaiweka wewe mkuu.
Sasa kama anaweza kutoka kwenda kununua kitunguu vipi asiweze kutoka kwenda kutibu wanawake wenzie.

NB :mwanamke kulea familia ndio bora zaidi ikiwa baba ataplay part yake vizuri katika kuhudumia.na hili liko wazi kabisa.

Ninachokataa ni wewe kuharamisha kabisa juu ya mwanamke kufanya kazi.
Naona una sahau mapema sana, huko awali nilikwambia Wanawake walikuwa wanatoka kwenda masokoni, wanatoka kwenda misikitini na wanatoka kwenda maharusini lakini katika maeneo ya karibu na majumbani mwao, hili liko wazi.

Hoja yako ya kusema mwanamke ni anahaja ya kutoka kwenda kutafuta pesa, na hii si katika yale mahitaji ya kila siku, sababu kazi huja kukidhi haja baada ya kupata ujira. Weka akilini hili ili usiendelee kurudia kitu ambacho kipo wazi tayari.

Pili, unaposema nimeharamisha mwanamke kutokufanya kazi kadhalika hii si kweli, sababu nilikuwekea kaida ya kiusuli nikamnukuu Imaam wa Usul shaykh Muhammad al Amini, na kuhitimisha ya kuwa jambo huwa haramu kwa kuangalia maslahi na faida, ikiwa faida ni chache kuliko madhara, jambo hilo linakuwa haramu na ikiwa madhara machache dhidi faida, jambo hilo linajuzu, na hii kaida asili yake ni katika aya ya kuharamisha pombe.
 
Waswahili gani wakati wengi hawazingatii kuwa wanasafiri ?

Nina shemeji yangu anakaa magomeni anafanya kazi kibaha na wala hapunguzi sala kwa kuitakidi kuwa hiyo kwake sio safari,na anasema hasa "nina safari ya kwenda kibaha"
sasa huyu ni mzungu ?

Nina ndugu wapo mbagala wanafanya kazi kariakoo hawapunguzi sala kwa kuitakidi kuwa sio kusafiri na husema kuwa "wana safari ya kariakoo"

Hawa nao wazungu sio waswahili sio ?

Nina ndugu wapo kijitonyama wanafanya kazi posta na hawapunguzi sala wakiwa posta kwa kuitakidi kuwa hizo sio aafari.

Hawa nao wazungu sio waswahili ?
Kusema mtu anasafari sio kwamba amemaanisha anasafiri ndugu.

Inaonesha hili ni geni kwako,pengine ukisikia mtu anasema anasafari ya kwenda karume basi unadhani anamaanisha anasafiri ?

Hili jambo pengine ni geni kwako.

Safari ya kisheria ni ile ambayo kwa ada za watu ni kusafiri.

Ingekuwa safari ni safari tu basi wakazi wengi wa dar wasingefunga kwa sababu wapo wanaokaa mbagala wanafanya kazi posta hawa ingekuwa wana ufahamu kama wako wa kuw ahiyo ni safari basi wakiend kazini wasingefunga wangekula mchana.

Wapo wanaokaa mkuranga wanafanya kazi mbagala na wanafunga,wangekuwa na uswahili unaoudai wewe bila shaka wangekula mchana wakazi wengi wa mkuranga pale wanapoenda kazini kwa sababu wanasafiri.

Huo uswahili unao wewe na huo sio uswahili ni ufahamu ambao hauko katika usawa.

Mimi nikisema kuwa kuwa nina safari ya kwenda magomeni na hapo nipo mbagala kwa mujibu wa bwana zuri hii safari ni ya kupunguza sala,na ya kula mchana wa ramadhani.

Yani bwana mkubwa haya maajbau
Sisi tulio wengi tukiingia Kibaha tunapunguza sala.
 
Hakuna aliyesema kusoma secular ni haramu, bali wanazuoni wetu wamefika mbali wakasema kama kuna sehemu kuna haja ya mtu kuwa na taaluma ya utabibu au uhandisi au mfano wake katika elimu za mazingira, na watu wa eneo wasisome elimu hiyo, watu hao hupata madhambi.
Sasa hapa hiyo ni faradhi kifaaya ambayo wakisoma wachache wengine haitawalazimu.

Ama ikiwa hakuna ambao wamesoma hiyo elimu hapo itakuwa faradhi ayni kwa kila mtu,wakisoma wachache tu wengine kwao sio wajibu.

Sasa kupatikana kwa wachache waliosoma hiyo fani na kuwaondokea dhima wengine sio hoja ya kuwa hawa wengine ambao wameodhokewa dhima ati kuwa haifai kwao kusoma.

Watasoma ila sio wajibu kwao kwamba wakiacha watapata dhambi.hili mbona liko.wazi.

Au inakuwa haramu kwa wengine..?
 
Mwanamke tabibu anaweza kukosa fadhila za kukaa nyumbani lakini akienda hospitali akitibu watu kwa huruma na uchamungu basi pia hupata malipo tena.
Sasa kama unajua hilo, vipi useme haya mambo si ya kiibada. ? Kuna ibada isiyo na fadhila yaani malipo ?

Kama unakumbuka huko awali kuna swali nilikuuliza, ni ipi nafasi ya nia katika jambo ?

Embu niambie kutibu watu kwa huruma na uchamungu ndiyo kukoje huko ? Je anakuwa katika mipaka ya Allah au anakuwaje ?
 
Sasa hapa hiyo ni faradhi kifaaya ambayo wakisoma wachache wengine haitawalazimu.

Ama ikiwa hakuna ambao wamesoma hiyo elimu hapo itakuwa faradhi ayni kwa kila mtu,wakisoma wachache tu wengine kwao sio wajibu.

Sasa kupatikana kwa wachache waliosoma hiyo fani na kuwaondokea dhima wengine sio hoja ya kuwa hawa wengine ambao wameodhokewa dhima ati kuwa haifai kwao kusoma.

Watasoma ila sio wajibu kwao kwamba wakiacha watapata dhambi.hili mbona liko.wazi.

Au inakuwa haramu kwa wengine..?
Sasa ndiyo uone hakuna haja ya wao kusoma udaktari kwa sasa sababu hao waliosoma wanakidhi hilo, na watu wanatibiwa, hasa ukiangalia mazingira si rafiki kwao hao wanawake na wasio kuwa wanawake.
 
Basi hiyo ni juu yenu usiwatie wengine katika hukumu hiyo.
Ilikuwsje sasa wewe ukatuweka sisi katika hukumu yenu ?

Turudi katika hoja ya msingi, mwanamke kutoka kwenda kufanya kazi, na usilete ubakaji wa neno hitaji na kufanya kazi kwa kulihusisha na mahitaji.
 
Makatazo unayadai wewe wala hujayaonesha katika aya ama hadithi.aya imeeleza kule kuwa watoke lakini wasitoke ile mitoko ya kijaahiliya,aya imeeleza wazi kabisa kuwa kutoka wanaruhusiwa.
Aya imeonyesha ya kuwa ikitokea katika hiyo haja, basi wasitoke kwa mitoko ya kijahiliya, tako hili jahiliya limekuja kwa maana zaidi ya mbili na tamko "qarni" kadhalika.

Sababu mtume alifasiri aya, na utendaji kazi wa aya ulifanyika zama za mtume.
 
Mafhum mukhaalafa inaonesha hivyo.
Hapa naona umegusia suala la Mufhuum, al Mukhalafah, suala hili hutakiwi kuliingia kichwa kichwa, sababu ndani yake kuna khilafu, mahanafi wanapinga suala hili, kwa hoja ya kuwa lazima iwepo dalili ya kuonyesha maana hiyo ya kinyume, na hapa wewe huna dalili hiyo ya kuwa kinyume chake ni Wanawake watoke. Kwahiyi hapo sababu aya imeshaeleza na jahaliya inajulikana na "qarni" inajulikana, hukupaswa kupoteza muda katika hili, zaidi ya kurejea aya kwa ukamilifu, na aya aya haikuonyesha mwanamke atoke kwenda kutafuta hela, sababu athari zimenukuliwa kwa wingi mwanamke alitoka katika mambo fulani. Sasa ndiyo maana suala la mwanamke kutoka kwenda kwenye kutafuta ugali bado suala ni la dharura, na ndiyo maana Ulamaa wamelikadiria kwa kurejea misingi ya aya na hadithi.

Kadhalika watu wa madhehebu ya Shafi, wana mapito yao juu ya hili.
 
Usalama wa nini ?

Anasema shaykh :

"Ama kufanya kazi katika maeneo yanayohusiana na wanaume, hilo halijuzu kwake kufanya hivyo; kwa namna ya kwamba inamlazimu yeye kuchanganyika na wanaume, na hiyo ni fitnah kubwa sana ambayo ni wajibu kujihadhari nayo.
Na inapasa ijulikane kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimwendee katika yale yaliyothibiti kutoka kwake kwamba alisema:

“Sijaacha baada yangu fitnah yenye kudhuru wanaume zaidi kuliko (fitnah ya) wanawake, na kwamba baniy Israaiyl walifitiniwa na wanawake.”

[Hadiyth ya kutoka kwa Usaamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) iliyopo katika Al-Bukhaariy na Muslim]

Ni juu ya mwanamme kumuepusha Ahli wake (mkewe) na sehemu za fitnah na kumuepusha na sababu zake (sababu za fitnah) kwa kila hali." (Mwisho wa kunukuu).

Usalama uko humo.
 
Back
Top Bottom