Umeona ulivyokuwa msahaulifu, ulipo niuliza swali la mwanamke harusiwi kutoka ila kwa dharura, au bila mahrim wake ulikuwa una dalili ya kupinga hili ?
Hakuna sehemu ama ushahidi umetoa unaosema kuwa kwa dharura hakuna ushahidi ulioweka hapa.
Kusema kwa dharura ni maoni yako ambayo hayana nafasi katika mambo ya sheria.
Ama uliweka hiyo aya ambayo imesema isipokuwa kwa dharura ?
Kumbuka hapa unatoa hukumu lazima uwe na hoja za wazi ambazo hazina uficho kabisa.
Nimecheka sana, hukumu ya safari inapimwaje mzee ?
Safari ni kwa mujibu wa ada za watu.
Kutoka dar kwenda mkuranga kwa ada za watu wengi hiyo sio safari ni matembezi ya kawaida tu.
Kutoka kimara kwenda kibaha kwa ada za watu wengi wa daressalam hiyo sio safari hayo ni matembezi ya kawaida tu.
Sasa kama wewe unaona safari hiyo ni juu yako usiwatie na ambao wanaona ni kawaida tu.
Hukumu ya safari hukadiriwa kwa kuzingatia ada na desturi, hataka kutoka kimara mpaka kibaha, hii ni safari kijana
Hii ni kwa mtazamo wako bwana,watu wengi hawaoni kuwa hiyo ni safari,wapo kama wewe mtaona kuwa ni safari lakini wapo ambao wanaona kuwa sio safari.
Ukisema dar to zanzibar kidogo nitakubali kuwa watu wengi wanaona kuwa ni safari ama dar to morogoro naam.
Sasa hilo la safari litabaki kwa watu wenyewe na bila shaka lazima watu wawe na maoni tofauti tofauti.
kijana,kwahiyo bado huna hoja ya kusema hadithi haipo.
Mbona nilikuambia kuwa hadithi hiyo ya mahrim iko wazi kabisa haina utata,alafh wewe unaniambia sina hoja ya kusema kuwa hadithi haipo ?
Kwani wapi nimesema haipo bwana mkubwa ?
Ninachokuambia ni kuwa kilichokatazwa mwanamke kutoka bila mahrim yake ni pale ambako anakuwa anasafiri.
Safari ambayo wao wenyewe watu wa mji wataizingatia kuwa ni safari ileee ya kupunguza sala hasa.
Huwezi kulazimisha mtu katoka kijitonyama kwenda ilala kutibu watu ukalazimisha atoke na mahrim wakati wao hawaitakidi kuwa kama hii ni safari.
Unataka utafute hoja zingine za kukusapoti ili tu uharamishe mwanamke kutoka nje,sasa hivi umekuja na hoja ya safari ?
Wapi tumegusia safari katika mada yetu ?
Au wewe mwenzetu mwanamke akitoka tu basi unahesabia kuwa lazima awe na mahrim na unaona kuwa ni safari ?
Tuende kwa umakini ndugu sio unaweza vitu ambavyo havihusiki.
Ndio maana nikakuambia kuwa tatizo sio kuweka dalili,tatizo unaweka dalili sehemu ambapo sipo yani unazifosi.
Sasa hapa umeweka hadithi ya safari wakati ambapo hapa hatuzungumzii safari tunazungumzia kutoka kwa kawaida mwanamke akiwa katika mipaka ya ndani ya mji wake.