Dalili niiweke mara ngapi ? Embu niambie niiweke mara ngapu, ili uione ?
dalili ya kuwa mwanamke hawezi kutoka pasi na maharim,mwanamke hawezi kutoka ila kwa dharura...
Hujatoa dalili ambazo zimeashiria kuwa mwanamke atoke kwa dharura hujatoa aya wala hadithi ikitaja hilo.
Unachoweka wewe ni maneno yasiyokuwa Qurani kusapoti msimamo wako bwana mkubwa.
Kumbuka kuwa hujaweza hoja yeyote ambayo inamkataza mwanamke kutoka kwenda kwenye mahitaji yake,hujatoa dalili.
Aya iliyonukuu haikatazi mwanamke kutoka kwenda kwenye mahitaji yake mbalimbali bali inamkataza kutoka ovyo ovyo.
Unatumia maandiko vibaya..
Mfano wa aya hizo zipo nyingi tu mfano..
Allah kasema "wala msipelelezane..."
Aya hii huwezi kuitumia kuwa ni katazo la kumchunguza ama kumpeleleza mchumba ambaye unataka kumuoa ati kwa kuwa aya imesema hivyo.
Pakitokea haja ya kuchunguza basi inafaa kuchunguza.
Kama ambavyo ikitokea haja ya mwanamke kutoka nje ya njumba itafaa kutoka.
Kutumia himizo la kukaa ndani kuwa ndo dalili ya kuwa haifai kutoka katika mahitaji yake ya kila siku huo ni ufahamu wa mbali sana.
Kwa hiyo mpaka hapo huwezi kutumia aya hii kumkataza mwanamke kutoka kwani mfano wa haya hizo zipo nyingi sana ambazo hazikatazi kinyume chake penye haja.