Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Hii ndiyo dharura sasa mzee.
Sasa unadhani dharura ya mwanamke kutibiwa na mwanaume kwa zama hizi itaondoka bila kuruhusu wanawake wasome zaidi wakae katika fani hizo ?

Kwa hiyo dharura hii ya mwanamke kutibiwa na mwanaume ambayo dharura hii ipo kila siku unaikubali na inatokea kila siku,lakini dharura ile ya mwanamke kwenda kusomea udaktari kila siku unaikataa kwa kigezo cha kuwa dharura hukadiriwa kwa makadirio.

Mbona mwanamke kutibiwa na mwanaume unaona ni dharura lakini kiuhalisia ni jambo la kawaida linalotokea kila siku ?

Unaposema dharura hukadiriwa kwa makadirio una maana gani ewe mja wa Mola ?
 
Hatuutuhumu usalafi tunawatuhumu masalafi.

Kama ambavyo hatuutuhumu uislamu bali tunawatuhumu waislamu.

Kuwa makini na wanayoyasema watu.
Na ndiyo maana nikakwambia kutokea kwa migongano katika safu ya maswali ni Allah anataka kutuoyesha ni katika wakweli katika da'wa, na hili lipo sababu Allah lazima atupime. Na hapo nimewazungumzia masalafi sababu huwezi kuwaongelea Masalafi bila kuuongelea Usalafi.

Sasa umakini ulitakiwa uwe nao wewe, kwa kuandika mambo ambayo hayana haja.
 
Wewe uko serious mkuu ?

Wako wengi sana.

Nakupa mfano kuna hospitali moja siitaji jina kuna wamama kibao tu wanatibu wako salama na dini yao.

Wapo wengi tu wana dini na wamesoma udaktari wewe unasemaje na nawajua kwa majina ?

Alafu kwani mbona kuna wanaume ambao wanasoma udaktari na hawajasalimika na dini yao kwa hiyo hii tuwakataze na wanaume kusomea udaktari kwa kuwa kuna baadhi hawapo salama na dini yao ?
Acha manebo mengi mzee, sisi tunaishi nao kijaa, na utuambie wamesalimika vipi na dini zao, maana usione Dini ni stara na kusali pekee.

Sasa leta shuhuda usipoteze muda
 
Pakiwa na migongano basi ina maana nyie kwa nyie kuna mmoja anamuona mwenzake yuko katika haki na mwingine yupo katika batili ndio maana mnagongana ati.
Migongano ya Kisalafi ni fitna, mathalani kuna fitna kipindi hiki ina vugu vugu, imeitwa fitna hiyo "Musa'afiqa" ukiifatitilia fitna hii imejengeka katika msingi wa husda,kutaka ukubwa na kuwazushia waislamu uongo. Kadhalika fitna nyingine zilizo pita.

Kwahiyo hiyo ndiyo maana ya migongano, mwingine lazima awe kwenye haki.
Kama wote mnajiona mpo katika haki mbona sasa yatokee magomvi baina yetu kwa yenu nyie.

Hapa hatusemi usalafi tunawasema wanaofuata huo usalafi wana matatizo wengi katika wao kwa sababu kama alizotaja huyo shekhe rabee.
Ongeza umakini, nimekwambia Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe mzee, katika jambo lolote la haki, mitihani lazima iwepo na huu ndiyo mwenendo wa Allah kwa waja wake, ili awaone waliothibiti katika hiyo haki na kuendelea kusafisha.
 
Katika hadithi ama aya gani inayosema kuwa kutafuta hela ni jambo letu sisi ?

Umesahau yule mkewe bwana mtume ambae alikuwa ni mfanya biashara mzuri tu katika maisha yake na Mtume pia akashiriki katika bishara hiyo ?

Wapi mtume alikemea utaratibu huo wa mwanamke kujitafutia katika vile vya halali ?
Nilikwambia huko mwanzo ya kuwa kuhoji hoji sana mpaka unahoji mambo ya kijinga, ambayo laiti ungesoma niliyo yaandika huko juu, usinge hoji.

Kiasili tunaotakiwa kutoka na kutafuta ni wanaume, na kwa wanawake hili linakuwa ni jambo la dharura, soma mafhumu ya aya ya 33 sura ya 33. Wanawake wamelazimishwa wakae majumbani sababu majumbani ndiyo salama yao, na kama wakitoka wasitoke mitoko ya Jahiliya, na ndiyo mitoko ambayo wanawake wa leo wanatoka.

Mke wa mtume mama Khadija baada ya kuolewa na mtume, kutafuta kwake mali kulikuwa chini ya mtume, na hivi ndivyo inatakiwa iwe, kwa mwanamke aliyejaaliwa mali aidha kwa urithi au mfano wake, inapo ondoka haja ya kufanya biashara zake anatakiwa ampe mtu azisimamie.

Uislamu unaruhus mwanamke kumiliki mali na kufanya biashara, na wapo wanao miliko mali katika Wanawake na wafanya biashara, ila biashara zao zinafanyika katika sheria na mipaka ya Uislamu, ila si katika mtindo ambao wanawake wa leo wanataka. Mwanamke shughuli zake zote anatakiwa azifanye katika mazingira ya nyumbani kwake, hii ni kwa sababu ya yale majukumu yake ya usimamizi wa nyumba.
 
Hivyo vigezo kaviweka nani zaidi ya Allah na mtume wake ?

Na ni vipi hivyo ?
Qur'aan na Hadithi mara nyingi mara nyingi huwa vinaelezea mambo kwa ujumla wake. Yaani hutoa misingi, kisha matawi huja kutolewa na wannazuoni kwa kurejea misingi hiyo kama ushahidi. Mifano iko mingi sana. Mathalani aya ya 33 katika sura ya 33,huu ndiyo msingi, na aya nyingine katika sura ya pili aya ya 165 au 195,kwa kumbukumbu zangu, na aya ziko nyingi na hadithi ziko nyingi. Mfano mwepesi leo hii hakuna hadithi wala aya inayosema bangi ni haramu, lakini kwa mujibu wa sheria ya Uislamu bangi ni haramu, sababu katika bangi kuna "Ila" na katika usul al Fiqh, kuna kitu kinaitwa Qiyas, kina tumika kutoa hukumu ya jambo hilo.

Wanazuoni wetu baada ya kusoma nususi na kuzielewa kutokana na nususi hizo wakatubainishia vigezo hivyo, na vyote vina marejeo. Mathalani mwanamke hatakiwi atoke kwenda safari yoyote bila Mahram wake, hii ni sheria. Stara hakuna dharura ya kupunguza stara mzee, kama ilivyo hakuna dharura ya kuzini, yaani mtu uzini halafu useme ni dharura. Kigezo kingine, pasipatikane michanganyiko, angalia kipindi cha mtume utaratibu ulivyo kuwa ili kuepukana na michanganyiko hiyo msikitini, utaratibu ulikuwa kuanzia kwenye safu, safu bora ya wanawake ni ile ya nyuma, lakini ilikuwa wakiwa msikitini muda wa kutoka msikitini huanza kwanza wanawake na kulikuwa na mlango maalamu, mpaka kuna swahaba baada ya kujua mlango fulani ni wa Wanawake, akaacha kuutumia mlango hata kama wanawake walikuwa hawapo msikitini. Sasa hili ni msikitini nje ya msikitini jambo hili awla zaidi.
Alafu kama unakubali kuwa hata wanaume yanawahusu yale ambayo wanawake yanawahusu katika mada hii mbona unamlenga mwanamke tu wakati huo mwanamke naye akienda nje atakutana na mwanaume ambaye wewe unaona haina shida kukutana na mwanamke..?
Nilikukanya huko juu, kuhoji sana mpaka unahoji mambo ya kijinga ambayo ni mepesi mno.

Hapa tunamlenga mwanamke sababu asili ya mwanamke ni kukaa nyumbani na si kutoka, ndiyo maana kutoka kwa mwanamke ni habar ila kutoka kwetu sisi ni wajibu.

Mwanamke kutibiwa na Mwanaume hii ni dharura, ila mwanamke kumtoa na kumpeleka nje ni uharibifu zaidi hasa akiwa na familia, adha za kazi ziajulikana, lazima uchague moja mzee, na tuna msemo wetu tunasema huwezi kutumikia mabwana wawili.

Tunamzungumzia mwanamke sababu nafasi yake ni kubwa sana na isiyokuwa na mfano katika kujenga familia na hatimaye jamii imara, unapo mtoa mwanamke huyu katika nafasi yake ujue umeiharibu jamii.

Sasa kipi bora, mwanamke akatibiwa na akabaki na dini yake, na mwanamke akawa tabibi, akatibu na akatabiwa na akapoteza dini yake ?
 
Wasipotafuta pesa watafanya Nini za Zaid ,wakati ukrsto unakubali ndoa na mke mmoja
 
Asili gani unayoisema wewe na umeshabainishiwa huko juu kuwa hata mkewe mtume alikuwa mfanya biashara na wanawake wa zama hizo walikuwa wengi wakitengeza mapambo na kuuza,walikuwa wanafanyia biashara majumbani ?

Asili gani inayokeukwa ?
Vijana mnachekesha sana aliyejibu swali la mkewe mtume alikuwa anafanya vipi biashara zake baada ya kuolewa. Asili ni mwanamke kukaa nyumbani. Hili nalirudia zaidi ya mara mbili sasa, sasa usiulize tena swali kama hiki.
 
Jambo ambalo ni mubaaha wewe unayekataza ndo utoe dalili.

Tokea hapo nimekuambia kusomea fani mbali mbali zaelimu isiyokuwa ya Allah na Mtume ni jambo la mubaaha.

Na mubaaha inajuzu mpaka dalili ya kukataza ije.
Unayo dalili ya kukataza mwanamke kusoma fani hizo ?

Unaposema mwanamke atoke kwa dharura ambayo hukadiriwa kwa makadirio na kwa haja.

Kwani mwa amke kwenda kazini kutafuta hela sio haja ambayo anahitajia kutimizamajukumu yake ya ndani ?

Au haja ya mwanamke kutoka ambayo hawezi kuifanya mwingine ni ipi ili tuone kuwa haja hizo kumbe mwanamke lazima atoke bila yeye hafanyi mwingine ?
Dalili nilikupa, aya nikakupa kaida ya kiusuli ya kuonyesha hali kadhaa juu ya ufanyaji mambo na kuwa haramu kwake, kwa kuanzia katika ile kaida uliyoitoa ya kuwa kila jambo kiasili ni lenye kufaa, kutokea hapa Wanazuoni wakazama na kutoa uchambuzi wa hali tatu,kwa kurejea katika hadithi na aya zenye mafhumu ya katazo la watu kuzidhuru nafsi zao.

Kwa haraka haraka, msingi na marejeo ni ya haya hapa :


قال الله تعالى : ( وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ) البقرة /195.
وقال الله تعالى : ( وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ) النساء /29.
وعَنْ أبي سَعيدٍ الخُدريِّ - رضي الله عنه - : أنَّ النَّبيَّ - صلى الله عليه وسلم - ، قالَ : ( لا ضَرَرَ ولا ضِرارَ ) رواه الحاكم (2 / 57 - 58) وقال صحيح الإسناد على شرط مسلم ، وصححه الألباني في " سلسلة الأحاديث الصحيحة " (1 / 498) .
 
Dalili nilikupa, aya nikakupa kaida ya kiusuli ya kuonyesha hali kadhaa juu ya ufanyaji mambo na kuwa haramu kwake,
Tatizo sio kutoa aya,tatizo kutoa aya ambazo haziendani na mambo unayoharamisha.
Hakuna aya umetoa ikajibu swala langu kwa sababu unaulizwa kingine unaenda kwingine.
kwa kuanzia katika ile kaida uliyoitoa ya kuwa kila jambo kiasili ni lenye kufaa, kutokea hapa Wanazuoni wakazama na kutoa uchambuzi wa hali tatu,kwa kurejea katika hadithi na aya zenye mafhumu ya katazo la watu kuzidhuru nafsi zao.
Kaida hii ya kuwa kila jambo kiasili ni lenye kufaa tulikubaliana kuwa kweli ipo.Unachoshindwa kuelewa ni kuwa hii kaida inajengeka katika mambo mawili.

KUHUSU KITU CHENYEWE.

1.kuna asili ya kile kitu chenyewe kuwa kinadhuru kwa kila mtu.

Mfano moshi wa sigara unadhuru kwa kila mtu,au sumu ya panya inadhuru kwa kila mtu.

Haya yenye kudhuru kwa kila mtu moja kwa moja ni haramu kuyafanya kwa kila mmoja kwa kule kuenea madhara yake kwa kila mtu.

Au kusomea kuroga,huku kusomea bila shaka kunakatazwa kusomea uchawi kwa kila mtu kwa sababu kuroga kuna madhara kwa watu wote.

2.Asili ya kitu chenye kudhuru kulingana na mtu mwenyewe na hakimdhuru kila mtu.

Mfano kuna watu wakila nyama ya bata wanadhurika,hapa nyama ya bata itakuwa haramu kwa huyu anayedhurika tu na wala haifai kwake kuwadhuru wengine ambao hawadhuriki na nyama hiyo ya bata.

Sasa hapa ile "hakuna kudhuru wala kujidhuru" inakuwa kwako wewe inayokudhuru na wala haifai kuharamisha kitu hicho kwa wengine wote ati kwa kuwa kuna baadhi kina wadhuru.

Hapo ilikuwa ni kile kitu chenyewe bila kuangalia njia inayotumia kukipata kama ina utata ama haina utata.

Sasa kusomea udaktari mwanamke kwa kuangalia ile fani yenyewe ya udaktari inamdhuru nini mwanamke katika nafsi yake ?

Mpaka Hapa nakuuliza tuu ile fani yenyewe ina madhara gani kwa mwanamke ?


قال الله تعالى : ( وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ) البقرة /195.
وقال الله تعالى : ( وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ) النساء /2
Hizi aya unazotoa zinawahusu wanawake na wanaume pia.

Ikiwa unafanya marejeo haya kuwa ndio hoja zako basi nijibu hapa kuwa.

je mwanaume anaruhusiwa kuiuwa nafsi yake katika kusomea hizo fani ila mwanamke haruhusiwi ?

Mwanaume anaruhusiwa kujiingiza katika maangamivu ila mwanamke haruhusiwi ?


لا ضَرَرَ ولا ضِرارَ
Hii hadithi inawahusu wanawake tu mzee ?

Mbona unawapa udhuru wanaume wasiingie katika hadithi hii ambayo wewe unaona kuwa ni marejeo ?

Ikiwa marejeo unayotoa yanawahusu wanawake na wanaume,sasa yako wapi marejeo ambayo yanamtoa mwanaume katika uharamu huo ambao mwanamke pia anaharamishiwa ?

Kama kweli kilichokusudiwa katika marejeo yako ni madhara yapatikanayokatika njia au mazingira ya kupata hiko kitu basi naomba nikuulize mkuu..

Jee hayo madhara ya hayo mazingira mbona yanawakuta wanaume pia na wewe unaona inafaa bila kuwa na dalili yeyote inayoruhusu mwanaume kuingia katika madhara hayo ?
 
Vijana mnachekesha sana aliyejibu swali la mkewe mtume alikuwa anafanya vipi biashara zake baada ya kuolewa. Asili ni mwanamke kukaa nyumbani. Hili nalirudia zaidi ya mara mbili sasa, sasa usiulize tena swali kama hiki.
Hakuna anayekataa asili hiyo,lakini haifidishi kuwa haruhusiwi kutoka kwa haja zake binafsi.

Asili kukaa nyumbani ila je akienda kazini kwa ajili ya kupata kipato halali akimaliza akalazimiana na nyumba yake asili iko palepale,tofauti na mwanaume akitoka kazini aenda vijiweni na sehemu zingine.

Ukisikia asili kukaa nyumbani unadhani ni kuwa haruhusiwi kutoka kwa namna yeyote ile ?

Mtume alikataza mwanamke kutoka nyumbani kwake hali kajipulizia manukato.
Kwa maana ATOKE akiwa hajajipulizia manukato yeyote.

Sasa ikiwa mtume anatambua kuwa mwanamke anaweza akatoka lakini kwa sharti ya kuwa asijipulizie manukato wewe ndugu una darja ipi kumzidi Mtume wa Allah ?

Hakuna hadithi yeyote ambayo Mtume alikataza wanawake kutoka majumbani mwao kuziendea haja zao za kimaisha,na wala haikuthibitipo kuwa Mtume aliwafukuza wanawake katika miji warudi majumbani mwao.

Hata aya zinaashiria kuwa mwanamke anaweza kutoka nyumbani.

Ndio maana kuna makatazo ama miiko ambayo mwanamke anatakiwa aizingatie pindipo anapotoka nyumbani.

Angalia aya hii..

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

[ AN - NUR - 31 ]
Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.

Ukiangalia kipengele cha kuwa

"Wala wasipige chini miguu yao..."

Mafhumu yanafahamika kuwa huo muongozo ni pale ambapo akiwa anatembea asipige chini moguu kwa mfumo wa maringo huko njiani asitamanishe.

Sasa hii aya haijamkataza mwanamke kutoka nyumbani kwenda katika haja zake,ila tu memuelekeza atembee vipi akiwa anaenda katika haja zake

Kwa nini wewe unakataza mwanamke kutoka kuelekea katika haja zake kwa kigezo cha kuwa ati asili yake ni ndani tu ?

Kuwa asili yake ni ndani tu ndo hoja kuwa asitoke nje ?
 
Tatizo sio kutoa aya,tatizo kutoa aya ambazo haziendani na mambo unayoharamisha.
Hakuna aya umetoa ikajibu swala langu kwa sababu unaulizwa kingine unaenda kwingine.
Siyo kwali, sababu hoja yako inaonyesha kuwaingiza na Wanaume. Sasa nilikukanya huko nyuma ya kuwa, hakuna baya ambalo ni baya tu kwa mwanaume na mwanamke asiingie, mpaka libainishwe.
 
Siyo kwali, sababu hoja yako inaonyesha kuwaingiza na Wanaume
Nawaingiza na wanaume kwa sababu ndio asili ya mambo yalivyo,huwezi kuwatoa wanaume kwenye mambo ambayo unamharamishia mwanamke bila dalili yeyote.

Kama kuchanganyika ni haramu kwa nini iwe haramu kwa mwanaume wakati madhara ya kuchanganyika yanawakuta wote kama tulivyokubaliana ?

Kwa hiyo lazima na wanaume niwaingize kwa sababu ndio utaratibu.


Sasa nilikukanya huko nyuma ya kuwa, hakuna baya ambalo ni baya tu kwa mwanaume na mwanamke asiingie, mpaka libainishwe.
Sasa kama unafahamu hivi kwanini unashindwa kuweka dalili ambayo imebainisha kuwa mwanaume anaruhusiwa kuchanganyika kusoma fani kuchanganyika ambako mwanamke haruhusiwi?

Mbona ubainisho wa kuwa mwanaume anaruhusiwa kufanya haramu ambazo mwanamke haruhusiwi hukutoa ubainisho huo ?

Bali mpaka sasa hujaleta uthibitisho unaomkataza mwanamke kutoka katika nyumba yake kwenda kutimiza mahitaji yake.

Bali aya zinaonesha kuwa mwanamke anaweza kutoaka kwenda kwenye mahitaji.

Na ile surat nnuur aya ya 3q ikasema..

"Wasipige chini miguu yao.."

Hapa maana yake wanapotembea,sasa kama uislamu ingekuwa unambana mwanamke mpaka kutembea kwa nini ikampa miiko ya kuwa akitembea atembee kwa aina fulani ?

Uhalisia ni kuwa mwanamke anaruhusiwa kutoka nyumbani kuziendea shida zake za kimaisha kama ambavyo aya zinaashiria hivyo.

Kama wewe unasema kinyume na asili ni haramu kwa hiyo mwanaume kulea watoto nyumbani ni haramu kwa kuwa asili hii ni ya mwanamke ?
 
2.Asili ya kitu chenye kudhuru kulingana na mtu mwenyewe na hakimdhuru kila mtu.

Mfano kuna watu wakila nyama ya bata wanadhurika,hapa nyama ya bata itakuwa haramu kwa huyu anayedhurika tu na wala haifai kwake kuwadhuru wengine ambao hawadhuriki na nyama hiyo ya bata.

Sasa hapa ile "hakuna kudhuru wala kujidhuru" inakuwa kwako wewe inayokudhuru na wala haifai kuharamisha kitu hicho kwa wengine wote ati kwa kuwa kuna baadhi kina wadhuru.
Haya ndiyo madhara ya kutumia ufahamu wako pasi na marejeo kwa Wakubwa, matokeo yake ni kukosea juu ya kukosea, unatakiwa ujue tunazungumzia nini mpaka muda huu, suala mazingira linamdhuru msomaji na linamfunga na kumuweka mbali na majukumu yake ya asili. Kwahiyo hili linamuhusu kila atakaye ingia katika mazingira hayo. Sasa hapa huna hoja ya kuyaepuka mazingira kijana.

Mwanamke anapo poteza dini anakuwa anaidhuru nafsi yake, na nukta zako mbili ni nukta moja hizo ila kwa uchachefu wako wa Elimu ukazigawa na kuwa mbili, wakati zote zinarudi kattika moja.

Sasa nionyeshe nani hadhuriwi na mazingira ya utafutaji elimu na ufanyaji kazi ? Kijana usilazimishe tui la nazi kuwa maziwa, abadani haliwezekani hili, ndiyo maana kadiri unavyo hoji ndiyo unazidi kuhoji ujinga na kurudia rudia nukta zako.
Sasa hapa ile "hakuna kudhuru wala kujidhuru" inakuwa kwako wewe inayokudhuru na wala haifai kuharamisha kitu hicho kwa wengine wote ati kwa kuwa kuna baadhi kina wadhuru.
Hakuna mchanganyiko usiyo dhuru kijana, acha kujidanganya,wala hakuna baya lisilo dhuru, ndiyo maana dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.

Hakuna mwanamke atakayetoka katika mazingira haya akasalimika. Shuhuda ziko nyingi, huko makazini na mashuleni. Kwahiyo hili linahesabiwa hivyo sababu kila anae ingia humo lazima limdhuru.

Ndiyo maana Wanazuoni walitoa changamoto kwa yule atakae tafuta shule au maofisi ambayo mwanamke anaweza kufanya kazi na akakidhi masharti, basi akasome au akafanye kazi, na hakuna anae weza kufanya hili hasa katika nchi zetu ambazo haziongozwi kwa Sheria.

Kadhalika kaida aliyo inukuu Mwanachuoni wa Usuli kwa zama zetu, akaiweka katika madhara na maslahi, na msingi wa kaida hiyo ni hadithi hiyo na aya zile.
 
Sasa kusomea udaktari mwanamke kwa kuangalia ile fani yenyewe ya udaktari inamdhuru nini mwanamke
Usiwe unapinga mambo ambayo huyajui. Udaktari wa kisekula unakwambia nini kuhusu viumbe hai na visivyo hai ? Udaktari wa Kisekula unakwambia nini kuhusu sababu za ugonjwa ?

Kama ulikuwa makini hapo awali nilikuweka wazi ya kuwa Elimu ya kisekula ina sehemu ina matatizo makubwa kwa dhati yake na ina matatizo makubwa katika upatikanaji wake.


Hizi aya unazotoa zinawahusu wanawake na wanaume pia.
Kijana mbona unarudia kuuliza maswali ambayo majibu yake nimeshayatoa ? Au umeishiwa hoja ?

Laiti kama ungekuwa unasoma na kuelewea usingekuwa unauliza maswali ambayo umeshajibiwa. Huki sasa ni kupotezeana muda. Nilikudharau na kukuona wa ajabu pale uliposema hata Sheikh angekuwa hai ungemuhoji, nikaona hapa kuna matatizo ya ufahamu na adabu, yaani unahisi kuhoji kwako ndiyo kila kitu, ajabu una hoji mambo bila kutafakari na hatimaye una hoji ujinga na kurudia jambo lili jibiwa. Uislamu unatutaka tuhoji vya maana.
 
je mwanaume anaruhusiwa kuiuwa nafsi yake katika kusomea hizo fani ila mwanamke haruhusiwi ?

Mwanaume anaruhusiwa kujiingiza katika maangamivu ila mwanamke haruhusiwi ?
Unani potezea muda. Narudia tena kwa mara nyingine na natarajia hutarudia tena kuuliza hili ambalo nilishakujibu.

Nilikwambia baya kwa mwanamume ni baya kadhalika kwa mwanamke, isipokuwa iwepo bayana. Nikasema sababu hapa tunamuongelea mwanamke na kutafuta pesa, ndiyo maana nikirejea narejea kwa munasaba wa Mwanamke, sababu Mwanamke kutoka ni jambo la dharura, ila Mwanaume kutoka ni jukumu lake na kwenda kutafuta.

Sasa ukiuliza tena mwanaume aya au hadithi haimuhusu nitakuuliza kivipi ? Kwahiyo jifunze kuweka kila kitu mahala pake, usipoteze muda kwa kujidai unahoji mpaka unasahau kama unarudia maswali ambayo ushajibiwa.
 
Hakuna anayekataa asili hiyo,lakini haifidishi kuwa haruhusiwi kutoka kwa haja zake binafsi.
Sasa huko kutoka kwake kwenda kujitafutia ndiyo dharura yenyewe na moaka akidhi vigezo. Kinyume na hapo akae nyumbani wale wenye wajibu wakumletea watamletea na atakidhi haja zake.
Asili kukaa nyumbani ila je akienda kazini kwa ajili ya kupata kipato halali akimaliza akalazimiana na nyumba yake asili iko palepale,tofauti na mwanaume akitoka kazini aenda vijiweni na sehemu zingine.
Nitakuuliza je anawajibika kutoka ? Je akitoka anakidhi masharti ? Je hayupo wa kumtimizia haja zake ?

Hapo asili haipo tena kijana unapoambiwa mwanamke akitoka mpaka iwe haja, ujue kutoka kwake aiyo kwa kawaida bali ni kwa dharura, aya iko wazi kijana,ndiyo maana unatapa tapa kutafuta pakutokea na hutoki, unarudia rudia maswali yale yale.

Huyo mwanume kwenda kwake vijiweni ni kukiuka adabu na si jambo zuri, ila asili yake ya kutoka na kutafuta ndiyo wajibi wake. Kwahiyo anae fanya hivyo anatakiwa anasihiwe.
 
Ukisikia asili kukaa nyumbani unadhani ni kuwa haruhusiwi kutoka kwa namna yeyote ile ?
Nacheka sana, kijana sijui aya ile hujaielewa aisee, unaoata shida sana, kuweka matamanio yako mbele ya nususi ma hili huliwezi.

Wanawake wameruhusiwa kwenda misibani, kwenda kuzuru makaburi, kwenda kwenye masherehe haya yapo mzee, na katika yote haya kuna taratibu zake.
Mtume alikataza mwanamke kutoka nyumbani kwake hali kajipulizia manukato.
Kwa maana ATOKE akiwa hajajipulizia manukato yeyote.

Sasa ikiwa mtume anatambua kuwa mwanamke anaweza akatoka lakini kwa sharti ya kuwa asijipulizie manukato wewe ndugu una darja ipi kumzidi Mtume wa Allah ?

Hakuna hadithi yeyote ambayo Mtume alikataza wanawake kutoka majumbani mwao kuziendea haja zao za kimaisha,na wala haikuthibitipo kuwa Mtume aliwafukuza wanawake katika miji warudi majumbani mwao.
Sasa aliwafukuza vipi katika miji wakati walikuwa wanakaa majumbani isipokuwa kwa dharura ?

Wala hakuna hadithi wala aya inayo waruhusu wanawake watoke wakatafute ugali na kulea familia au kwa mambo yake biafsi.
 
Kama kuchanganyika ni haramu kwa nini iwe haramu kwa mwanaume wakati madhara ya kuchanganyika yanawakuta wote kama tulivyokubaliana ?
Mbona unauliza mambo ambayo sijayasema kijana, wapi niliandika Mwanaume ameruhusiwa kuchanganyika ? Usipoteze muda kujadili mambo ambayo hayapo, huku ni kupoteza muda na kuishiwa hoja.
 
Mungu atuepushe sote na hili mbali.

Kuna watu miongoni mwa Waislamu wanataka watakachokifuata wao Waislamu sote tukifuate hicho hicho. Hii ni siasa ya Firauni! Firauni alikuwa atakachokiona yeye ni sawa hicho kinapita kwa ninyi nyote nacho ni halali kwenu kuwa sawa.

Mfano wa watu hawa ukimkhalifu anakuambia umemkhalifu Mungu na Mtume. Hajakhalifiwa Mungu na Mtume imekhalifiwa fahamu yako. Kwa nini tusiige mfano wa watu wema waliyotangulia mfano Imam Malik r.a.

Alipoambiwa kitu mfano wa Zurri anachokilazimisha jawabu lake linapingana na wewe Zurri unachokilazimisha kwenye huu Uzi. Alimjibu Khalifa kwa ufupi tu kuwa Maswahaba walienda sehemu mbalimbali kwa kutawanyika kufundisha dini na walikuwa na dalili kwa kile walichokifikisha kwa watu. Ukitaka wafuate mwenendo wangu tu hali ya kuwa tumetofautiana kwenye ufahamu wa baadhi ya mambo na kila mtu ana dalili ukilazimisha itakuwa si sawa.

Sasa Bw. Zurri jiangalie mahesabu yako kwenye dini unapiga kama mahesabu ya siasa ya Firauni. Ni lazima tukuambie ukweli, huko unakoelekea ambapo wewe unakuona pako sahihi ukweli ni kuwa unakopaelekea huko umepotea.

Ibn Sina R.A anasema: "Sema tumepewa mtihani tumeonjwa na watu ambao kwamba wanadhani Mwenyezi Mungu hakuwaongoza watu kwenye haki isipokuwa ni wao."

Hao watu aliyowasema Ibn Sina wewe ni mmoja wao. Kingine ujibuji wako ni wa kiburi (dharau dharau) kwamba mimi ni bora najua kuliko wewe. Sasa hayo nayo ni mahesabu ya Ibilisi. Yaani mahesabu yako unayapiga kama Ibilisi.
 
Back
Top Bottom