Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

1.kunawake zetu na mama zetu ambao kisheria wanatakiwa watibiwe na wanawake wenzao huko mahospitalini,kusoma wanawake udaktari kunasaidia kuwepesisha jambo hilo.ila kwa dharula ya uhaba wa wanawake ndo wanatibu wanaume.
Haja hakuna sababu waliopo katika hao Wanawake wanatosheleza wengine.

Lakini hakuna Mwanamke anayesoma hizo fani aasalimika katika dini yake, na dini ndiyo jambo la msingi na linalo tangulizwa kuliko mengine. Leo hii ukifa hutaulizwa kwanini hukuwa Daktari mzee wala kwanini hukuwa Muhandisi.

Na hii dharula ya Wanaume kuwatibu Wanawake bado ina nafasi, sababu ya Maslahi na athari yake ni ndogo.
 
Naendelea kuhoji kuwa kwa mujibu wa sheria ya dini ni mwanamke peke yake ndo anayekatazwa kuwa katika mchanganyiko na wanaume ama hata mwanaume anakatazwa kuchanganyika na wanawake ?
Hujakatazwa kuhoji ila hoji vitu vya maana.
 
Munkari huo ni ule wa mke wako,mke wangu,mama yako,mama yangu kufunuliwa nguo na kuonwa tupu zake na daktari wa kiume ambaye ndo alisomea udaktari kwa sababu wale wanawake mliwakataza.
Hii ndiyo dharura sasa mzee.

Ama hiyi ya Wanawake kwenda kusoma hakuna barakka wala natija ya jambo hilo kwani uovu ndiyo unakuwa maradufu. Hakuna mwanamke anaesoma fani ya Udaktari kisha akajipangia yeye kazi ya kufanya, lazima afate mfumo ulio pangwa na kuratibiwa. Ndiyo maana Wanawake wanasoma na wanapoteza dini zao sababu hakunw mazingira yanayo waunga mkono katika jambo hilo.
 
Kwa hiyo wanaume wanaruhusiwa kuchanganyika na wanawake ila wanawake tu ndo hawaruhusiwi kuchanganyika na wanaume ?
Mwanamume haruhusiwi kuchanganyika na Wanawake na yeye anaingia katika hili. Sababu tunaangalia suala la Mwanamke na kutafuta, ndiyo maana kutafuta kwa mwanamke ni dharura ila kutafuta kwetu sisi Wanaume ni wajibu na hili ni jambo letu.
 
Kwani hapo tatizo ni uharamu wa elimu au tatizo ni uharamu wa mchanganyiko ?
Madhara yanayo patikana katika uchukuaji wa Elimu hiyo ndiyo hufanya jambo hilo kuwa haramu, sababu ni haramu kuzidhuru nafsi zetu.

Elimu kwa ujumla wake si haramu, japokuwa kuna baadhi ya mambo ya kufru katika Elimu hizo.
 
Sheria yenu hiyo ya kuwakataza wanawake tupu imetokea wapi ?
Fitna ya mchanganyiko iko wazi sana katika Uislamu, hii inaingia kwetu sote, ila kutafuta kwa mwanamke ni jambo la dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.

Kuchelea fitna na tumeusiwa juu ya kuiogopa fitna. Kwahiyo hili lilikatazwa na Qur'aan kwa kuwaambia Wanawake watulizane majumbani mwao, ndiyo ikitokea haja ya wao kutoka, basi itifaki huzingatiwa na kama ikionekana madhara ni makubwa kuliko faida basi atakaa.
 
Kwa hiyo unakubali kuwa kama haifai mwanamke kusoma kwa zama hizi kutokana na mazingira basi na mwanaume pia haifai kusoma kwa sababu kama ni baya basi baya kwa wote ?
Swadaktaa, huu ndiyo Uislamu.

Ila linapokuja suala la kutafuta,kutafuta ni kwetu sisi Wanaume.
 
Unajitutumua sana aisee ila ndo hivyo tu,mambo mazito haya.

Inataka ufahamu kuacha ushabiki na ufulani kasema.
Nimecheka sana, sababu mimi situmii akili zangu zaidi ya kurejea kwa wakubwa zangu, hili ni jambo rahis sana kwangu.
 
Hizo athari si zinafanywa na wanawake na wanaume.sasa mbona akatazwe mwanamke tu wakati hizo athari zinatokea kwa kutekeleza wote wawili mwanamke na mwanaume.
Suala la mchanganyiko hili ni la haramu kwa wote. Ila tunalo kuja kuangalia, kutafuta hela kwa mwanamke, hili si jambo lake ni jambo letu sisi,ndiyo maana mpaka mwanamke atoke na akatafute vigezo vyake kuvikidhi ni muhali hasa kwa nchi zetu hizi ambazo hazifati sheria za dini. Ila Wanaingia wanawake wote katika madhara haya, ukimuharibu mwanamke ujue umeharibu jamii kubwa sana.

Sasq msiwe mnahoji ujinga bila kuyaangalia mambo haya kwa mapana yake na athari zake hasi.
 
Allah akubaarik ndugu.

Umeongea maneno mazima sana.

Umegusia mambo makubwa sana.

Na nilimuambia bwana zurri kuwa huo msimamo wake ndio ambao unawaponza masalafy wengi kukatana kila kukicha,magomvi hayaishi,kejeli wao kwa wao mpaka unashangaa hawa jamaa vipi hawa.

Leo hakuna salafy ambaye amesalimika na mwenzake,huyu atamsema tule,yule atamsema yule mwingine na mwingine atamsema mwingine basi tafrani tupu kwa hawa ndgu.

Wanaziendea hadithi pasi na ufahamu,kuharibu kwaao ni kukubwa sana kuliko kutengeneza.
Suala la migongano baina ya Masalafi hili si jambo la ajabu na hii migongano haionyeshi ya kuwa Masalafi hawako katika haki ila hii ni mitihani tu ili Allah awaone ni kina nani Wakweli katika hili, na kuonyesha watu hilo, na kila mgongano unao usikia katika safu ya Masalafi una julikana chanzo chake.

Shaykh Rabee Allah amuhifadhi hili amelibainisha wazi na miongoni mwa sababu alizo taja ni vijana kupenda ukubwa, kupenda kuwa na wafuasi, kupenda umaarufu na husda.
 
Masalafi wengi sana wanaamini kuwa chao ndo sahihi na kufuata kisichokuwa chao basi ni dhwalaala.

Kuna mwalimu wetu mmoja yeye hakubaliani na mambo ya maulidi na dua za msikitini,lakini anavyoyazungumzia kwa utaratibu na ustaarabu mpaka wengine wanamsema kuwa anatetea watu wa bidaa,lakini maalim yeye harudi nyuma anasema kuwa wale ni watu wana maoni yao ijapokuwa kwa upande wangu naona sio sahihi.

Hawa ndio watu wa kusoma kwao ni watu wenye busara na hekima na uvumilivu.
Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe, hili hakuna anae pinga isipokuwa mtu wa matamanio na mzushi.

Mimi nawapa kazi nyinyi, mlete ushahidi wenu ya kuwa ni binti gani aliyesomea udaktari na akafanya kazi ya fani, amesalimika katika dini yake.

Uovu unakimbiwa uovu haufatwi.

Ahsante.
 
Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe, hili hakuna anae pinga isipokuwa mtu wa matamanio na mzushi.

Mimi nawapa kazi nyinyi, mlete ushahidi wenu ya kuwa ni binti gani aliyesomea udaktari na akafanya kazi ya fani, amesalimika katika dini yake.

Uovu unakimbiwa uovu haufatwi.

Ahsante.

Haki si ajabu uko na kasoro kubwa kwenye ufahamu wako!!

Hebu funga break kidogo urudi nyuma!!

Waangalie na wanawake ambao wengi wao sio wasomi wala hawana uwezo tofauti na kufanya kazi ngumu na hatari (mama ntilie, wahudumu migahawani n.k) ili mradi yeye pamoja na watoto wapate japo kushibisha matumbo yao!!!

Kumbuka aina hii ya wanawake wengi wao ni wale either wameachwa na waume zao waliotangulia mbele za haki ama ni matokeo ya kupangwa kama team ya mpira matokeo yake mke wa kwanza mpaka wa nne na vimada wote wana watoto wa mwanamume mmoja tena hasiye hata na kazi ya kueleweka wala biashara ya maana ya kutunza na kulisha familia ya more than 20 people! Hapo hujaweka ndugu na jamaa!!

Japo ni kweli kumekua na wimbi kubwa la wanawake wenye watoto bila baba, lakini tukumbuke haya ni matokeo ya misingi ya familia walizozaliwa na kukulia huko! Na pia haya ni matokeo ya matendo ya wote wawili (kiumeni na kikeni) kwa baadhi ya cases!!

Tatizo la wanaume kama wewe linaathiri sana mfumo wa kimaadili kizazi na kizazi!! Imagine physiology na future ya watoto wanaozaliwa katika familia za wababa kama wewe zitakuwaje na zitazaa matunda gani?? Or maybe I should remind you that an apple never falls far from its tree?!? Utu ni mizizi na mizizi ikisimikwa katika upuuzi huzaa upuuzi!!

Binaadam yoyote yule wa kike ama wa kiume, ameumbwa ayatawale na kuyashinda mazingira na sio the other way around!!

Kingine, wote wanawake kwa wanaume wako mashakani kimaadili muda wote wa uhai wao endapo tu wakiyaruhusu mazingira yawatawale! Na ndio maana kuna wanawake wanalala na boda boda drivers na wanaume wanaolala na mabinti wa kazi!!


Ps; Hatimaye Leo umekiri uSalafy!! Allah Akbar! (Mungu ni Mkubwa!!) [emoji2296][emoji28]
 
Usalafi ndiyo Uislamu wenyewe, hili hakuna anae pinga isipokuwa mtu wa matamanio na mzushi.
Hatuutuhumu usalafi tunawatuhumu masalafi.

Kama ambavyo hatuutuhumu uislamu bali tunawatuhumu waislamu.

Kuwa makini na wanayoyasema watu.
 
Mimi nawapa kazi nyinyi, mlete ushahidi wenu ya kuwa ni binti gani aliyesomea udaktari na akafanya kazi ya fani, amesalimika katika dini yake.
Wewe uko serious mkuu ?

Wako wengi sana.

Nakupa mfano kuna hospitali moja siitaji jina kuna wamama kibao tu wanatibu wako salama na dini yao.

Wapo wengi tu wana dini na wamesoma udaktari wewe unasemaje na nawajua kwa majina ?

Alafu kwani mbona kuna wanaume ambao wanasoma udaktari na hawajasalimika na dini yao kwa hiyo hii tuwakataze na wanaume kusomea udaktari kwa kuwa kuna baadhi hawapo salama na dini yao ?
 
Suala la migongano baina ya Masalafi hili si jambo la ajabu na hii migongano haionyeshi ya kuwa Masalafi hawako katika haki ila hii ni mitihani tu ili Allah awaone ni kina nani Wakweli katika hili, na kuonyesha watu hilo, na kila mgongano unao usikia katika safu ya Masalafi una julikana chanzo chake.

Shaykh Rabee Allah amuhifadhi hili amelibainisha wazi na miongoni mwa sababu alizo taja ni vijana kupenda ukubwa, kupenda kuwa na wafuasi, kupenda umaarufu na husda.
Ndo hayo tunayazungumza.

Pakiwa na migongano basi ina maana nyie kwa nyie kuna mmoja anamuona mwenzake yuko katika haki na mwingine yupo katika batili ndio maana mnagongana ati.

Kama wote mnajiona mpo katika haki mbona sasa yatokee magomvi baina yetu kwa yenu nyie.

Hapa hatusemi usalafi tunawasema wanaofuata huo usalafi wana matatizo wengi katika wao kwa sababu kama alizotaja huyo shekhe rabee.

Na hapa ndo tunachozungumza ndicho shekh rabee nae kakizungumza na kuna sababu nyingi tu kama kiburi,kujiona mtu yeye ndo anapatia sana,kujifanya wachungu na dini n.k

Haya yote yanapelekea salfu baina ya salafiyyuun kukatika mapande mapande.

Kikubwa vijana wengi mnaojinadi masalafi hamna subra na umakini katika kuyaendea mambo.

Na hili linadhihirika kwako hapa.
 
Sijasoma uzi ila nasemaje "Mwanamke mke ,mchumba , hawara hasomeshwi.
 
Suala la mchanganyiko hili ni la haramu kwa wote
Enheee..
Ila tunalo kuja kuangalia, kutafuta hela kwa mwanamke, hili si jambo lake ni jambo letu sisi
Katika hadithi ama aya gani inayosema kuwa kutafuta hela ni jambo letu sisi ?

Umesahau yule mkewe bwana mtume ambae alikuwa ni mfanya biashara mzuri tu katika maisha yake na Mtume pia akashiriki katika bishara hiyo ?

Wapi mtume alikemea utaratibu huo wa mwanamke kujitafutia katika vile vya halali ?


ndiyo maana mpaka mwanamke atoke na akatafute vigezo vyake kuvikidhi ni muhali hasa kwa nchi zetu hizi ambazo hazifati sheria za dini. Ila Wanaingia wanawake wote katika madhara haya, ukimuharibu mwanamke ujue umeharibu jamii kubwa sana.
Hivyo vigezo kaviweka nani zaidi ya Allah na mtume wake ?

Na ni vipi hivyo ?

Alafu kama unakubali kuwa hata wanaume yanawahusu yale ambayo wanawake yanawahusu katika mada hii mbona unamlenga mwanamke tu wakati huo mwanamke naye akienda nje atakutana na mwanaume ambaye wewe unaona haina shida kukutana na mwanamke..?
 
Swadaktaa, huu ndiyo Uislamu.
Kwa hiyo ni sahihi kwa upande wako mwanaume apitie kuyafanya ya haramu haina shida kwa kuwa anatafuta riziki sio ?

Haina shida hiyo kumbe kwa mwanaume kufanya haramu hiyo ya mchanganyiko kwa kigezo cha riziki ?
Ama hiyi ya Wanawake kwenda kusoma hakuna barakka wala natija ya jambo hilo kwani uovu ndiyo unakuwa maradufu. Hakuna mwanamke anaesoma fani ya Udaktari kisha akajipangia yeye kazi ya kufanya, lazima afate mfumo ulio pangwa na kuratibiwa. Ndiyo maana Wanawake wanasoma na wanapoteza dini zao sababu hakunw mazingira yanayo waunga mkono katika jambo hilo.
Unasema hakuna tija wala baraka binafsi nina mtu wangu wa karibu wa kike ametibiwa mara nyingi na madaktari wa kike tena kutibiwa ambako kunahitaji kufunua maungo yake.

Na hao madaktari ni wanawake wamehifadhika na dini na tabia zao.

Na hapo wanapofanya kazi wamepangiwa na utaratibu na sio kama wamejipangia wao.

Kutibiwa mwanamke na mwanamke mwenzie sio baraka na tija ?

Sababu ya kupoteza dini zao ni kwa sababu hawana msimamo na sio kwa sababu ya udaktari wanaosomea.

Kuna binti mmoja ni rafiki wa mke wangu amesoma pale MUHAS kamaliza udaktari lakini alikataa kufanya kazi.

Lakini mpaka anamaliza chuo alikiwa ni salafi mzuri huyo dada.sasa huyu mbona mpaka amemaliza masomo amehifadhika na dini na tabia ?

Unasemaje juu ya uwepo wa wanawake ambao ni madaktari na wamehifadhika na dini na tabia zao , hawa unasemaje ?
 
Fitna ya mchanganyiko iko wazi sana katika Uislamu, hii inaingia kwetu sote, ila kutafuta kwa mwanamke ni jambo la dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadirio yake.

Kutafuta kwa mwanamke kunategemea na mahitaji.

Mwanamke anahitaji kula kila siku kwa hiyo sio vibaya kwake akatafuta chakula kila siku kwa njia ya halali.

Mwanamke anahitaji kuvaa katika muda wote wa maisha yake hivyo sio vibaya mwanamke akatafuta mavazi katika muda wote wa maisha yake.

Sasa kusema kuwa ati mwanamke kutafuta ni dharura huu udharura umeutoa wapi wakati naye ana mahitajio yake ?

Yaliyowekwa na sharia ni kuwa ikiwa MWANAMKE AMEOLEWA BASI MAJUKUMU YA HUDUMA NI YA KWAKE MWANAUME AMHUDUMIE MKEWE.

Sasa hapo ni kwa aliyeolewa atahudumiwa na mumewe,kwa ambae hajaolewa na kuna wangapi hawajaolewa watahudumiwa na nani wengine ndugu hawana wanajitegemea wenyewe pia.

Na kuwa majukumu ya huduma kuachiwa mwanamume hiyo haifidishi katazo la mwanamke kujitafutia pesa.

Kama ambavyo jukumu la ulezi wa familia ni la mwanamke haina maana kuwa ati mwanaume ni haramu kulea familia.bali mwanaume pia anaweza kulea familia kama ambavyo mke analea.

Sasa wewe unaharamisha kwa msingi upi madhubuti wa kisheria ?
 
Sasa niambie ulazima wa jambo ambalo linakiuka asili ya mwanamke ni upi ?
Asili gani unayoisema wewe na umeshabainishiwa huko juu kuwa hata mkewe mtume alikuwa mfanya biashara na wanawake wa zama hizo walikuwa wengi wakitengeza mapambo na kuuza,walikuwa wanafanyia biashara majumbani ?

Asili gani inayokeukwa ?
Aya inasema wanawake walazimiane na majumba yao.
Naam.
Aya inasema wanawake walazimiane na majumba yao. Ikitokea wakatoka basi watoke kwa haja, hii haja inakuwa katika mlango wa dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadiriyo yake. Kwahiyo unapo uliza swali la hovyo kama hili ulitakiwa utoe ushahidi wa kuruhusu jambo hili, toka katika hadithi au Qur'aan. Sasa Uislamu wetu umeruhusu watu kuhoji ila umekataza kuhoji ujinga, na tukapigiwa mfano kwa Wana wa Israeli walivyo potea kwa kuhoji hoji kwao ujinga.
Jambo ambalo ni mubaaha wewe unayekataza ndo utoe dalili.

Tokea hapo nimekuambia kusomea fani mbali mbali zaelimu isiyokuwa ya Allah na Mtume ni jambo la mubaaha.

Na mubaaha inajuzu mpaka dalili ya kukataza ije.
Unayo dalili ya kukataza mwanamke kusoma fani hizo ?

Unaposema mwanamke atoke kwa dharura ambayo hukadiriwa kwa makadirio na kwa haja.

Kwani mwa amke kwenda kazini kutafuta hela sio haja ambayo anahitajia kutimizamajukumu yake ya ndani ?

Au haja ya mwanamke kutoka ambayo hawezi kuifanya mwingine ni ipi ili tuone kuwa haja hizo kumbe mwanamke lazima atoke bila yeye hafanyi mwingine ?
 
Back
Top Bottom