Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Wallahi

Wallahi nimecheka mpaka mtoto kashtuka...
Nilikwambia Jurjani ww ni mwepesi...nilikueleza kuwa ww hauko smart upstairs zaidi ya dada Coach Slamah Hamad loooh....

Iko hivi....waliozama katika elimu Tofauti Kuna Mambo ya FALSAFA na NAHAU....

Na hiyo uliyonukuu Ni mojawapo,alhamdulillah unazd kudhihirisha IMMATURITY yako.....

Kweli wahabi mMazwazwa...


😀😀😀😀
 
Hii dunia Yani mtu ili awe mwanaume kamili anaona mpaka amunyanyase mkewe au mwanamke


Wapo wanaojitambua sema ni wachache wengi ni hawa jamii ya akina jurjani na yule mwenzie.
 
Na argument yoyote Kuna kukubaliana au kutokubaliana and I'm serious na Wala sito kushindana hapa kwani Kuna hela useme napata, it's just a matter of discussion and not competition.
Umeshasema ulikuwa una argue.... I wasn't arguing with you.... I thought i was discussing this with you.
 
Wapo wanaojitambua sema ni wachache wengi ni hawa jamii ya akina jurjani na yule mwenzie.
Tatizo Ni elimu na uelewa Kuna baadhi ya jamii zina hold Mambo ya mateso, thank God nimekuwa na jamii ya watu waelewa na wastaarabu, Mambo za kujiona eti Mimi mwanaume ni Bora hazipo nazisoma humu JF, wote tumekuwa tukilelewa kuheshimu watu wote sawa, tumepewa elimu sawa, Tena wanawake tunatiwa moyo kusoma na kufanya kazi kwa bidii, na hamna kilichobadilika.
Ila nawahurumia wanawake wanaoishi na wanaume type ya jurjani, and Samcezar maana wamebeba mizigo ya misumari haibebeki wako so bitter towards women's.
 
Jibu nililo kupa laiti kama ungekuwa na akili, ungekomea pale, maana habari za al Imaam al Ghazali kwa Wanafalsafa ni nzito, wewe si unawaona kwamba ni vichwa sana na unawareja, sasa kipindi cha uhai wa al Ghazali, hakuna walio onekana ni Wajinga katika mgongo wa ardhi kuwazidi Wanafalsa. Sasa soma hicho kitabu uijue Falsafa na uwajue Wanafalsafa, ndiyo maana nimekwambia nimekupa jibu lilijitosheleza.

Hapa labda nikufundishe wewe, mimi nimesoma kitabu kiitwacho "Adabul Bah'th wal Munadhara (The Etiquette of Debate and Research) cha Imaam ash Shanqity. Kwahiyo najua nini nachokifanya.

Nacheka sana, Elimu ya mantiki kihistoria ni Elimu mpya katika Ulimwengu wa Kiislamu. Historia yake ni Baadhi ya Waislamu kuichukua kutoka kwa Wakristo walioshi Jordani ya zamani na kwa Wale Sabaia, hii iliwaathiri sana na kuwapelekea kukanusha sifa za Allah kwa kufata mawazo ya kina Aristosto. Miongoni mwa wasomi hao wa Kiislamu ni akina Ja'ad bin Dirham, kina Abul Ma'al al Juweinyi, lakini hao baadhi yao kabla ya hawajafa walitubia kwa Mola wao na kujutia muda walio upoteza katika Elimu ya Mantiki. Soma vitabu kama "Swaun al Mantiq" cha Imaam Jalaludin as Suyuti ameidhoofisha mno fani hiyo, soma kadhalika kitabu "Dham al Kalam wa ahlihi" uone ya kuwa Mantiki ni nusu uchizi na siyo fani ya mtu kusoma sababu inamfanya mtu awe mjinga zaidi.
Wewe ni msalafi sugu?
 
Vijana acheni ujanja ujanja, mbona hamuelezi hizo biashara walikuwa wanazifanyaje ?

Kuna binti mmoja, huko juu alidai ya kuwa mama Khadija alikuwa anafanya biashara na mtume, basi kwa ujinga wake akajua ya kuwa alikuwa anachangamana na kuruka mitaa, wakati alipoolewa akakaa nyumbani na mtume akawa anatumwa na mkewe juu ya biashara hizo. Sasa kwa kutusaidia tunaomba utuambie biashara za huyo mamma na binti yake,walikuwa wanaifanyaje ?

Wanawake wanafanya biashara na kumiliki mali, ila si kwa namna ya wanawake hawa wanavyofanha, na hili tuliwaambia tangu mwanzoni mwa hii mada.

Kwenye Quran Allah anaamrisha wanawake wa Mtume swallallahu alayhi wasallam na wanawake wa ulimwengu mzima wakae nyumbani kwao wasitoke majumbani kwao isipokuwa kwa haja au kwa dharura ambayo kwamba ni dharura ya msingi itakayomfanya aweze kutoka nyumbani.

Swali la msingi: Yafaa mwanamke kufanya kazi?
Jawabu ni naam! Mwanamke anafaa kufanya kazi kwa masharti ambayo Maulamaa ambayo wameyaweka. Ambayo ni
•Kujistiri kwa istara ya heshima.
•Asijitie manukato ambayo kwa hakika ni yenye kumshawishi mwanaume.
• Asichanganyikane na mwanaume. Kuchanganyika hapa si kwamba asikae naye karibu bali ni kuchanganyika kwa kichoheo cha kuyaleta matamanio.
Na mengineyo.

Ikiwa mwanamke akiyaweza hayo mwache akafanye kazi.

Biashara alizokuwa akifanya mama yetu Bi. Khadija R.A zinafahamika, aliwekeza kwenye biashara na zilikuwa ni biashara za masafa marefu kutoka Makka kwenda Syria n.k. Kwa maumbile ya mwanamke na kwa mazingira yamwanamke biashara ya masafa marefu kwao ni changamoto. Ndiyo maana tangu awali kulikuwa na mtu akisimamia misafara yake ikiwa kwenye safari hizo za masafa marefu hata kabla ya Mtume s.a.w.

Sasa Mtume ndiye mumewe na biashara zake ni za masafa marefu na mama yetu Bi. Khadija R.A amewekeza ni mtaji wake hiyo biashara. Unafikiri ni nani atakayekuwa msimamizi wa hizo biashara kama siyo mumewe Mtume swallallahu alayhi wasallam?

Si busara kulazimisha msimamo (rai yako) wako na kuufanya uwe sahihi zaidi na kuiweka batwil, uharamu kuwa haifai kabisa mwanamke kufanya kazi kisa alishasema Sheikh Al Fawzaan, Sheikh al Uthaymiin basi yatosha! Ya hao haki na ya wengine ni baatwil.

Binafsi yako umeamua kufuata fatwa hiyo na kwako imekinai hakuna mushkeri ifuate. Wenzako wamefuata fatwa ya Ulamaa mwengine na kwao imekinai hakuna mushker waache waifuate. Mushkeri unakuja kulazimisha ya kwako ni sahihi ya wengine ni ujanja.

Na hii hali unayo! Si ya mara 1 au mara 2. Kwa kadri ulivyosoma wewe basi wewe upo sahihi zaidi na wenzako hawako sahihi zaidi. Hiko si kipimo cha elimu! Hicho ni kipimo cha kutokuwa na nidhamu ya kielimu.
 
Tatizo Ni elimu na uelewa Kuna baadhi ya jamii zina hold Mambo ya mateso, thank God nimekuwa na jamii ya watu waelewa na wastaarabu, Mambo za kujiona eti Mimi mwanaume ni Bora hazipo nazisoma humu JF, wote tumekuwa tukilelewa kuheshimu watu wote sawa, tumepewa elimu sawa, Tena wanawake tunatiwa moyo kusoma na kufanya kazi kwa bidii, na hamna kilichobadilika.
Ila nawahurumia wanawake wanaoishi na wanaume type ya jurjani, and Samcezar maana wamebeba mizigo ya misumari haibebeki wako so bitter towards women's.
Naskia hawa Ndio wana wivu balaa
 
Umeshasema ulikuwa una argue.... I wasn't arguing with you.... I thought i was discussing this with you.
Yote sawa tu Ina same meaning depending na wewe unatumia muktadha gani, by the way that's not a case
 
At least Google basi the difference between Argument vs discussion....
 
Kwenye Quran Allah anaamrisha wanawake wa Mtume swallallahu alayhi wasallam na wanawake wa ulimwengu mzima wakae nyumbani kwao wasitoke majumbani kwao isipokuwa kwa haja au kwa dharura ambayo kwamba ni dharura ya msingi itakayomfanya aweze kutoka nyumbani.
Unaweza kunitajia hizo dharura ni zipi na vipi hukadiriwa kwa mujibu wa sheria ya Uislamu ?
Biashara alizokuwa akifanya mama yetu Bi. Khadija R.A zinafahamika, aliwekeza kwenye biashara na zilikuwa ni biashara za masafa marefu kutoka Makka kwenda Syria n.k. Kwa maumbile ya mwanamke na kwa mazingira yamwanamke biashara ya masafa marefu kwao ni changamoto. Ndiyo maana tangu awali kulikuwa na mtu akisimamia misafara yake ikiwa kwenye safari hizo za masafa marefu hata kabla ya Mtume s.a.w.
Hoja yangu ni kuwa baada ya kuolewa na mtume, biashara zake alikuwa anazifanyaje ?
Au tuonyeshe alikuwa anashiriki vipi katika biashara zake ?
•Kujistiri kwa istara ya heshima.
Hii stara ya heshima ni stara gani na ina sifa gani ? Nikajua ungeandika stara kwa mujibu wa sheria ya Uislamu..
• Asichanganyikane na mwanaume. Kuchanganyika hapa si kwamba asikae naye karibu bali ni kuchanganyika kwa kichoheo cha kuyaleta mat
Maelezo haya ni ya msomi gani au marejeo yako ni wapi ? Maana sijawahi kuona maelezo kama haya hapo kabla.

Kwani Uislamu unasemaje juu ya kukaa karibu kati ya jinsia mbili zenye kutofautiana na wenye kuweza kuoana ?
Ikiwa mwanamke akiyaweza hayo mwache akafanye kazi
Kwa harakaharaka kwa masharti hayo, japokuwa maelezo yako hayaja tosheleza, kwa mazingira yapi mwanamke anaweza kukidhi masharti hayo ?

Hapa umenikumbusha swali moja aliulizwa Imaam Ibn Baz, kuhusiana na michanganyiko baina ya jinsia mbili tofauti.
Sasa Mtume ndiye mumewe na biashara zake ni za masafa marefu na mama yetu Bi. Khadija R.A amewekeza ni mtaji wake hiyo biashara. Unafikiri ni nani atakayekuwa msimamizi wa hizo biashara kama siyo mumewe Mtume swallallahu alayhi wasallam?
Sasa kwanini mtume hakumruhusu hata kufanya hizo biashara za masafa mafupi ? Au kuna sehwmu unaweza kutupa ushahidi ya kuwa mama Khadija alikuwa anafanya biashara mbali na nyumbani kwake ?
 
Unaweza kunitajia hizo dharura ni zipi na vipi hukadiriwa kwa mujibu wa sheria ya Uislamu ?

Hoja yangu ni kuwa baada ya kuolewa na mtume, biashara zake alikuwa anazifanyaje ?
Au tuonyeshe alikuwa anashiriki vipi katika biashara zake ?

Hii stara ya heshima ni stara gani na ina sifa gani ? Nikajua ungeandika stara kwa mujibu wa sheria ya Uislamu..

Maelezo haya ni ya msomi gani au marejeo yako ni wapi ? Maana sijawahi kuona maelezo kama haya hapo kabla.

Kwani Uislamu unasemaje juu ya kukaa karibu kati ya jinsia mbili zenye kutofautiana na wenye kuweza kuoana ?

Kwa harakaharaka kwa masharti hayo, japokuwa maelezo yako hayaja tosheleza, kwa mazingira yapi mwanamke anaweza kukidhi masharti hayo ?

Hapa umenikumbusha swali moja aliulizwa Imaam Ibn Baz, kuhusiana na michanganyiko baina ya jinsia mbili tofauti.

Sasa kwanini mtume hakumruhusu hata kufanya hizo biashara za masafa mafupi ? Au kuna sehwmu unaweza kutupa ushahidi ya kuwa mama Khadija alikuwa anafanya biashara mbali na nyumbani kwake ?
Wewe una elimu ya mabadiliko ya kawaida, hauna elimu ya mabadiliko ya kweli ya ufahamu.
 
Back
Top Bottom