Sasa ndiyo uone hakuna haja ya wao kusoma udaktari kwa sasa sababu hao waliosoma wanakidhi hilo,
Sasa hapa nakuuliza tokea hapo kuwa kuwepo kwa wanaokidhi hizo haja ni dalili kuwa hawa ambao hawajasoma ni haramu ?
Yani kuwepo kwa watu ambao watamswalia maiti ina maana kuwa wengine wakitaka kuswalia ni haramu kwa kuwa kuna ambao wameshatosha kukidhi jambo hilo ?
Alafu pia haja ipo.suala sio kutibiwa suala ni kuwa unatibiwa na nani ?
Huwezi kusema kuwa wanakidhi wakati idadi ya madaktari wa kike ni chache kuliko wa kiume na hii hupelekea munkari wa wanaume kuwatibu wanawake.
Na hii ya wanaume kuwatibu wanawake katika uislamu haifai kwa sababu hii ya mwanamke kuonwa tupu yake na daktari athari ni kubwa kuliko mwanamke kuchanganyika na wanaume.
Sasa ajabu unakubali dharura ya mwanamke kuwa chumbani na dokta akifunuliwa maungo,alafu hapo hapo unakataa mwanamke kukaa darasa moja na wanaume akiwa amejistiri anasoma udaktari ili aje kupunguza wanawake kutibiwa na wanaume ?
hasa ukiangalia mazingira si rafiki kwao hao wanawake na wasio kuwa wanawake.
Huwezi kusema mazingira ya wanawake sio rafiki alafu hapo hapo unakubali dharura ya mwanamke kukaa chumbani na dokta wa kiume akitibiwa na pengine kufuniliwa maungo,hili unasema dharura.
Madhara ya dokta wa kiume kukaa chumbani na mwanamke akimtibu na kuona maungo yake,hili lina madhara zaidi kwa sababu linakusanya mambo mawili.
1.mazingira ya ufalagha baina ya dokta na mgonjwa ambayo kisheria hayafai.
2.kuona maumbile ya mgonjwa wa kikeyasiyotakiwa kuonekana na mwanaume wa kando. hili pia halifai.
Sasa ukiangalia kusoma chuo mazingira yake hayazidi uhatari wa mazingira ya dokta na mgonjwa kwa sababu kwa docta huingia mmoja mmoja na chuo watu hukaa kwa vikundi zaidi.
Alafu pia kukaa faragha ndio hatari kuliko kuchanganyika kwa sababu faragha watu hubakwa na kuzini wakiwa peke yao.hili la ufaragha linapatikana kwenye utibuji ambao wewe unautia kwa jina la dharura.
Lakini pia kwenye mchanganyiko wa mavyuo hakuna kufunuana maungo baina ya mwanamke na mwanaume kama ambavyo dokta humfunua maungo binti chumbani.
Sasa kusoma mchanganyiko huwezi kusema mazingira yake sio rafiki wakati kule kwa daktari mazingira ndo sio rafiki zaidi.
Lakini ajabu huku unasema dharura,na huku unaharamisja wakati ambao hii dharura unayoidai itaendelea kuwepo kwa sababu ya wewe kukataza mchanganyiko ambao madhara yake sio makubwa ukilinganisha na madhara ya mgonjwa na daktari wa kike.
Sasa ukipima maslahi utaona kuwa kutibiwa na daktari wa kiume mwanamke ni jambo la hasara zaidi kuliko mwabamke huyu kusoma mchanganyiko.
Kwa sababu faragha baina ya mwanamke na mwanaume ina madhara makubwa zaidi ya mchanganyiko baina ya wanawake na wanaume.
Lakini pia mchanganyiko wa watu ni jambo gumu kuliepuka kwa sababu..
1.masokoni kuna michanganyiko.
2.kwenye madaladala kuna michanganyiko.
3.njiani kuna michanganyiko.
Hii michanganyiko uhatari wake ni mdogo kuliko ule mchanganyiko wa mgonjwa wa kike na daktari wakiwa peke yao chumbani.
Kwa hili huwezi kuwa na hoja ambao itaweza kushawishi haya madhara yakawa madogo na kule yawe makubwa.