Swali kwa wasabato na wakatoliki kuhusu kuja kwa Yesu

Swali kwa wasabato na wakatoliki kuhusu kuja kwa Yesu

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Katika waraka wa kitabu cha wathesalonike wa pili,sura ya pili msitari wa kwanza hadi wa nne,Paulo anazungumzia tukio linalotangula kuja kwa Yesu .
Imesemwa siku hiyo haitakuja hadi yule mwasi ajiinuaye juu ya kila kitu kiitwacho Mungu afunuliwe.Naye ataketi katika hekalu la Bwana.
Swali hapa ni kwamba,je ameshafunuliwa?
Na hekalu la Bwana ni lipi?
Kama kuna changamoto kubwa sasa hivi ni kujua hekalu la Bwana ni lipi!
Wakatoliki wanadai wao ndio wakristo wa kweli,wasabato nao huita kanisa lao kama kanisa la kweli.
Sasa huyu mtu wa kuasi atajiinua kwenye hekalu lipi kati ya hayo ambalo ndilo hekalu la Bwana?
Kuna watu hawaendi kanisani kwa kuwa tu hawajui hekalu la Bwana ni lipi?
Tuambieni ili twende huko huko na hatujali huyo mtu wa kuasi akijiinua ni yeye na dhambi zake lakini sisi tunataka tubaki katika hekalu la Bwana
 
Tayari ameshafunuliwa ni nani ufunuo 13 imemwelezea vizuri na pia ufunuo 17 kanisa lililoasi ufunuo 12 ni kanisa safi la kristo atakayekuja kuchukua hawa ndio wanaoshka amri ya mungu na shuhuda zake.
 
Tayari ameshafunuliwa ni nani ufunuo 13 imemwelezea vizuri na pia ufunuo 17 kanisa lililoasi ufunuo 12 ni kanisa safi la kristo atakayekuja kuchukua hawa ndio wanaoshka amri ya mungu na shuhuda zake.
Kwa hiyo hekalu la Bwana ni katolki?
 
Back
Top Bottom