Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo mbona simple tu? Jiulize kwa nini gari inayokimbia wakati wewe umekaa ndani yake ikisimama ghafla unaweza kutokea kwenye kioo cha mbele kama ipo speed sana? Jibu ni unakimbia sawasawa na speed ya hiyo gari ......sasa je kama unakimbia speed sawa na gari unawezaje kutembea taratiibu ndani ya hilo hilo gari kuhama siti moja kwenda nyingine? Au kutoka siting ya nyuma kwenda sit ya mbele taratiibu kabisa? Tena hapo tunaongea gari ambayo speed yake inabadirika badirika ......sasa dunia inaenda constant speed, vitu vyote vilivyopo ndani yake vitakimbia speed hiyo hiyo..vipi nzi aliekaa juu ya bawa la hiyohiyo ndege. akitaka kuruka kutoka bawa moja kwenda lingine?.. mruko wa kuikatiza ndege inayosafiri uelekeo tofauti na nzi.
au
nzi huyo huyo akiwa hukohuko nje ya ndege akiamua kuruka uelekeo huohuo wa ndege kitambo cha mita moja kufikia anapotaka. atafanikisha lengo?
msingi wa swali nimezingatia vitu vyote vinaenda kat
tunapoambiwa na watabiri wa hali ya hewa kwamba Upepo utavuma kwa kasi ya 30km/h. huu upepo hauhusiani na hii dunia au?
iweje mabati yaezuliwe na upepo ambao haufiki hata robo ya speed ya dunia?
Ni kweli na baadae ikaja gundulika kua DUNIA ni Kama tufe (spherical)Galileo alinyongwa na wagalatia vilaza kwa kusema dunia ni tufe na sio tambarare
Sababu alichoeleza ni uongo, hakikubaliani na nature.Sijaelewa sjui ni kichwa changu kigumuu
Kuna kuta za dunia/nguzo ambazo wazungu hawataki zifikiwe, mwezi ndio husogeza maji yaan kupwa na kujaa kwa bahari kwa sababu ya utambalale, kuzama na kuibuka kwa jua upande mwingine yaani nguzo moja na nguzo nyingine na kufanya kati kati kusiguswe na mwanga wa jua
Mifano mingine inayohusisha vyakula vya wanga vinavyohitaji joto maalum ili viive kwa namna inavotakiwa:Nje ya mada; Una unga wa ugali, maji, sufuria, mkaa ,jiko la mkaa, mwiko wa kuongea ugali na banio. Lengo ni kupika ugali.
Umewasha jiko la mkaa kisha ukatenga sufuria la ugali, umeweka maji na unga kiasi ili uandae uji ambao ukichemka ipasavyo utaweka unga halafu kwa kutumia mwiko utasonga ugali.
Swali; Ni kwanini ukiweka unga kabla maji / uji haujachemka vizuri ugali hautaiva (utakuwa mbichi) hata kama utaongeza moto mwingi ?
Niliwahi kuuliza swali hili kwa mwalimu wangu wa physics, badala ya kunijibu alinichapa kwa madai kwamba nauliza maswali ya ajabu ajabu
Hahahahaha"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"
Nadhani swali limefanana hivi; kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?
Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karibuni
Ukitumia common sense kireason kwamba dunia ni flat au ni sphere, utagundua dunia haizunguki au haipo sphere.Hawa flat earth society ukiwasikiliza kama vile wana point flani hivii
Wakati Joshua anapigana vita, Mungu alimwambia Joshua simamisha jua, hakumwambia asimamishe dunia.😄
😄 Mfano mzuri wape hii!! Tuonavyo linapochomoza mashariki kwenda magharibi ni kama tunaona kama linazama chini. Je linazungukia chini Ili liibukie tena mashariki? Jibu ni hapana! Itoshe kusema linazunguka clockwise. Hivyo dunia imesimama tuli kama plate ya saa na jua linazungukia juu ya Dunia kama mshale wa saa unavyozunguka juu ya plate ya saa yenyewe.
Duh! Unaona sasaWakati Joshua anapigana vita, Mungu alimwambia Joshua simamisha jua, hakumwambia asimamishe dunia.
Hata ndege ikiwa juu bado iko controlled na gravity ya dunia."Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"
Nadhani swali limefanana hivi; kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?
Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karibuni
Dunia inazunguka pamoja na kilichopo juu ya ardhi, ni sawa na kusema nzi akiwa ndani ya ndege akataka kuruka kutoka siti ya nyuma kwenda siti ya mbele atashindwa kufika kwa vile ndege inakimbia kwa kasi sana, Hapana si kweli huyo nzi atafika vizuri tu sababu ndege inayembea na yeye anatembea hayupo excluded. Ndivyo ilivyo kwa helikopta hiyo uliyoitolea mfano. Ngoja wanafizikia waje wakufafanulie kitaalamu zaidi.
Wakatoliko walimweka Galileo under house arrest kwa mawazo kama yako. Miaka miambili baadae wakaja kukiri hadharani kuwa jamaa alikua sahihi kwa kusema dunia ndio inazunguka sio jua.Wakati Joshua anapigana vita, Mungu alimwambia Joshua simamisha jua, hakumwambia asimamishe dunia.
Ukitaka kujadili hoja za kisayansi Acha hivyo vitabu pembeni....Wakati Joshua anapigana vita, Mungu alimwambia Joshua simamisha jua, hakumwambia asimamishe dunia.
Kweni ni Jua ndilo linalozunguka Dunia?Wakati Joshua anapigana vita, Mungu alimwambia Joshua simamisha jua, hakumwambia asimamishe dunia.
Shukrani mkuu jibu sawiha kabisa.Hakutakuwa na mabadiliko makubwa kihisia kwa abiria waliondani ya hiyo JET kwani chombo hicho kitakuwa bado ndani ya mvuto wa Dunia na hakingeweza kuathiri kitu kama wakati au nafasi kwa kiwango kikubwa.(MFANO NI ULE WA UKIWA NDANI YA LIFTI NA UKAWA UNATAKA KUPAA). Ni kama tu kuzunguka Dunia haraka zaidi kuliko ilivyo kawaida.
Labda Kwa mujibu wa nadharia za Einstein za uhusianifu, iwapo chombo hicho kingeweza kufikia kasi karibu na ile ya mwanga, kungeweza kutokea athari kama za kupinda kwa muda (time dilation), ambapo muda ungeonekana kupita polepole kwa abiria wa chombo hicho ikilinganishwa na wale walioko duniani. Lakini kwa kasi ndogo za jet, athari hizi hazitakuwa kubwa.
Kama nimfuatiliajibwa movie kama uliwahi ona series moja inaitwa
The Flash. Kuna majibu ya hili swali lako ndani ya ile series.
Sijui umepata kitu.? Ahsante
Kweli kabisa. Sisimizi ukimuuliza mpira una umbo gani atasema tambarareUjinga hujaelewa geography rudi shule
Dunia inazunguka
Mfano ukichukua mpira wa miguu ukaweka sisimizi juu ya mpira kisha uzungushe mkononi sisimizi hawezi Anguka chini
Binadamu na maji yote uyaonayo ya mito na bahari ni kama kisisimizi tu kwenye tufe la dunia ndio maana hata likizunguka hatuwi kichwa chini miguu juu na kudondoka kama sisimizi tu ukiweka juu ya mpira wa miguu atabaki wima tu
Kwa ufafanuzi wako kwa huo mfano mdogo umebeba majibu ya kisayansi kwa swali la mtoa hoja, kwa hiyo jibu hili limeifunga mada.Dunia inazunguka pamoja na kilichopo juu ya ardhi, ni sawa na kusema nzi akiwa ndani ya ndege akataka kuruka kutoka siti ya nyuma kwenda siti ya mbele atashindwa kufika kwa vile ndege inakimbia kwa kasi sana, Hapana si kweli huyo nzi atafika vizuri tu sababu ndege inayembea na yeye anatembea hayupo excluded. Ndivyo ilivyo kwa helikopta hiyo uliyoitolea mfano. Ngoja wanafizikia waje wakufafanulie kitaalamu zaidi.