Swali kwa wasomi wa Jiografia na Fizikia wenye akili zao, kama ulienda shule kukariri pita mbali

"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi; kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karubuni
Basi linatembea kwa spidi 60 kwa saa, nzi anaruka toka kiti cha nyuma kwa spidi ndogo sana na kwenda kutua kiti cha mbele, kwanini nzi huyu asingezidiwa spidi na kujigonga kwenye kioo cha nyuma ya basi.
 
Tena waambie kile tunachoambiwa ni bara la barafu(Antactica) ni ukuta wa barafu aliouweka Mungu kuzuia maji yaliyo tambarare yasi over flow. Na kule hakufikiki tungeweza kufahamu kilichopo mbele zaidi. Ila tubaki tu kuamini uumbaji wa Mungu alioufanya,ambao unakinzana kabisa na sayansi tuliyokaririshwa mashuleni. Dunia ni flat na haizunguki.
Pamoja na kudhani hakufikiki kwenye ukuta huo lakini ndege zinaruka juu ya huo ukuta.
Kuhusu jua, tuamini kuwa yapo majua mengi yanatoka mashariki na kutumbukia magharibi!
 
Eti jua ndio asili ya maji
Jua na mwezi vimeumbwa na Mungu baada ya hayo maji kuwepo na kutngamishwa. Na ni Mungu aliyesema pawepo na mianga miwili mkubwa! Mmoja utawale mchana na mwingine utawale usiku.
 
😄

😄 Mfano mzuri wape hii!! Tuonavyo linapochomoza mashariki kwenda magharibi ni kama tunaona kama linazama chini. Je linazungukia chini Ili liibukie tena mashariki? Jibu ni hapana! Itoshe kusema linazunguka clockwise. Hivyo dunia imesimama tuli kama plate ya saa na jua linazungukia juu ya Dunia kama mshale wa saa unavyozunguka juu ya plate ya saa yenyewe.
Likizungukabhivyo kisha tunaona Giza ? Manake si liko juu ya Dunia Giza linatokea wapi
 
Jua na mwezi vimeumbwa na Mungu baada ya hayo maji kuwepo na kutngamishwa. Na ni Mungu aliyesema pawepo na mianga miwili mkubwa! Mmoja utawale mchana na mwingine utawale usiku.
Vyema sana mkuu, pia kuhusu mwisho au ukingo wa dunia, kwanza kabisa watu wajue kwamba ndege haziruhusiwi kufika huko, na ule ukuta hakuna aliye fanikiwa kuvuka.

Endapo watu watavuka, basi watakutana na ardhi nyingine, mabara mengine ambayo yame zungukwa na Glass Dome.
 
Ni kama Mr Ebbo alivotudanganya kwenye wimbo Mi Mmasai.

Eti alipanda Landrover akawa anaruka juu, akapandisha mori akaruka sana gari ikamuacha.

Jeez,

Newtons 1st Law of Motion hairuhusu hii kitu.
Hii mbona inawezekana ukiwa juu ya pickup au lorry au....😂😂
 
"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi; kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Ndege zina paa within earth spheres... Hazifiki kwenye space so ni part ya dunia, elewa zones za dunia......
 
Swali lako lina msingi mzuri, lakini kuna sababu kadhaa za kisayansi zinazofanya ndege au helikopta zisifanye hivyo.

1. Ndege, Helikopta, na Atmosphere Vinazunguka Pamoja na Dunia: Dunia inazunguka kwa kasi ya takriban 1,674 km/h kwenye ikweta. Hata hivyo, si Dunia pekee inayozunguka — angahewa, ikiwa ni pamoja na ndege na helikopta, pia inazunguka pamoja na Dunia kwa kasi hiyo hiyo. Kwa sababu ya hili, kama ndege au helikopta itapaa juu, itabaki ikiendelea kusogea kwa kasi ile ile ya mzunguko wa Dunia.

2. Kanuni ya Inertia: Kanuni ya kwanza ya Newton ya mwendo inasema kwamba kitu chochote kilicho katika mwendo kitaendelea katika mwendo huo isipokuwa nguvu ya nje itumike kukibadilisha. Kwa kuwa ndege au helikopta tayari zina mwendo wa kasi ya mzunguko wa Dunia, zinahitaji nguvu kubwa sana ili kuzizuia zisisogee pamoja na Dunia.

3. Uhitaji wa Nguvu za Nje:Ili ndege au helikopta zisitii mwendo wa Dunia, zingehitaji nguvu ya nje (kama vile injini zenye nguvu) ili kuondoa mwendo huo. Hii haifanyiki kwa sababu ni ngumu mno na kinyume na kanuni za fizikia za kawaida.

Kwa hiyo, ndege au helikopta zinapaswa kuruka kwa kawaida ili kufika mahali zinapohitaji, kwa sababu ziko ndani ya angahewa inayozunguka pamoja na Dunia.
vipi ndege ikienda vise versa i mean dunia inazunguka kutoka magharibi kwenda mashariki ndege ikaenda tofauti yani mashariki kwenda magharibi..??
 
H
Dunia inazunguka pamoja na kilichopo juu ya ardhi, ni sawa na kusema nzi akiwa ndani ya ndege akataka kuruka kutoka siti ya nyuma kwenda siti ya mbele atashindwa kufika kwa vile ndege inakimbia kwa kasi sana, Hapana si kweli huyo nzi atafika vizuri tu sababu ndege inayembea na yeye anatembea hayupo excluded. Ndivyo ilivyo kwa helikopta hiyo uliyoitolea mfano. Ngoja wanafizikia waje wakufafanulie kitaalamu zaidi.
Hapa ndipo mwisho wa huu uzi.
 
vipi ndege ikienda vise versa i mean dunia inazunguka kutoka magharibi kwenda mashariki ndege ikaenda tofauti yani mashariki kwenda magharibi..??
Hakuna kitacho badilika Mkuu naomba upitie Mifano kadhaa nimeiweka ..

Au mfano rahisi zaidi ni huu hivi mtu akiwa anatembea ndani ya basi(Bus)lililo kwenye mwendo kutoka mbele upande wa dereva kuelekea nyuma ya basi je mtu huyo atapishana na uelekeo gari linalotembea na yeye akiwa ndani yake.?
 
"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi; kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karubuni
Kwasbabu ya force of gravity
 
Jua na mwezi vimeumbwa na Mungu baada ya hayo maji kuwepo na kutngamishwa. Na ni Mungu aliyesema pawepo na mianga miwili mkubwa! Mmoja utawale mchana na mwingine utawale usiku.
Sayansi inatudanganya kwamba jua ni mkusanyiko wa gesi anuai sijui
Likizungukabhivyo kisha tunaona Giza ? Manake si liko juu ya Dunia Giza linatokea wapi

Likizungukabhivyo kisha tunaona Giza ? Manake si liko juu ya Dunia Giza linatokea wapi
Mbona ni jambo rahisi tu kuelewa kinachojiri hadi kupata usiku na mchana? Kuna picha ya mdau mmoja humu inayoonyesha namna watu wa zama walivyotumia kivuli kuratibu muda! Kwa mfano ule wa plate ya saa(iliyoandokwa namba 1 hadi 12) ilaze flat ukiwa kwenye giza. Kisha chukua torch uizungushe juu ya round ya hiyo plate ya round kubwa ya saa kwa usawa wa kati ya ncha ya kati na round ya nje(kati ya ncha ya kati na namba zinapoandikwa. Utaona kadri torch inavyo zunguka,mwanga wa torch utakuwa unahama location kuanzia usawa wa namba 1 kuzunguka 2.3.4.....12. unaingia tena kuanzia1. Na mwanga wa torch( mfano wa mwanga wa jua) unapohama automatically kule unapotoka panabaki kuwa giza hadi mzunguko utakapopafikia Tena.
 
Na namna Mungu alivyoumba ni kwamba mwanga wa jua ukishapita,mwezi ambao nao upo kwenye mzunguko kuzunguka round table hiyo(Dunia)unapita kumulika kule jua lilipohama kimzunguko.
 
Ni sawa na mwanafunzi amuambie mwalimu athibitishe kwamba binadamu alikuwa sokwe...

Hapo lazima fimbo ihusike
Je! Ni kweli wanadamu tulianza kuwa sokwe kwanza na ndio tukawa binadamu? Jibu ni HAPANA KUBWA. Mungu alituumba tukiwa wanadamu kamili. Tena kwa sura na mfano wake.
 
Hakuna kitacho badilika Mkuu naomba upitie Mifano kadhaa nimeiweka ..

Au mfano rahisi zaidi ni huu hivi mtu akiwa anatembea ndani ya basi(Bus)lililo kwenye mwendo kutoka mbele upande wa dereva kuelekea nyuma ya basi je mtu huyo atapishana na uelekeo gari linalotembea na yeye akiwa ndani yake.?
sio kwamba sielewi ila nataka ueleze how..? kutembea sio kupaa sasa tutumie ndege ama nzi yupo hewani ni kivipi, nafikiri mpk hapo utakuwa umeshaelewa swali!
 
Sawa basi ili uelewe hili unatakiwa kujua kuwa hii issue angahewa na dunia vinatenda kazi kama vile tu bus yaani Na huyo mtu anaekuwa anafanya movement.

Chukua huo mfano wa nzi awe anafanya movement zake kwenye gari linalotembea ndo hivo hivo na kwa ndege zinapokuwa zikifanya movement zake kwenye anga hewa.
 
Attachments

  • samsung 029.gif
    samsung 029.gif
    1.4 MB · Views: 2
Back
Top Bottom